Pierre Liquid kuongozana na wabunge hadi Misri kuishangilia Taifa Stars

Pierre Liquid kuongozana na wabunge hadi Misri kuishangilia Taifa Stars

Mlachake

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2009
Posts
4,437
Reaction score
4,618

Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amesema wabunge 48 watakwenda kuishangilia timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ katika Fainali za Mataifa ya Afika (AFCON) zinazofanyika nchini Misri wakiambatana na Peter Mollel maarufu Pierre Konki Liquid.

Akizungumza bungeni jijini Dodoma leo Jumanne Juni 18, 2019 Ndugai amesema wataambatana na mchekeshaji huyo katika fainali hizo huku akiwataka wabunge zaidi kujiandikisha ili kwenda Misri.

Katika fainali hizo zitakazoanza Juni 21 hadi Julai 19, 2019, Taifa Stars imepangwa kundi moja na Algeria, Senegal na Kenya.

Msafara wa wachezaji 32 wa Taifa Stars uliondoka nchini Juni 7, 2019 kwenda Cairo kuweka kambi ya maandalizi ya mwisho ya fainali hizo na tayari timu hiyo imeshacheza mechi mbili za kirafiki na Misri na Zimbabwe.
 
Wanasafiri kwa ndege.

Kuna maombi nilitaka kuomba kwa Mungu lkn kwa sababu Piere atakua miongoni mwao basi naondoa shilingi mpaka wakati mwingine
Ata mie kaka daaah imebidi nighairi
 
Je, mwenyekiti kamati ya uhamasishaji ndugu malyamungu DAB a.k.a naibu rais ameridhia hilo LA kumpeleka MTU wa hovyohovyo misri.
 
Hivi mnajua hata Piere hajui ni nini kimemfanya aonekane kama celebrity! ndio maana kila anakoitwa anabaki kunyoosha mikono juu akisema atabaki kuwa juu juu mawinguni.
 
Back
Top Bottom