Jamani wana jf nasikia boxa zinakufa sana piston...rings...block
Tena wazoefu wanasema hazirekebishiki zinatoa sana moshi, wengi wao zimewafia na wamezipak ndan.
Pia service yake ni garama sana. Je, wanaJF nini madhaifu ya pikipiki boxer?
Naomba ubadilishe heading yako iwe swali ili uelimishwe
1. Nianze tu kukuelimisha kuwa Boxer sio Pikipik ya Kichina, Ile ni Pikikipi kutoka India - Kampuni ya Bajaj
2. Bajaj ipo kwenye kundi la pikipiki zilizotengenezwa kwa tecnologia ya juu zaidi ukilinganisha na hizi za kichina
Ninamaanisha inahitaji vitu OG, Ifanyiwe sevise kwa wakati kwa kutumia Oil sahihi ( sio zile za kupima mtaani ), Iwekwe mafuta safi (sio ya kununua kwenye vichupa nk)
Ukifanya hivyo na ukijua kuiendesha kwa usahihi na maanisha uendeshe kwa gia stahiki kulinganga na speed na mzigo; Sio unaweka gia namba mbili halafu unavuta mafuta hadi mwisho ndio unaua hizo piston. Unaweza kupitwa na pikipiki inangurunga Engine inataka kupasuka, maana yake ameweka gia 1 au mbili na mafuta mengi sana; ni makosa!
Ukweli ni kuwa unaweza kukaa na Boxer bila matengenezo kwa miaka hadi ukasahau kuwa inaharibika
Kuhusu gharama za service, inategemea tu kwani sana sana ni kubadilisha oil filter & Oil yenyewe ambayo hata za kichina zinabadlishwa (Badilisha Oil kila kilometa 1000 hivi) angalia kilometa sio siku kwa kuwa kuna siku unaweza kuwa umepaki au ukatembea kidogo sana, hivyo kuhesabu siku haileti maana kiufundi
Kuhusu kutoa Moshi: Tatizo wengi hununua used (zilizotumika) na aliyetumia mwenyewe
alikuwa Sio dereva mzuri, au hafanyi Service kwa wakati au anafanya kwa oil isiyo stahil nk ndio sababu zinatoa moshi
Kwa kuzingatia mahitaji ya Boxer, nafikiri zinafaa zaidi mazingira ya mjini...