Kuna wakati ukiwa na Jambo kubwa la Furaha Machozi huwa yanatoka kana kwamba uko kwenye hudhuni nzito, kumbe ni furaha iliyoukamata Mwili wako wote, na kusababisha kumwaga machozi mazito!!!
Huyu Mama yuko kwenye furaha nzito sana!!
Amejaribu kuvuta picha jinsi Mh. Tundu Lissu alivyochungulia kaburi ikiambatana na mateso Mengine mengi!!
1. Kesi za jinai 6 zenye lengo la kumfunga miaka mingi Gerezani = zimefutwa
2. Kupigwa Risasi 16 Mwilini = alipona
3. Kuzuuliwa kugombea Urais TLS = aligombea
4. Kukimbilia uhamishoni kwa Tishio la kuuawa na kuishi nje zaidi ya miaka 5 = amerudi
5. Yule aliyeagiza auawe = alikufa yeye!!
Hayo mambo 5 ndo yanamuliza huyo Mama!!!
Hakika ukitafakari vzr ni lazima machozi yakutoke,
Na hayo ndo Maajabu ya Mungu Muumba mbingu na nchi!!!
COPY & PASTE kutoka kwa mdau mmoja huko kanda ya ziwa.