Pierre a.k.a Konki Fire na Mungu asiye na mipaka

Pierre a.k.a Konki Fire na Mungu asiye na mipaka

Wapo watu unaweza kuwahukumu kwa akili zako lakini hujui amebeba nini! Hujui Mungu anampango gani nae ...Soma hii kutoka kwa mdau lauzi96 nanukuu ..

"Halafu huyo piere ana bahati sna muacheni atusue tu alishaanguka na ghorofa keko kutoka ghorofa ya 5 kashuka nalo mpaka chini na hakuchunika hotel ilikuwa inaitwa chang'ombe village wala hajaruka alikuwa floor ya juu kabisa."

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunatambulika kwa mungu kutokana na matendo yako na imani yako!
Watu wanadhani ukiwa sijui umeokoka! Mungu atakuwa anakuangalia ww tuu. kisa? Umeokoka, unakesha makanisani, lakini Kumbe Mungu hachagui anaangalia imani yako kwake!
 
Wakuu,

Kwa tafakari fupi kupitia mfano wa kijana Pierre a.k.a Konki Fire.

Mungu ni wa ajabu sana, na hakuna mtu aliyefikia viwango vya kumfahamu kikamilifu. Wakati mwingine tupo baadhi ambao tunambinafsisha kuwa anatenda kwetu/kwako sababu umeokoka au mkristo mzuri sana.

Sisemi kuokoka au kuwa Mkristo safi sio standard rasmi za kukutana na Mungu bali tusimuwekee Mungu mipaka kwasababu ni Mungu. Ndio maana wakulima wote bila kujali dini zao hali zao kiroho wanapata mvua na jua kwa wakati ulio sawa.

Hebu angalia, huyu kijana maarufu kwasasa Pierre a.k.a Konki fire, video ya kwanza iliyompa umaarufu haikuwa video njema bali kwa jicho la kawaida ilibeba aibu na kila namna ya ulevi wa kupindukia na aibu hata kwa familia yake.

Dhihaka, hukumu na kila ubaya wa video ile umegeuka kuwa neema na baraka kwa kijana huyu. Hili linahitaji tafakari sana badala ya kulichukulia kwa wepesi.

Wangapi wamesugua goti milango ya baraka za fedha zifunguke lakini bado wapo kwenye msoto huku Pierre akipata baraka tena kutokea kwenye tukio la fedheha?

Huyo ndio Mungu, anajua kilichomo ndani mwa kila mtu hata muokota makopo mtaani mwako. Hujui Pierre amebeba nini kilichofanya Mungu ageuze ile fedheha kuwa baraka.

Sina lengo la kukatisha tamaa waombaji, lengo langu ni kusisitiza Mungu hana mipaka. Sasa wewe ukitaka uache maombi ukitegemea upate bahati kama ya Pierre utakufa bila kufikia ulipopangiwa.

Nimekumbuka msemo wa Jamhuri Kihwelo "Julio" kuwa Mungu habagui ndio maana akamchukua Nyerere lakini katuachia vichaa kibao barabarani.

Karibuni kwa tafakari zaidi ....

Sent using Jamii Forums mobile app
Waafrika acheni upumbavu mungu hayupo ,mvua ni mvuke ulioganda ,pandeni miti lindeni mazingira mtapata mvua ,na hata zikitokea hazinyeshi fanyeni kilimo cha umwagiliaji msiombe hakun wa kumuomba,fanyeni kazi
 
Na wewe ni walewale wanaomchukulia Mungu kama Mjomba wao.

Acha dhihaka kwa Mungu aisee...

Kitu gani cha kumtukuza Mungu huyo Pierre amefanya?

Mwishowe utakuja sema hata makahaba na madrug dealer wamebarikiwa na Mungu.

yaani imebidi nishangae Mkuu pamoja na kusoma uzi mara mbili mbili, doh kweli watu tunatofautiana kwenye fikra
 
Una uhakika kila pesa/mafanikio anayopata mtu yanatokana na Mungu....?? Sasa watu kwa waganga wanafuata nini...? Mtu akiwa malaya akafanikiwa kwa kupata pesa ni neema..??

Wapo Wengi waliofanikiwa kupitia bihashara hii ya kuuza viungo vyao vya harusi na wanapiga hela zakutosha tu.....ila ukiangalia kwa jicho la pili hiyo ni laana na ni dhambi kwa Maelezo ya diza zote ....hapa ndo uwa najiuliza nn maana kamili ya dhambi na laana kama vipo upande wa Negative au postive??
 
Back
Top Bottom