Naomba Tuweke kumbukumbu sawa kidogo...... Picha hii ni ilipigwa miaka ya 90 kipindi Dr. Slaa anahamia Chadema akitokea CCM, Na huyo Mwenye Kaunda suti ndiye alikuwa mbunge wa kwanza Na pekee kupitia chadema Dr. Aman Walid Kabourou jimbo la Kigoma Mjini, ilikuwa ziara ya kwanza Kwa Dr. Slaa kufika jimbo la Kigoma Mjini kujifunza Na kujionea chadema ilivyo kuwa inafanya vizuri, angalizo langu ni Kwa wote mlioingia chadema kipindi cha uchaguzi wa 2010 kuweni makini Na chadema yenu mnayoivuruga Kwa dhambi ya kubaguana, chadema ni ya watanzania Na si ya tabaka la watu flani...... Kaeni chini muelewane Kama kweli Mna nia ya dhati ya kuwakomboa watanzania.