- Source #1
- View Source #1
Picha hii ya Seneta Edwin Sifuna akiwa amejawa na vumbi si halisi.
Picha hii inayosambaa mitandaoni kuonesha hali mbaya ya barabara za Homabay imeundwa kutumia A.I
Picha hii inayosambaa mitandaoni kuonesha hali mbaya ya barabara za Homabay imeundwa kutumia A.I
- Tunachokijua
- Edwin Watenya Sifuna ni mwanasiasa maarufu wa nchini Kenya ambaye kwa sasa ni Seneta wa Nairobi City County kupitia chama cha ODM ambacho kikochini ya Dkt. Oburu Oginga.Pia ni mmoja wa wanasiasa vijana wenye ushawishi mkubwa katika siasa za upinzani nchini Kenya.
Madai
Kumekuwepo na picha zinazosambaa mtandaoni zikimuonesha Seneta Edwin Sifuna akiwa amejaa vumbi na kudai kuwa mavumbi hayo yametokana na ubovu wa barabara ya Homabay.
Picha hiyo imechapishwa pia na Seneta Sifuna mwenyewe kupitia ukurasa wkae wa X na kuandika;
"Bwana walisema huku Homabay ndio kuna shiny things kumbe ni ukora tu…dust is constant"
Uhalisia wa picha hiyo
Baada ya ufatiliaji wa kidigitali wa kubaini maudhui yaliyo chapishwa kwa akili unde (AI) imebainika kuwa picha hiyo imehaririwa kwenye picha halisi akiwa katika tukio la ushirikishwaji wa umma kwa ajili ya muungano wa linda Mwananchi lililofanyika Aprili, 2026 na kuchapishwa upya, hali ambayo imepelekea picha hiyo kupoteza uhalisia wake.