Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Moja ya picha ya Magufuli katika kipindi cha uhai wake ambayo ilipigwa wakati akiwa Ikulu akimuapisha Dkt. Bashiru Ally Kakurwa kua Balozi na Katibu mkuu kiongozi Februali 27, 2021
Picha hii ilibeba hisia nzito na kumuonyesha JPM hayupo sawa maana hata siku hiyo baada ya uapisho Magufuli akuongee chochote kile.
Na baada ya hapo mwamba akawa kimya na baada ya wiki kadhaa ambayo ilikuwa March 17, 2021 taarifa za kifo chake zikatangazwa na Serikali kupitia makamu wa Rais Samia kipindi hicho akiwa kwenye nafasi hiyo.
Hakika ilikuwa ni siku ngumu kwa watanzania wengi sana hata mataifa jirani, lakini kuna wale waliofurahia kifo chake.
Endelea kupumzika kwa amani JPM ulioyafanya yanaendelea kuishi. Hadi wale waliokukataa leo wana kukumbuka sana
Na uliwahi kusema Mtanikumbuka! Hakika tunakukumbuka.
Miaka 5 bila Magufuli nchini Tanzania