Picha za Mzungu anayemiliki Tigo Tanzania

makandemoja

Member
Joined
Apr 17, 2016
Posts
57
Reaction score
48
Habari wana Jamvi!

Dada Cristina Mayville Stenbeck mwenye umri wa miaka 39 (Asili yake Sweden) ndio mmiliki halali (Chairman and principal owner) wa kampuni ya Investment AB Kinnevik. Kampuni hio inafanya biashara za Holding ambapo inamiliki makampuni kadhaa makubwa kama Zalando, Millicom, Tele2, Rocket Internet, Global Fashion Group and MTG.

Millicom international cellular SA inayofanya biashara zake hapa nchini kama MIC Tanzania Limited kupitia jina la bidha yake kubwa ijulikanayo kama Tigo ndio mtandao wa pili kwa ukubwa Tanzani wenye wateja zaidi ya milioni 7. Zaidi ya 46% ya wateja wake wanatumia MFS(Metropolitan Fiber Systems).

Kama umesajiliwa na Daresalaam Stock Exchange kama muwekezaji halali kwenye kampuni ya Tigo Mic (T) Ltd, Basi utakumbuka Ngwe ya pili ya mwaka 2014(Q2 2014) soko la hisa lilifikia 29.8% ambapo kwa Ngwe ya pili ya mwaka huu wa 2016 (Q2 2016) mapato yamegonga kwenye $1.57B zilizogawiwa kwa waliowekeza(investors) kulingana na wingi wa hisa zao.

Japo kua kwa sasa Tigo ndio inayomiliki Zantel kwa 85% lakini report kutoka makao makuu sweden report inaasema nchi zote za Africa zilizo na mtandao wao wa tigo zina report nzuri ya ukuaji wa biashara yao(Organic growth) ipokua kwa Tanzania tu wanapata wakati mgumu kibiashara na report sio nzuri.

Makala hii ni ya uchumi na biashara japo inaeza kukaa popote kwa sababu mchambuzi ni mwanauchumi msela.

kama unaswali uliza!

 
Unafikiri kwanini kwenye nchi ya Tz tu ndo wanapata ugumu wa kibiashara?
 
Unafikiri kwanini kwenye nchi ya tz tu ndo wanapata ugumu wa kibiashara..?

Organic Growth kwa upande wa Tanzania hali sio nzuri kutokana na mazingira ya uwekezaji kutokua rafiki.
 
Duh! sasa mkuu hiyo heading hata ukiangali wewe binafsi huoni imekaa ndivyo sivyo? kwa jinsi ulivyoandika hapo inatafsiri kunatolewa huduma nyengine kbs tofauti na tigo kama mtandao! kumbuka maneno yanatafsiri zaidi ya moja....
 
Hata aliyebadili bado heading inaleta utata. Angeandika "PICHA ZA MMILIKI WA MTANDAO WA SIMU ZA MKONONI TIGO"
 
Haya tumepata taarifa. Na wewe una share humo lakini?Maana umepigia chapuo kweli kweli.Love it,live it.Dah,kweli wajinga ndio waliwao,watu wanakufanya kuwa ndondocha halafu wanakuambia "Love it." Kazi kweli kweli.
 
unafikiri kwanini kwenye nchi ya tz tu ndo wanapata ugumu wa kibiashara..?
Hakuna lolote,Wanasingizia ugumu kwa sababu mfumo wa tz wa ulipaji kodi ni manual,yaani we ukilalama unapata hasara basi serikali inakuonea huruma hivyo unalipa kodi utakavyopenda.

Wewe una wateja zaidi ya milioni 7 yaani wateja milioni 2 wakiweka 500 kwa siku tu una B Moja.....Yaani wana uhakika wa kuingiza zaidi ya B 30 kwa mwezi kisha wnaleta bla bla.
 
Amerithi kutoka kwa Babu Yake ,so hana jipya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…