Mchekeshaji maarufu aliyejipatia umaarufu wake kupitia mitandao ya kijamii, Pierre Liquid amelazwa Hospitali ya Muhimbili Mwaisela wodi namba 6 iko ghorofa ya pili.
Aidha inaelezwa kuwa haijafahamika mpaka sasa Piere anasumbuliwa na ugonjwa gani.
Aidha inaelezwa kuwa haijafahamika mpaka sasa Piere anasumbuliwa na ugonjwa gani.
- Tunachokijua
- Konki Liquid. Pierre. Mama nakufa. Chii. Ni utambulisho wa mwanaume huyu aliyejizolea umaarufu siku za hivi karibuni.
Huyu ni Peter Mollel, umaarufu wake uliibuka baada ya video iliyomuonyesha akisema “mama nakufa” kuzagaa mitandaoni mwishoni mwa mwaka 2018.
Amepitia mambo mengi ikiwemo kupata ajali ya kuvunjika mguu, na sasa inasemekana yuko hoi taabani akiugua.
Ukweli upoje?
Taarifa rasmi kutoka kwa Pierre Liquid ambaye yeye mwenyewe ameamua kuzungumza Agosti 30, 2022, amesema:
"Ni kweli ninaumwa, afya yangu haipo sawa na kwa sasa nipo nyumbani. Taarifa zaidi siwezi kueleza lakini afya yangu siyo nzuri."
Piere Liquid ni mfanyabiashara wa samani, hana watoto na hajaoa.