Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Brazil, Neymar Jr., hatarajiwi kurejea uwanjani hadi michuano ya Kombe la Dunia itakapofikia hatua ya mtoano. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 bado hajaanza mazoezi na kikosi chake kuelekea mchezo wa pili wa hatua ya makundi dhidi ya Haiti, huku akilazimika kurudia vipimo vya afya ili kuangalia maendeleo ya jeraha lake.
Neymar alijumuishwa kwenye kikosi cha Kombe la Dunia licha ya kupata jeraha la misuli ya mguu (daraja la pili) tangu Mei 17 alipokuwa akiichezea klabu ya Santos. Jopo la madaktari wa timu hiyo lina matumaini ya kumrudisha akiwa fiti asilimia mia moja kwa ajili ya hatua ya mtoano, ikimaanisha kuwa atakosa mechi zote mbili zilizosalia za Kundi C dhidi ya Haiti na Scotland.
Soma, Pia: Neymar arejea Kikosi cha Brazil kwa Kombe la Dunia 2026!
Brazil ilianza kampeni zake kwa sare ya 1-1 dhidi ya Morocco siku ya Jumamosi, ambapo Neymar alishuhudia mchezo huo akiwa benchi bila kuvaa jezi. Kikosi hicho kinatarajiwa kushuka uwanjani kukabiliana na Haiti siku ya Ijumaa,Juni 19, 2026 kabla ya kuhitimisha mechi za makundi dhidi ya Scotland siku ya Jumatano, Juni 24.
Kocha wa Brazil, Carlo Ancelotti, amesisitiza kuwa Neymar anapambana kwa bidii ili kupona na kuungana na timu wiki ijayo. Aliongeza kuwa walimjumuisha kikosini sio tu kwa sababu ya uwezo wake mkubwa wa kiufundi ambao hauna mashaka, bali pia kwa ajili ya uzoefu wake na mfano mzuri kwa wachezaji wachanga kikosini.