Pikipiki ya 110cc naweza kusafiri nayo umbali mrefu?

umetisha hii inapasua sana ... yangu mimi speed 60 inatosha kabisa
 
Copy ya wosia pia uiache kwa wazazi wako
 
Nimeipenda hii mashine.naomba detail zake na wapi inapatikana na bei.
 
Nikiwa na boxer speed ya 50 tuu naona kama inapaa, ndio useme 70 israel yulee
Hiyo labda ma san lg
Aaah mkuu mimi 70-80 natembea vizuri tu na Boxer 150. Tena hapa hapa mjini kukiwa na uwazi wa kutosha. Mfano darajani Kigamboni pale huwa naserereka kinoma.
 
Mkuu hapo unapiga route bila shida kabisa! tena cc za injini sio kigezo maana kuna jamaa amezunguka nchi nyingi sana akiwa na pikipiki yake siikumbuki aina ila ilikuwa na 60cc

mimi mwenyewe ni mtu wa route ndefu na pikipiki katika vitu ambavyo huwa nazingatia

1. Tairi ziwe vizuri kuepuka pancha wakati wa safari

2. mfumo wa mafuta na uchomaji mafuta uwe vyema kabisa

3. Hakikisha chain na Sprocket ziwe katika hali nzuri lakini pia usisahau ku adjust chain pamoja na kuifanyia Lubrication (Hii ni muhimu sana)

4. beba mzigo kidogo ili pikipiki iwe nzito kidogo, hii inakupa balance hata kwenye spidi kubwa na hata kwenye upepo mkali

5. vaa protective gears

6. weka vituo vya kupumzika angalau nusu saa lakini pia kunywa maji ya kutosha inasaidia kupunguza uchovu
 
Mkuu umetisha Sana.. asante sana
 
Mkuu ukitumia Lita ngapi ..? Je gharama zilizidi kusafiria na gari...? Najipanga kwenda simiyu/shinyanga kesho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…