Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,897
- 6,925
Blocks zenye mfereji katikati (grove) kwa rinta nyumba ya kawaida ya kifamilia
Katika ujenzi wa nyumba za kawaida za kifamilia tumekuwa na kasumba ya kuingia gharama kubwa za ujenzi kwa kutumia umiminaji wa rinta ghali sana kana kwamba nyumba itabeba uzito wa kuchukua floor nyingine juu yaani ghorofa. Nyumba ya kawaida haina haja ya kumimi rinta nzito sana ila inawezekana kuwa na bloks zenye grove katikati na hapo zikawekwa nondo kuzunguka kisha kumimina zege, gharama yake ikawa nafuu na ujenzi kwenda kasi zaidi badala ya huu wa gharama kubwa za kumimina rinta na mbao nyingi ni mtindo wa kizamani zaidi na hugharibu zaidi.
Solid blocks kwa ujenzi wa msingi wa nyumba
Ujenzi wa nyumba hauhitaji zile blocks ambazo ni solid isipokuwa kwenye msingi (foundation), ili kupunguza gharama hizi blocks ambazo zina tundu au matundu katikati ni gharama nafuu na pengine hupunguza uzito kwa ujenzi wa ghorofa.
Ujenzi wa kuta/partition ndani ya nyumba kugawa vyumba hauhitaji blocks nene na nzito, zinahitajika nyembamba na zenye tundu zaidi kupunguza gharama.
Huu ni ushauri tu ili kuondokana na gharama zisizo muhimu katika ujenzi.
Kuta za ndani ya nyumba kutenga vyumba si lazima kujenga kwa kutumia maofali au blocks, inawezekana kabisa kutumia mbao na vyumba vikaonekana pengine nadhifu zaidi.