Mimi Mkenya, Tena Mzalendo, Lakini hii kenya ambayo Uhuru na ruto walioitunga wao na kuiita kenya hapo mimi sipo. Kenya hii bandia ya ufisadi, wizi, ubepari na ukabila mimi siwezi kuwa mzalendo.
Angalia Mfano wa JPM, alijua kwamba watanzania wengi walikuwa wamepoteza uzalendo sababu tanzania ilikuwa imebadilika kuwa nchi ya rushwa na wapiga dili. Wengi watanzania kwa kipindi kilicho pita walipata fedheha kuhusishwa na Tz.
Pili, wanariadha wa kenya nawashabikia pia ubunifu wa wakenya ni wa juu sana. Lakini, haya sio mambo ambayo inafanya nchi iwe "Nation".
Hii kenya ya Uhuru na Ruto siijui wala siitambui, hii ni yao wao na kabila zao