Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
PICHA HIZI ZA JENGO LA AL JAMIATUL ISLAMIYYA FI TANGANYIKA ZINASEMA MANENO ELFU MOJA
Picha hizo hapo chini za majengo mawili ya Al Islamiyya fi Tanganyika zimekuwa ndani ya Maktaba kwa zaidi ya miaka ishirini lakini zilikuwa picha tu.
Moja katika hizo picha tatu iko kwenye kitabu cha maisha ya Abdul Sykes (1998) lakini ilikuwa picha kama picha nyingine yeyote ile.
Leo picha hizi zikaletwa hapa FB kama, ''Your Memories in Facebook,'' nikawa nazitazama.
Sasa nikawa naangalia picha kwa kuanza na picha moja baada ya nyingine kwa wale ambao mimi niliwafahamu wakati wa utoto wangu hadi nanyanyukia nikiwa kijana na kidogo wengine nikawanao zaidi ya hapo.
Nimeiangalia ofisi ya Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika iliyokuwa uani nyuma ya jengo lenyewe la taasisi hiyo, jengo lililokuwa Muslim School.
Nyumba hii aliishi Ali Mwinyi Tambwe (akiwa Katibu wa Al Jamiatul Islamiyya baada ya Kleist kujiuzulu nafasi hiyo mwaka wa 1940), hii nyumba ilikuwa imeungana na ofisi.
Nikamwangalia Maalim Mohamed Matar katika picha wakati ule kijana.
Picha yake ya ujana nimeiweka hapo chini.
Picha hizi imepigwa katika miaka ya 1930s.
Maalim Mohamed Matar alikuwa akisomesha dini hapo shuleni na mwalimu wa Qur'an na ndiye aliyemuanzisha Abdul Sykes, na wadogo zake wawili Ally na Abbas alif kwa kijiti.
Maalim Matar alikuja akawa rafiki mkubwa wa Abdul Sykes ukubwani kwake na Abdul Sykes alipofariki, Maalim Matar ndiye aliyemkosha akisaidiana na Sheikh Kassim Juma.
Naendelea kumwangalia Maalim Matar na mengi katika mambo yaliyomfika ya kukamatwa na kufungwa jela Zanzibar baada ya mapinduzi yananijia.
Yananijia mazungumzo yangu na Kleist Abdulwahid miaka mingi nyuma akinieleza simanzi iliyompata baba yake, Abdul Sykes aliposikia kuwa mwalimu na rafiki yake Maalim Matar kakamatwa na kapelekwa jela Zanzibar.
Ilimshangaza Abdul Sykes ni sababu gani Maalim Matar atakamatwa ilhali Maalim Matar hakupata katika maisha yake kujihusisha na siasa yoyote si Tanganyika wala Zanzibar.
Baadae ikasikika kuwa kulikuwa na watu wanaomba dua serikali ya Karume ianguke.
Katika kamatakamata ya wavutaji nyuradi Maalim Matar akasombwa maana yeye muda wote ana tasbih mkononi anamsabih Mola wake.
Maalim Matar (nyuma wa kwanza kushoto), Kleist Sykes, Ali Mwinyi Tambwe na Abdul Sykes niliowataja mpaka hapa watafute kwenye picha.
Abdul ni huyo mtoto mdogo mwanafunzi wa shule ya msingi hapo Muslim School hapo kwenye picha kavaa koti na kofia ya tarbush.
Baba yake, Kleist Sykes yuko pia kwenye hiyo picha mtafute.
Nakumbuka siku nilipokwenda nyumbani kwa Ali Mwinyi Tambwe wakati natafiti kitabu cha Abdul Sykes.
Ali Mwinyi aliniambia, "Mimi mkubwa sana kwa Abdul na Ally nikiwaona wanakuja sala ya Maghrib Msikiti wa Kitumbini wameshikwa mikono na baba yao."
Mwangalie Ali Mwinyi Tambwe umri wake na mtazame Abdul Sykes uone walivyopishana umri.
Katika uongozi wake Kleist akiwa Katibu na Mzee bin Sudi, Rais ndipo majengo hayo yakajengwa na Muslim School kuanzishwa.
Allah aliwakutanisha hawa watu watatu Maalim Matar, Ali Mwinyi Tambwe na Abdul Sykes miaka mingi baadae katika historia ya kusisimua wakati Tanganyika inadai uhuru wake miaka ya 1950.
Ali Mwinyi Tambwe alikwenda Nansio, Ukerewe na Abdul Sykes mwaka wa 1953 wakati huo Abdul ni Katibu na Kaimu Rais wa TAA kukutana na Hamza Mwapachu kupata kauli yake kuhusu kumtia Julius Nyerere katika uongozi wa juu wa TAA na mwaka unaofuatia, 1954 iundwe TANU na Nyerere aongoze harakati za kudai uhuru wa Tanganyika.
Ali Mwinyi Tambwe mwaka wa 1964 atahusika katika mapinduzi ya Zanzibar yaliyopelekea baadae Maalim Matar akamatwe Dar es Salaam kusafirishwa Zanzibar na kufungwa jela ambako aliteswa sana.
Jengo la Al Jamiatul Islamiyya lilimaliziwa ujenzi na Aga Khan, Patron wa EAMWS mwaka wa 1936 baada ya kuona juhudi za Waislam kutaka kujenga shule.
Safari ya kwanza ya Julius Nyerere kwenda UNO mwaka wa 1955, hafla ya kumuaga ilifanyika katika jengo hili.
Jengo hili lililobeba historia kubwa ya ukombozi wa Tanganyika limechukuliwa na serikali baada ya kuvunjwa kwa EAMWS na kuundwa BAKWATA mwaka wa 1968 na ingawa jitihada nyingi zimefanyika kutaka lirejeshwe kwa Waislam jitihada hizi hazijafanikiwa.
Maisha ya wazalendo niliowataja yamebeba mengi katika historia ya uhuru wa Tanganyika.