Tetesi: Pikipiki alizotoa waziri mkuu Arusha ulikuwa ni mradi wa mtu kuwakopesha vijana

Tetesi: Pikipiki alizotoa waziri mkuu Arusha ulikuwa ni mradi wa mtu kuwakopesha vijana

Riba ya 46% ni zaidi ya mabenki yanayotoza kati 15% na 23%, huu ni utapeli na wizi kwa wanyonge.
..Na hapa bado ADHA ya Trafiki.....Kukibia kupata 8000 kwa siku pamoja na fedha ya mafuta na ya Mtu binafsi. Pikipiki 200 Mjini zikitafuta Milioni 1.6 kwa siku. Kasi ya utafutaji ITAWAUA wamiliki ....
 
Dodoma wamechagua CCM kwa 100% lakini hawajapelekewa Piki piki........... Arusha wameikataa CCM kwa 99% wamepewa Piki Piki 200


Kuna usemi unaosema mtoto anayelia mara kwa mara ndiye anayefaidi ziwa la *****
 
Hakuna aliyeumia ila nawaonea huruma sana wakopaji kwa uzoefu wangu wa mikopo only 25% ya wakopaji huweza kurudisha wengine huishia kufilisiwa na mifano ipo mingi.
Ulitakaje wapewe bure?
Kwenye kata funua gaweni bure basi
 
.., akili zenu, mnazijua ninyi wenyewe..., yaani mnahonga pikipiki ili mfanikiwe kuishawishi mioyo ya watu wa Arusha kumsahau mbunge wao ambaye mnamnyima dhamana kila siku!? Mnasahau haraka sana ninyi watu..,

.., katika uchaguzi mkuu wa 2015 (kipindi cha kampeni), aliyekuwa mgombea wa CCM katika jimbo la Moshi Mjini (Davis Mosha) alihonga pikipiki kwa 'staili' kama hii..., kwenye sanduku la kura wananchi wakamchagua Japhary Michael (CHADEMA).., ambaye ni mrithi wa Phillemon Ndesamburo.

.., Davis Mosha akaomba pikipiki zake..., jamaa wakamwambia '.., na wewe turudishie vitambulisho vyetu vya kupigia kura, tungekuchagua vipi wakati vitambulisho ulikomba vyote?'..,

akaona imekuwa' too much '.., akaamua kwenda kwenye chama chake cha CCM na kuwaeleza kwamba wamekula wali wake na posho wamelamba na wamemsaliti..., Jamaa wakamwambia..., 'huku hawa jamaa hawaelewi, wewe Rudi DSM na huyo Lemutuz wako.., hapa umekula wa chuya'..,

KWANINI MANENO HAYA; Tunajaribu kukumbushana tu kwa wale ambao wanadhani jimbo la Arusha linaweza kuondoka kwa pikipiki 200 mikononi 'mwa' CHADEMA.., kwamba Jimbo litaondoka Lema akifungwa..., kitu nawaeleza.., kuna Godbless Lema zaidi ya zile pikipiki ambazo mligawa pale Chuga.., Lema wako Arusha nzima..

..., ninyi CCM, kwa Arusha mmecheza peku.., kwenye vyupa vingi.., mchezo wenu haramu.., hizi pikipiki ndiyo tutafunga bendera zetu siku mnampa dhamana Godbless Lema, tutaimba 'people's Power'.., na hizi TOYO zitarindima..., nawaeleza hivi..., WATU WA KAGERA BADO WANAPIGWA NA JUA NA MVUA KWA KUKOSA MISAADA YA MAAFA KULE.., hizi milioni 400 zilitosha kufanya kitu kwao..,

SIASA ZA MAJITAKA.., SIASA ZA BEI RAHISI.., SIASA ZA KUNUNUA FIKRA ZA MASKINI..., SIASA ZA SIHASA!
 
KUMBE WAZIRI MKUU AMEINGIZWA KWENYE MRADI WA KITAPELI ARUSHA.

Siri imefichuka kuhusiana na pikipiki 200 zilizogawia kwa vijana wa Arusha, mwishoni mwa wiki iliyopita WAZIRI MKUU Majaliwa K Majaliwa alizindua pikipiki 200 waliokopeshwa vijana wa Arusha,

Jana nilikutana na mmoja wa wafanyabiashara wakubwa wa pikipiki mjini Arusha ambaye kwa maelezo yake aliniambia anafahamu kuhusu huo Mradi na kwa mara kadhaa walikutana na mkuu wa mkoa wa Arusha ndg Mrisho Gambo kukubaliana ili pikipiki zake ziingizwe kwenye Mradi huo, kwa maelezo yake kuna mambo walishindwa kukubaliana na RC Gambo nadhani ndo ikawa sababu ya yeye kutoshwa,

Sasa kwa msiyojua huo mradi haukuwa msaada kama ulivyokuwa ikitangazwa bali ni biashara tena ya kinyonyaji embu fuatilia masharti ya mkopo wa pikipiki hizi,

Kila aliyekopeshwa pikipiki alitakiwa adhaminiwe na mtu mwenye hati ya nyumba au mali isiyohamishika, hapa mkopeshaji anapata hakika ya kupata marejesho ya mkopo wake.

Kila mkopaji wa pikipiki alitakiwa arejeshe kiasi cha Tsh 8000 kwa siku ndani ya mwaka mzima yaani kwa siku 365

Sasa wewe chukua 8000×365=2920,000

Kwa maana hiyo kila mtu atakuwa ameuziwa pikipiki tsh 2,920,000/=

Bei ya Pikipiki ya aina zilizokopeshwa dukani ni tsh 2000,000/=

Kwa maana hiyo tsh 920,000/= anayopata mkopeshaji ni riba ya mkopo wake huo,

Hii inamaana kwamba amepata fursa ya kuuza pikipiki 200 kwa mwaka kiasi ambacho siyo rahisi kwa kipindi kama hichi kukifikia mauzo ya kiwango hicho, lakini pia anapata riba ya mtaji wake ya kiasi cha tsh 920,000/= kwa pikipiki moja,

Hii inamaana kuwa Ukiacha faida ya kawaida tu ya kuuza pikipiki moja tsh 2000,0000/= mkopeshaji anapata cha ziada yaani riba ya tsh 920,000×200=184,000,000.

Mwisho wa siku huyo anayesema amewasaidia vijana kujikwamua kiuchumi atakuwa ametengeneza tsh milioni 184 kwa mwaka.

Ukiacha bishara ya madini ya Tanzanite hapa Arusha sijui kama kuna biashara nyingine inalipa kama hii, sasa sijui Waziri mkuu ameingizwa kwenye dili hili kwa kujua au kwa kutojua sijui, ila mimi tu niwatakie wakopaji kila la Kheri katika kurejesha fedha kwa waliowasaidia kwa wakati wasije kufilisiwa waliyowadhamini.
tuliambiwa ni Tshs. 7000 kwa siku sasa hiyo 8000 umeitoa wapi??
 
Riba ya 46% ni zaidi ya mabenki yanayotoza kati 15% na 23%, huu ni utapeli na wizi kwa wanyonge.
Wengi hawakuliona hili....na mbaya zaidi kwenye matangazo na hotuba tumeambiwa ni pikikipi za msaada [emoji144] [emoji144] [emoji144]
Lakini vile vile serikali ingekuwa inafuatilia taarifa mbalimbali za vyombo vya motor huu maxi usingekubalika...!. kwasasa pikikipi ndio zinaongoza kwa ajali vifo na kuzalisha walemavu
Kama Taifa tunategemea vifaa tiba toka nje, imagine ni pesa kiasi gani zinatumika hapo
Vijana Wengi wanakuwa ni tegemezi kutokana na ulemavu! Hii ni hasara kwa Taifa. ..kuna ishu ya wajane na yatima hapo
Vyovyote iwavyo huo mradi ulilenga zaidi faida binafsi na kujitangaza kisiasa Lakini kiuhalisia ni mradi mbaya wenye kuhujumu uchumi
 
Bakeza hizo pikipiki ni aina gan? Kama ni boxer hiyo fedha ni sahihi, lakini pia ungefanya utafiti wa kutosha pengine huyo bwana uliyekutana naye amekueleza kwa mihemko ya kukosa hilo diri. Ni vyema pia ungeambatanisha maoni ya wananchi waliokopesha pikipiki husika, tujue wao wanasemaje kuliko kutuletea story za jamaa aliyetoswa diri.
Lakini pia naamini hao wakopeshwaji wanaakili timamu na hayo masharti uliyoyataja watakuwa wanayajua vizuri kuliko wewe uliyoyasikia
 
..Na hapa bado ADHA ya Trafiki.....Kukibia kupata 8000 kwa siku pamoja na fedha ya mafuta na ya Mtu binafsi. Pikipiki 200 Mjini zikitafuta Milioni 1.6 kwa siku. Kasi ya utafutaji ITAWAUA wamiliki ....
Kwani walishikiwa bunduki lazima wazichukue?
 
Tujiandae kusikia vilio vya wakopaji, walioweka bond nyumba na mkopeshaji.

Wasifikiri kupata elfu 8 kila siku ni jambo rahisi, kuna masika, pikipiki mbovu wiki, ajali, kuibiwa/kuporwa, kuugua/kulazwa na matatizo mengine ya kijamii.
Umeongea point. Hizo piki piki zifikisha miezi mi8 vilio vitaanza.
 
Mount Meru Hospital kuna ward inaitwa TOYO, waiboreshe tu.
 
Kama RC Gambo kawa mbunifu kawapa wana Arusha piki piki bila kuweka down payment asifiwe sio kudhihakiwa!
Lema nilimsifu ktk mradi wake wa hospital na huyu Gambo asifiwe kwa hili
 
Utapeli uko wapi? Unadhani kama kila mmoja angeamua kujichanga ili aje kununua pikipiki yake angefanikiwa? mtaji angeutoa wapi? Kama muuzaji/mkopeshaji angeuza kwa cash unadhani angezungusha mara ngapi? kwa nini na yeye asipate faida?
Utapeli ni pale jamii imedanganywa kuwa ni mgao wa pikipiki kwa vijana kumbe ni mradi wa matajiri
Na wakishindwa kulipa dhamana zinachukuliwa kiulaini kama sikutiana umasikini ni nini ?
 
Bakeza hizo pikipiki ni aina gan? Kama ni boxer hiyo fedha ni sahihi, lakini pia ungefanya utafiti wa kutosha pengine huyo bwana uliyekutana naye amekueleza kwa mihemko ya kukosa hilo diri. Ni vyema pia ungeambatanisha maoni ya wananchi waliokopesha pikipiki husika, tujue wao wanasemaje kuliko kutuletea story za jamaa aliyetoswa diri.
Lakini pia naamini hao wakopeshwaji wanaakili timamu na hayo masharti uliyoyataja watakuwa wanayajua vizuri kuliko wewe uliyoyasikia
Unafikiri wanaokwenda kukopa benki hawana akili timamu, ni kutokana na unyonge wako tunalazimika kukopa hata kama unapewa masharti magumu, kilio huja baadae.

Walizopewa ni SanLg sokoni zinauzwa mil.2.
 
Tena amewafanyia fair sana maana pikipiki yamkataba wanapelekaga 10000 kwa siku piga Mara miezi kumi unapata bei gan?elfu nane tu daaah wamebahatika sana,,,pia ni fursa hyo kuna ubaya gan hapo?
 
Kwa nini waliweka taswira kama vile hizo Pikipiki wanazigawa bure na Magige ndiye kazitoa?
 
Back
Top Bottom