KWELI Pierre Liquid ni mgonjwa, asema yupo nyumbani anajiuguza (Agosti 11, 2022)

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Mchekeshaji maarufu aliyejipatia umaarufu wake kupitia mitandao ya kijamii, Pierre Liquid amelazwa Hospitali ya Muhimbili Mwaisela wodi namba 6 iko ghorofa ya pili.

Aidha inaelezwa kuwa haijafahamika mpaka sasa Piere anasumbuliwa na ugonjwa gani.

 
Tunachokijua
Konki Liquid. Pierre. Mama nakufa. Chii. Ni utambulisho wa mwanaume huyu aliyejizolea umaarufu siku za hivi karibuni.

Huyu ni Peter Mollel, umaarufu wake uliibuka baada ya video iliyomuonyesha akisema “mama nakufa” kuzagaa mitandaoni mwishoni mwa mwaka 2018.

Amepitia mambo mengi ikiwemo kupata ajali ya kuvunjika mguu, na sasa inasemekana yuko hoi taabani akiugua.

Ukweli upoje?
Taarifa rasmi kutoka kwa Pierre Liquid ambaye yeye mwenyewe ameamua kuzungumza Agosti 30, 2022, amesema:

"Ni kweli ninaumwa, afya yangu haipo sawa na kwa sasa nipo nyumbani. Taarifa zaidi siwezi kueleza lakini afya yangu siyo nzuri."

Piere Liquid ni mfanyabiashara wa samani, hana watoto na hajaoa.
Pole kwake ila mbona thread haina comment hii 😁😁🤐🤐
 
Kwa ule umaarufu wa unywaji wa pombe kupitiliza unategemea atupe habari nzuri?!

Mara ya kwanza kupata umaarufu ni kuruka stejini na kuvunja mfupa wa mguu. Sasa kwasababu kaamua kuwa balozi wa ulevi na pombe wacha sasa figo, maini na moyo vitoe majibu.

Pombe inayonywewa kupitiliza sio nzuri kiafya. Kuwa mlevi wa kunywa sijui mzinga mzima au kreti nzima ya pombe haitakufanya kuwa imara bali una uhujumu mwili wako na unauangamiza taratibu baadae utakuja kusumbua sana magonjwa haya yasiyo ya kuambukiza.
 

Ebu nipe faida moja ya kufa ukiwa na ini ama figo nzima.
 
ndugu….wewe mtakie Heri tuu katika changamoto zake za afya. Hayo ya figo hata wasiokunywa Pombe na wanashinda gym….zinaharibika tuu. wangapi wameishi miaka 90 na wanavuta sigara tangu utotoni? Wangapi wametangulia mbele ya haki hata Nyama hawagusi……red meat tunaambiwa. Reality is….kila mtu ana namna yake ya kupigania afya. Mwisho wa siku….uhai anatoa Allah.
 
Huu mkao nakumbuka alikuwa anasilibwa na makonda
 
Ushaona wapi mtu anayekunywa namna ile ili atoke akabaki salama? Labda atoke kabisa dunia kwa kuharibu miundombinu ya mwili wake. Kuna mambo hayana longolongo, kama afya.
 
Hii thread ya Mwaka Jana ,vipi Konki Piere Liquid Fire anaendelea?
 
Yupo kwenye godown za silent ocean kule sokota , anashinda Tu kule , ukienda hata sa hv utamkuta

Habari Njema kama afya yake ilitengemaa ,Jamaa nachomkubali ni wa kujichanganya naona ameacha kazi yake ya ukapenta.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…