MTAZAMO
JF-Expert Member
- Feb 8, 2011
- 19,675
- 33,583
Wakuu,
Kwa tafakari fupi kupitia mfano wa kijana Pierre a.k.a Konki Fire.
Mungu ni wa ajabu sana, na hakuna mtu aliyefikia viwango vya kumfahamu kikamilifu. Wakati mwingine tupo baadhi ambao tunambinafsisha kuwa anatenda kwetu/kwako sababu umeokoka au mkristo mzuri sana.
Sisemi kuokoka au kuwa Mkristo safi sio standard rasmi za kukutana na Mungu bali tusimuwekee Mungu mipaka kwasababu ni Mungu. Ndio maana wakulima wote bila kujali dini zao hali zao kiroho wanapata mvua na jua kwa wakati ulio sawa.
Hebu angalia, huyu kijana maarufu kwasasa Pierre a.k.a Konki fire, video ya kwanza iliyompa umaarufu haikuwa video njema bali kwa jicho la kawaida ilibeba aibu na kila namna ya ulevi wa kupindukia na aibu hata kwa familia yake.
Dhihaka, hukumu na kila ubaya wa video ile umegeuka kuwa neema na baraka kwa kijana huyu. Hili linahitaji tafakari sana badala ya kulichukulia kwa wepesi.
Wangapi wamesugua goti milango ya baraka za fedha zifunguke lakini bado wapo kwenye msoto huku Pierre akipata baraka tena kutokea kwenye tukio la fedheha?
Huyo ndio Mungu, anajua kilichomo ndani mwa kila mtu hata muokota makopo mtaani mwako. Hujui Pierre amebeba nini kilichofanya Mungu ageuze ile fedheha kuwa baraka.
Sina lengo la kukatisha tamaa waombaji, lengo langu ni kusisitiza Mungu hana mipaka. Sasa wewe ukitaka uache maombi ukitegemea upate bahati kama ya Pierre utakufa bila kufikia ulipopangiwa.
Nimekumbuka msemo wa Jamhuri Kihwelo "Julio" kuwa Mungu habagui ndio maana akamchukua Nyerere lakini katuachia vichaa kibao barabarani.
Karibuni kwa tafakari zaidi ....
Sent using Jamii Forums mobile app