Picha za Trump na Flaviana Matata Zaibua Mambo Bongo
Mgombea urais tajiri wa Chama Cha Republican, Donald Trump akiwa nna mwanamitindo wa kimataifa wa Tanzania, Flaviana Matata (kulia) na Miss Albania 2010, Angela Martini (kulia).
DAR ES SALAAM: Zikiwa zimesalia takriban siku 53 kufika Novemba 8, mwaka huu, siku ya Uchaguzi wa Urais wa Marekani, picha za mmoja wa wagombea wake kutoka Chama Cha Republican, Donald Trump na mwanamitindo wa kimataifa wa Tanzania, Flaviana Matata zinazowaonesha ‘live’ kwenye redcarpet zimeibua mambo, Ijumaa linafunguka.
DONALD NA FLAVIANA
Donald Trump ni mgombea urais tajiri ambaye ni mfanyabiashara aliyefanikiwa duniani na mwenye kauli tata dhidi ya wageni na matajiri wenzake nchini Marekani huku Flaviana Matata akiwa ni binti wa Kitanzania aliyetwaa Taji la Miss Universe Tanzania 2007. Akiwa mmoja wa mamodo wa kimataifa wenye mafanikio Bongo, Flaviana ambaye ni Mkurugenzi wa Flaviana Matata Foundation (FMF) kwa sasa anaishi na kufanyia kazi zake za kutangaza mavazi huko New York nchini Marekani, akiwa amepitia lebo nyingi kubwa za mavazi za nchini humo.
Donald Trump akimbusu Miss Albania 2010, Angela Martini na Flaviana Matata akishangaa.
SOURCE; MUUNGWANA BLOG