Ukenya sio lugha tu, mimi hapa ninaweza kukushushia Kinyambo na pia Kipare zote lugha za Tanzania....Leo hii ninaweza kuishi ndani ya Tanzania bila yeyote kushtukia uraia wangu maana najua mengi kuhusu Tanzania hata zaidi ya wengi wenu, nimetembelea na kukatiza maeneo mengi ndani ya nchi yenu hiyo, mikoa na wilaya na vitongoji vingi, lakini kwa yote hayo, mimi ni Mkenya tena mzalendo wa nchi yangu kwa kwenda mbele, huniambii kitu na kamwe sitaihama nchi yangu, tutabanana humu humu hadi kieleweke.
Hivyo, Ukenya sio lugha tu, Ukenya sio kuijua Kenya, Ukenya ni zaidi ya hayo, Ukenya ni kuipenda nchi yako na bendera yake, wimbo wa taifa na kuwa tayari kuitetea kwa hali na mali. Wakenya, hata mkiona tunazozana, kila mmoja anaipenda Kenya mpaka ndani ya mifupa. Huyo Raila Odinga pamoja na kwamba ni mpinzani, au hata Kalonzo na wafuasi wao wanaipenda nchi yao mwanzo mwisho na hutokuta wanaponda kwenye mambo yasiyohusiana na siasa.
Sasa huyu mnayemsifia kuwa Mkenya kisa amejiita Mkikuyu timamu na kuongea maneno ya Kikikuyu na kuandika andika mambo ya Kikenya sio sifa tosha za Ukenya. Maana kasoro yake kubwa, anaponda hata mambo ambayo yanakumbatiwa na Wakenya wote, mambo ambayo yanatupa fahari ya kuwa Wakenya. Haiwezekani uponde ushindi wa wanariadha wetu au mafanikio ya vijana wetu kwenye nyanja za teknolojia halafu ujiite Mkenya.
Humu kuna Watanzania ambao hufungua akaunti zenye majina ya Kikenya, kunao ambao huchukia kila kitu cha Kenya, hawa Watanzania huwa nashuku labda jamaa atakua aliambiwa kwamba mamake kabakwa na Mkenya ndio akazaliwa, maana utakuta mtu ana hasira na Kenya na Ukenya kwa kila hatua au kila kitu, hadi mada zisizohusu Kenya lazima atazitafutia jinsi ya kuihusisha Kenya.
Subiri nitakuletea hapa picha ya Raila Odinga akimkumbatia mwanariadha Mkenya baada ya ushindi, itakupa uelewa kwa kina nini maana ya Ukenya.....