Pika supu ya kongoro namna hii

Pika supu ya kongoro namna hii

Jospina

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2013
Posts
2,421
Reaction score
1,395
Mahitaji

1.Makongoro (miguu ya ng'ombe) kiasi

2.Limao 1 kubwa
3.Kitunguu swaum
4.Tangawizi
5.Chumvi
6.Pilipili


Matayarisho


Safisha makongoro kisha yatie kwenye pressure cooker. Kisha tia kitunguu swaum, tangawizi, chumvi,limao na maji kiasi. Baada ya hapo yachemshe mpake yaive na yawe malaini na pia ubakize supu kiasi inaweza kuchukua kama dk 45 au saa 1 hivi. Baada ya hapo yaipue na upakue supu yako kwenye bakuli katia pilipili kiasi kisha itakuwa tayari kwa kuliwa.


Note:

Ukiwa unanunua makongoro hakikisha unachukuwa yale yasiyokuwa na manyoya na pia
hakikisha usiyachemshe kupitiliza kwani yakiwa malaini sana utashindwa kuyaenjoy

NB karibuni SENENE G RESTAURANT-OPENING SOON
 

Attachments

  • KONGORO.JPG
    KONGORO.JPG
    9.4 KB · Views: 724
hii supu ilishanishinda jaman... sijui ni wapishi au ladha yake
 
Katika makabila ambayo hayajui kupika mojawapo ni wahaya. Sasa ushauri wangu hilo jina la biashara alibadilishe kwa kuwa litawaharibia biashara
 
Back
Top Bottom