Pierre a.k.a Konki Fire na Mungu asiye na mipaka

MTAZAMO

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2011
Posts
19,675
Reaction score
33,583
Wakuu,

Kwa tafakari fupi kupitia mfano wa kijana Pierre a.k.a Konki Fire.

Mungu ni wa ajabu sana, na hakuna mtu aliyefikia viwango vya kumfahamu kikamilifu. Wakati mwingine tupo baadhi ambao tunambinafsisha kuwa anatenda kwetu/kwako sababu umeokoka au mkristo mzuri sana.

Sisemi kuokoka au kuwa Mkristo safi sio standard rasmi za kukutana na Mungu bali tusimuwekee Mungu mipaka kwasababu ni Mungu. Ndio maana wakulima wote bila kujali dini zao hali zao kiroho wanapata mvua na jua kwa wakati ulio sawa.

Hebu angalia, huyu kijana maarufu kwasasa Pierre a.k.a Konki fire, video ya kwanza iliyompa umaarufu haikuwa video njema bali kwa jicho la kawaida ilibeba aibu na kila namna ya ulevi wa kupindukia na aibu hata kwa familia yake.

Dhihaka, hukumu na kila ubaya wa video ile umegeuka kuwa neema na baraka kwa kijana huyu. Hili linahitaji tafakari sana badala ya kulichukulia kwa wepesi.

Wangapi wamesugua goti milango ya baraka za fedha zifunguke lakini bado wapo kwenye msoto huku Pierre akipata baraka tena kutokea kwenye tukio la fedheha?

Huyo ndio Mungu, anajua kilichomo ndani mwa kila mtu hata muokota makopo mtaani mwako. Hujui Pierre amebeba nini kilichofanya Mungu ageuze ile fedheha kuwa baraka.

Sina lengo la kukatisha tamaa waombaji, lengo langu ni kusisitiza Mungu hana mipaka. Sasa wewe ukitaka uache maombi ukitegemea upate bahati kama ya Pierre utakufa bila kufikia ulipopangiwa.

Nimekumbuka msemo wa Jamhuri Kihwelo "Julio" kuwa Mungu habagui ndio maana akamchukua Nyerere lakini katuachia vichaa kibao barabarani.

Karibuni kwa tafakari zaidi ....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mihogo aliikimbilia kei akiamini ni bora kuliko watu wake bahati kei ikamlipa!! Ingawa ilikua fedheha lakini ndio ilimtoa the same to piere! Shetani huwalipa watu wake pia!!

Kinyesi kimemfwata aliko vipi atakimbia?
 
Na wewe ni walewale wanaomchukulia Mungu kama Mjomba wao.

Acha dhihaka kwa Mungu aisee...

Kitu gani cha kumtukuza Mungu huyo Pierre amefanya?

Mwishowe utakuja sema hata makahaba na madrug dealer wamebarikiwa na Mungu.
Ndio hiki ninachosema, unaweza usione utukufu wa Mungu kwasasa lakini tusihukumu. Inawezekana Pierre aliyekuwa mlevi asiyejielewa akabadilishwa na status yake mpya na mwisho ukauona huo utukufu "unaoutaka".

Mafanikio ya Pierre yapo wazi, mfano huu usingefaa kwa watu ambao hatufahamu vyanzo vyao vya fedha kama drug dealers.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Una uhakika kila pesa/mafanikio anayopata mtu yanatokana na Mungu....?? Sasa watu kwa waganga wanafuata nini...? Mtu akiwa malaya akafanikiwa kwa kupata pesa ni neema..??
 
Una uhakika kila pesa/mafanikio anayopata mtu yanatokana na Mungu....?? Sasa watu kwa waganga wanafuata nini...? Mtu akiwa malaya akafanikiwa kwa kupata pesa ni neema..??

Sent using Jamii Forums mobile app
Hao wamepata pesa kupitia uovu. Pierre kwasasa anapata pesa kupitia njia halali kabisa tena kwa kibwagizo very simple.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na wewe ni walewale wanaomchukulia Mungu kama Mjomba wao.

Acha dhihaka kwa Mungu aisee...

Kitu gani cha kumtukuza Mungu huyo Pierre amefanya?

Mwishowe utakuja sema hata makahaba na madrug dealer wamebarikiwa na Mungu.
Jambo asilolijua hata
shetani huwa anafanya, matendo na baraka zake kwa watu na wafuasi wake!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kwa mtazamo wako,
upo sahihi
lakini katika swala la ki Imani na Mungu.HAUPO SAWA!

Soma neno la Mungu uta,note mengi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kwa mtazamo wako,
upo sahihi
lakini katika swala la ki Imani na Mungu.HAUPO SAWA!

Soma neno la Mungu uta,note mengi

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndio maana nikasema tusimuwekee Mungu mipaka. Pengine hujui safari ya Pierre inaelekea wapi. Nimejifunza kuacha kukimbilia kumpa shetani sifa kwenye mambo ambayo yapo kwenye mtiririko wa mpango wa Mungu.

Kama nilivyosema hapo juu, nimemtumia Pierre kama mfano wa safari ya maisha na jinsi mafanikio yanavyokuja kwa mtu.

Siwezi kuusemea moyo wa Pierre lakini huwezi jua anamshukuru Mungu kwa viwango gani kwa hapo alipomuweka. Pengine safari yake halisi ndio anaianza. Tumuombee tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukristo na utajiri ni vitu viwili tofauti. Ukristo ni dini ya watu masikini, haihusiani na utajiri hata kidogo.
 
Acha kumfananisha Mungu na vitu vya kipuuzi yaani unafikiri Mungu akitaka kumuinua mtu anashindwa katika njia nzuri na zenye maadili? Huyo mungu wako wa bar labda

Mungu ni Mtakatifu na huwa katika utakatifu labda itokee siku pierre amebadilika na kua mfano bora katika jamii lakini kwa haya anayofanya na kuyahusisha na Mungu nafikiri hata wewe unamthihaki huyo Mungu unaojifanya unamuabudu
 
Umaarafu wa Pierre Kondi Ni kielelezo tosha kwa watanzania wanapenda na kuvipa vipaumbele vitu vya kijinga kuliko vitu vya maana.
Yaani mtu "MLEVI WA TAIFA" amepata tu umaarufu kwa ulevi wake na kupiga kelele.

Waliosema usidharau nguvu ya wajinga wengi walikuwa na maana Sana

Watanzania wengi walioko mitandaoni Ni wajinga na wemempa mjinga mwenzao umaarufu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Konk fire hakuna jambo la aibu alilofanya kwanza utambue pombe inaongeza mapato kwa taifa cha pili ni starehe kama starehe zingine cha tatu ajavunja katiba ya nchi cha nne kila jambo ukilifanya kwa mafanikio lazima utusue Pierre kafanikiwa kwa kutumia pombe pia ni mlipa kodi mzuri..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…