Pika popcorn simple kwenye jiko la gesi nyumbani

Pika popcorn simple kwenye jiko la gesi nyumbani

kwanini mpaka niwape watoto kwani me sitaki popcorn
 
  • Kicheko
Reactions: EEX
Hakuna haja ya kununua bisi. Ni gharama ndogo sana kuzipika nyumbani kwa kutumia jiko la gesi.

Nunua mahindi ya popcorn. Kilo inauzwa 4,000 na ndonya 1,500.

Tenga sufuria kubwa kubwa jikoni. Weka mafuta. Pasha mafuta hadi yaive. Yakiiva punguza moto uwe mdogo kabisa na weka popcorn zako ndani yake.

Hakikisha zinaenea vizuri kwenye sufuria na hazipandiani. Tia chumvi na anza kukoroga polepole kwa moto mdogo(Kufanya haya ni kuhakikisha zote zinapata moto sawa ili ukifungulia moto mkali ziive kwa pamoja).

Ukiona zimepata moto vya kutosha funika sufuria na weka moto mkali mpaka mwisho. Utaanza kusikia pu, pu, pu, pu, pu. Pu pu zikikata zima jiko lako na acha popcorn zipoe kidogo. Zoezi zima halichukua zaidi ya dk 10.

Ukifunua mfuniko utashangaa popcorn zimejaa na ni chache sana hazijapasuka. Wagawie watoto wajitafune.
Asante sana kwa somo zuri sana mkuu. Ungetupa na video kidogo inayo onyesha hizo hatua zote:

AGIZA GESI YA KUPIKIA HAPOHAPO ULIPO USIONDOKE KAA HAPOHAPO MTAANI KWAKO
Gesi zote zipo: Oryx Gas, Taifa Gas, Manjis Gas, O-Gas, Total Gas, Mihan Gas, na Puma Gas: zote zinapatikana hapo
 
Back
Top Bottom