Pikipiki kubadili muungurumo

Joined
Aug 24, 2015
Posts
53
Reaction score
36
Habari wanajamvi nina pikipiki yangu Boxer 150, naitumia matumizi binafsi imebadili muungurumo na kupoteza nguvu. Shida Itakua kitu gani?

Kwa anaejua tafadhali kwenye injini
 
Je, inatoa sana moshi wa blue? Kama ndiyo basi badilisha piston ring na gasket zote maana hapo kuna compression inapotea sehemu. Baada ya hapo piga test ride kuona hiyo ishu ya mlio
 
Nenda kwa fundi afungue block, kisha akague piston rings, valve zote inlet na outle, block kama limechimba pembeni na piston kama Ina tatizo.

Baada ya kukagua block, piston, valve, valve seal, cylinder head gasket, gasket ya chini kwenye block na Uzi wa moto ndio akuambie ubadili vitu gani.

Hiyo tabia ya kubadili piston rings tu muda si mrefu tatizo litarudi tena. Hao mafundi wanaokuambia badili rings tu kila siku utaenda garage.
 
Check mkazo wa tapeti pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…