Picha ya mmiliki wa home shopping center

Picha ya mmiliki wa home shopping center

hhhh.jpg
1.gif

MFANYABIASHARA maarufu na Mmiliki wa maduka ya Home Shopping Center(HSC), Said Mohamed Saad, ambaye wiki iliyopita alimwagiwa tindikali maeneo ya Msasani City Mall, jijini Dar es Salaam, sasa yuko Afrika Kusini kwa matibabu zaidi.
Hali yake inadaiwa kuendelea vizuri, lakini kuna uwezekano wa jicho lake moja kutokuona kabisa baada ya kuathirika sana, lakini jicho la pili liko salama.
Wiki iliyopita majira ya saa moja jioni, mfanyabiashara huyo alimwagiwa tindikali na mtu mmoja ambaye hakufahamika na mara baada ya kutenda tukio hilo, mhusika alikimbia huku mlinzi wa eneo hilo akijaribu kumkimbiza pasipo mafanikio baada ya kuteleza na kuanguka.

Hatua hiyo ilitoa mwanya kwa mtuhumiwa kutoroka eneo la tukio kwa kutumia usafiri aina ya pikipiki.

Hapo awali ilidaiwa kuwa Saad alikuwa anaweza kuzungumza japo amefungwa mashine sehemu ya pua kwa ajili ya kumsaidia kupumua.

Matukio ya watu kumwagiwa tindikali yameonekana kushamiri nchini katika siku za hivi karibuni.

Tukio la kumwagiwa tindikali mmiliki huyo wa Home Shopping Centre, limekuja ikiwa ni takribani wiki mbili tangu Sheikh Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, mkoani Arusha, Said Juma Makamba naye ajeruhiwe vibaya usoni kwa kumwagiwa maji maji yanayosadikiwa kuwa ni tindikali majira ya usiku akiwa nyumbani kwake.




HII NDIYO TINDIKALI YENYEWE (SULPHURIC ACID) >>> ANGALIA VIDEO UONE NAMNA GANI ILIVYO HATARI







Hii nchi ni ya ajabu sana Polisi watumia Video ya kwenye Yuotube na JF kumkamata Lwakatare lakini nashangaa sana kama huyu jamaa maelezo yametolewa humu jinsi anavyofanya/alivyofanya uhalifu lakini hakuna hatua zinazochukuliwa kwake yeye na watu wengine waliotajwa kushirikiana naye.
 
Last edited by a moderator:
lakini jamani twende mbele na kurudi nyuma pamoja na yote yanayosemwa na wengine hatujui which is which........
ukiangalia picha yake ya kada juu hapo anaonekana mwenye hadhi na mwonekano wa upole...na huwa wanasema mtenda maovu sura yake huwa kuna namna inamsuta!...lakini naona jamaa sura yake imepoaaaaa!sa sijui ndo Simba mwenda pole....
 
Tushukuru domo lake limebaki salama halijaungua ili aje kulitumia kuwataja wabaya wake na lazima aunganishwe nao kwenye kesi ya kuwadhulumu wa Tanzania.

TUMEANZA NA MUNGU TUTAMALIZA NA MUNGU
 
kwa experience yangu na maswala ya psychological criminology jamaa aliyefanya huo mchezo alikuwa na intention moja tu ya REVANGE yes Revange kwani inaonekana alitaka jamaa wa HSC afeel pain kwa chochote baya ambalo alikuwa anahisi kafanyiwa na jamaa wa HSC
na ndio maana yake alitumia acid hawakutaka kumuua ndio maana walitumia acid ya kumuharibu aidha kumpofua au kuharibu sura

inaonekana mind ya aliyefanya hivyo alitaka jamaa wa HSC afeel pain kwa kila muda atakaojiangalia kwenye kioo, kwa kila muda atavyooga, kwa kila muda atavayovaa nguo

na kufeel pain kwa kila muda atakaokutana na watu...
so kitu kikubwa hapa kinachoonekana ni kuwa inaelekea mtendaji unyama huu ana pain ambayo anahisi imesababishwa na jamaa wa HSC na itadumu kwake the rest of his/her life so akaona bora a share the pain na jamaa wa HSC kwa aina moja au nyingine
 
Safi sana... Huyu mshenz alitakiwa atobolewe macho kabisa..
 
mmesoma yote na kushanga jinsi alivyo umia ila amjasoma mali anazo miliki, jinsi anavyo fanya unya wa kuiba nyara za serikali na kuzipeleka nje na pia biashara ya dawa za kulevya anazo fanya hawa watu ni hatari sana nani wakufunga tukipata utawala dhabiti na wenye nguvu
tuanya kama CHINA tu yaani muhujumu uchumi km huyu ni KUUA KABISA hapo ndipo utakapotokomeza mtandao mzima.
Hivi nani akienda Arabuni kote akaiba km huyu, akalawiti maadui zake km huyu, akaua binadamu eti kwa kujaribu silaha yake na Serikali AKAPONA? hiyo ndio Arabuni na hii ndio Tanzania na huruma zake
 
Pole ndugu,hata kama una madhaifu kama wanavosema waengwana bado hukustahili kufanyiwa ukatili huuAlaaniwe yeyote aliyekufanyia unyama huu na laana hii iwaendee pia wanaofurahia hayo yaliyokukuta.GET WELL SOON MY FELLOW TANZANIAN.
 
What goes around Comes around...

Wangemuogesha kabisa yote tu.
 
Li-acid ikidondokea kwenye meza/mbao jinsi inavyoiunguza fasta,sipati picha eti mtu amebeba kabisa hiyo acid kuja kumwagia binadamu mwenzake?huu ni unyama aiseee......narudia tena hata kama ana makosa kiasi gani,unyama aliofanyiwa ni wa hali ya juu.pole kwa wale wote waliofikwa na masahibu ya kumwagiwa tindikali.Na nyie mnaoshangilia muombe mungu majanga kama haya yasiwakute,kwani yakiwakuta ndio utaona uchungu wake.
 
Li-acid ikidondokea kwenye meza/mbao jinsi inavyoiunguza fasta,sipati picha eti mtu amebeba kabisa hiyo acid kuja kumwagia binadamu mwenzake?huu ni unyama aiseee......narudia tena hata kama ana makosa kiasi gani,unyama aliofanyiwa ni wa hali ya juu.pole kwa wale wote waliofikwa na masahibu ya kumwagiwa tindikali.Na nyie mnaoshangilia muombe mungu majanga kama haya yasiwakute,kwani yakiwakuta ndio utaona uchungu wake.

Kwa hiyo ww huoni uchungu, kwa yale ambayo yeye aliyowafanyia wengine?, Au kwa vile hakuna picha zake hapa jf?.
 
Kwa hiyo ww huoni uchungu, kwa yale ambayo yeye aliyowafanyia wengine?, Au kwa vile hakuna picha zake hapa jf?.

ndio maana nikasema hata kama amefanya mabaya kiasi gani,si jambo jema kumdhuru binadamu mwenzako kwa kiwango hiko.
 
Kwa Jinsi Inavyoonekana Alikuwa Firahuni. hivyo he derseved it.
 
kama ni hivyo M/Mungu amjaalie kifo kabisa kwa maana hana faida Duniani wala Akhera
:Cry::A S-fire1::A S-fire1::A S-fire1::A S-fire1:
 
Back
Top Bottom