Kulingana na Mamlaka ya Usalama wa Chakula ya Ireland (
FSAI), kuna aina nyingi za uyoga wa asili unaokua Ireland, kati yake aina 13 ni hatari na zinaweza kusababisha sumu kwenye ini na figo na, hatimaye, zinaweza kuwa hatari kwa maisha.
Amanita phalloides ukijulikana zaidi kwa jina la 'death cap' ni chanzo cha kawaida na hatari zaidi cha sumu kutokana na uyoga.
Amanita phalloides hutoa
Amanitins, sumu zenye nguvu zinazolenga ini kwa kuzuia
RNA polymerase II, kuvuruga usanisi wa protini, na kusababisha kifo cha seli (necrosis).
Idara ya Afya ya Umma ya California (
CDPH) katika taarifa yake ya Desemba 05, 2025 ilitoa tahadhari ya dharura kufuatia mlipuko wa sumu ya 'amatoxin' uliohusishwa na ulaji wa uyoga wa porini.
Idara hiyo inabainisha kuwa kesi zilizothibitishwa zilisababisha uharibifu mkubwa wa ini kwa wagonjwa watoto na watu wazima ikiwemo kifo cha mtu mzima mmoja. Kufikia tarehe 5 Desemba 2025, kesi 21 zilitambuliwa na Mfumo wa Udhibiti wa Sumu wa California (CPCS).
Daktari Erica Pan mkurugenzi wa CDPH na Afisa Mkuu wa Afya ya Umma wa Jimbo alinukuliwa akisema “Uyoga wa
death cap una sumu hatari sana ambayo inaweza kusababisha ini kushindwa kufanya kazi. Kwa sababu
death cap inaweza kuchanganywa kwa urahisi na uyoga unaoliwa kwa usalama, tunashauri umma kutochuma uyoga wa porini kabisa katika msimu huu wa hatari kubwa.”
Uyoga wenye sumu, kama vile uyoga wa
death cap (
Amanita phalloides), unaweza kuchanganywa kwa urahisi na uyoga ambao ni salama kutokana na kufanana kwa muonekano na ladha. Kula uyoga huu kunaweza kusababisha sumu kali. Kupika, kuchemsha, kukaushwa, au kugandishwa kwa uyoga huu hakufanyi kuwa salama kuliwa.
Je, unawezaje kutambua uyoga huu wenye sumu?
Tovuti ya
Mushroom appreciation inaweka bayana sifa za uyoga huo ambazo mtu anaweza kuutambua kama ifuatavyo.
Vinyama au magamba juu ya kofia ya uyoga. Angalia “mabaka” yenye rangi tofauti juu ya kofia. Mabaka haya ni mabaki ya
universal veil iliyokuwa inauzunguka uyoga ukiwa mchanga. Wakati mwingine mabaka haya huonekana zaidi kama mistari ya nukta zilizoinuka.