Picha za Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika zimebeba historia kubwa

Hawana ujanja wowote mbali ya kupenda kudhulumu kutokana na kutofuata dini takatifu.
Ukiona upole wa waislamu unaodumisha amani ni sababu ya kufundishwa kuwa na subira.

Siamini katika kudhulumiwa. Naamini katika competence ya mtu. Haya yanayosemwa si kweli. Hakuna anayenyimwa kuabudu Tanzania. Sijafanya kazi serikalini ila najiuliza kwani lazima muwe wakurugenzi na mawaziri kuleta impact?
Dunia ya sasa ni pana na ina mambo mengi. Kusema siasa ndio pekee itamkomboa mtu ni kujidanganya nafsi. One of the unique ways that make some socities, no matter how small there numbers are, continue evolving, is there ability as a society to do self reinvention.
 

Kwahiyo Shekhe Mohammed, leo kwa mfano serikalini waislam wakawa asilimia 80, mambo yenu yatakuwa sawa?
Naogopa sana mtu anayeidanganya nafsi yake mwenyewe.
Sifanyi kazi serikalini na kusema kweli sio lazima. Hata watoto wangu nawafundisha ukweli kuwa Dunia hii ni pana sana. Watafute maarifa. If they opt to narrow their minds, they should not blamed anybody.
Kama society haijaweza kujitambua na kutambua nini malengo ya maisha yao hapa duniani, hata tuwape nafasi gani bado watalalamika wanaonewa.
Sikubaliani na wewe kabisa unaposema waislamu wanazuiwa kuabudu. Wapi? Na kwanini?
Kuna sehemu wamejenga msikiti wakakatazwa kuabudu? Au wamechukua jengo ambalo hawana mahesabu nalo wakakatazwa.
 
Ndahani,
Nadhani umeingia katika mjadala huu ukiwa umeshasonga mbele sana kwa hiyo huelewi maudhui yake.
Ikiwa una haja ya kufanya mjadala na mimi sasa itakubidi uanze mwanzo usome nini mimi na wengine tumeandika.

Hakuna popote nimezungumzia suala la kuabudu.

Lakini kwa haraka na wepesi unaweza kuanza na hizo takwimu za mgawao wa nafasi kama zilivyoandikwa na Shura ya Maimamu.
 
Wewe inaonekana ni mtu wa kuropoka na kweli hauko serikalini na jengine umezoea kuwatukana waislamu na huwajui waislamu ni nani katika hii Tanzania angalau kabala mtazamo mpana wa dunia,
Mfano wa matusi yako kwa waislamu unapatikana hata kwenye hiki kipande kifupi ulichoandika.Unaposema mkiwa asilimia 80 ndio mambo yenu yatakuwa sawa?.Mambo yetu sisi kama nani kwako.Wewe kwa mtazamo wako huna sifa ya kuwaambia waislamu ni narrow minded na waislamu upana wa mawazo haufundihiwi na wewe na wala mtu mwengine yoyote.Upana wa mawazo ya waislamlu unapatikana katika Qur'an na sunna za Mtume Muhammad s.a.w.
Ukija upande mwengine uliogusia hapo kwa ujinga wako ni kuwa unadhani maendeleo ya waislamu yamekosekana si kwa sababu ya uchache wao serikalini na kubaguliwa isipokuwa ni asili ya maumbile yao.Hili halikubaliki.Iwapo Mwenyezi Mungu kwa uadilifu wake anawapa nyinyi mnaomkufuru atashindwaje kutupa sisi tunaomuabudu kisawasawa.Na kwa maneno yake anapotupa tukamshukuru basi hutuongezea zaidi na zaidi.
Kwa mtazamo wako usiozingatia elimu ya kiislamu unadhani ibada kwa waislamu iko misikitini tu na ukiona misikiti imeongezeka unataka waislamu wasilalamike kwa jengine ambalo wanazuiwa kulitekeleza katika ibada.Huelewi kuwa kuwajengea watu wa jamii fulani uwezo wa kiuchumi na kuwaajiri kwa wingi serikalini kuna uhusiano mkubwa na ukandamizwaji wa kiimani.Kwani watakaokuwa wakifaidi jasho la wenzao zao ndio watakaokuwa na jeuri ya kuwakandamiza na kuwafanya wengine wadharaulike mitaani.
 

Chonde chonde. Msilazimishe mambo ambayo hayapo.
Tanzania ni yetu sote. Mnapotaka nyinyi mpewe special preference mnatumia kigezo gani? πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 

Kuna siku Mama alisema mwanga mpe mwanao akulelee. JK angelijaribu kujenga msikiti wa Bakwata kama ushawishi au ufuatiliaji kama JPM angeitwa mdini.
Tunapoongea haya mambo tuwe na kiasi. Sio rahisi kufanyika kama mnavyotaka.
Nashauri kama nia ni kuongoza kwa wingi, wekezeni kwenye elimu bora na uadilifu. Tanzania inahitaji watu waadilifu wenye elimu bora na si vinginevyo.
 
Chonde chonde. Msilazimishe mambo ambayo hayapo.
Tanzania ni yetu sote. Mnapotaka nyinyi mpewe special preference mnatumia kigezo gani? πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Kauli nzuri ya chonde chonde Tanzania ni yetu sote.Lakini hii huwa kiuhalisia inahusu pale waislamu wanapokandamizwa wakae kimya .Inapokuja kutoa fursa sawa basi waislamu haiwahusu. Inakuwaje unachagua baraza la mawaziri wote wakristo isipokuwa watatu na wabunge wote wakristo isipokuwa wachache halafu useme chonde chonde.
 
Kwani viongozi Tanzania ni wangapi wote.Na jee waislamu wenye elimu kuliko yako ni wangapi.Hii ni kabla hata ya uwekezaji wowote mwengine.
 
Ndahani,
Miradi mitatu ya elimu imehujumiwa Tanzania na laiti serikali ingeruhusu miradi hiyo leo tusingekuwa hapa wewe unahimiza Waislam wathamini elimu.

Unazungumza hapa mambo usiyoyajua.

1968 mradi wa ujenzi wa Chuo Kikuu kilichokuwa kinajengwa na EAMWS ulihujumiwa kwa EAMWS kupigwa marufuku na kuundwa BAKWATA.

1970s serikali iliwakatalia IOC kujenga Chuo Kikuu Tanzania chuo hicho kikajengwa Mbale, Uganda.

1980s Darul Imaan ilihujumiwa isijenge Shule ya Ufundi Kibaha.

Haya nimeyarudia kukukumbusha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…