Pikipiki zenye Kelele na Taa kali zakamatwa Arusha

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
977
Reaction score
1,966

​
Kamati ya Usalama ya Wilaya ya Arusha imeanzisha operesheni maalum ya kukamata pikipiki zinazokiuka sheria za usalama barabarani, hususan zile zinazotoa kelele za milipuko na zilizofungwa taa zenye mwanga mkali. Hatua hiyo inalenga kuboresha usalama wa usafiri na kupunguza kero kwa watumiaji wengine wa barabara pamoja na wananchi kwa ujumla.

Akizungumza katika Kituo Kikuu cha Polisi Arusha, Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, Dkt. Jacob Julius Rombo, aliwataka waendesha bodaboda wanaoharibu mifumo ya pikipiki zao kuacha mara moja, akisisitiza kuwa kazi ya bodaboda ni muhimu lakini inapaswa kufanywa kwa kuzingatia sheria, kanuni na maadili ya kazi bila kusababisha usumbufu kwa jamii.

Kwa upande wake, Mkuu wa Polisi Wilaya ya Arusha SSP Georgina Matagi amesema kuwa katika operesheni iliyofanyika kwa miezi mitatu, jumla ya pikipiki 248 zenye taa kali na pikipiki 13 zinazotoa kelele kali zilikamatwa. Pia wamebaini baadhi ya pikipiki zinaficha namba za usajili kwa kuandika majina ya watu, jambo linalohusishwa na vitendo vya uhalifu.​
 
Bodaboda wengi ni kama vile wako juu ya sheria. Wanapewa pikipiki ikiwa mpya na nzima kabisa! Hawa viumbe wanakera mpaka basi.

Wanatoa side mirrors, wanatoa taa ya mbele na kuweka taa zenye mwanga mkali, wanaliharibu bomba la kutolea moshi ili lipige kelele zisizo za kawaida, nk. Na polisi wa usalama barabarani wenye wapo busy na waendesha magari tu!!
 
🤣🤣Yaani ukishaona hivyo kimbia hatari hio, kaa mbali, anaweza kukulaza miezi mingi pale MOI huyo
huku uswahilini kwangu wamejaa muda wowote wanapita kama mshare asee🏹🤣,,

, kuna siku nilikua naenda mahali ila sipafaham vizuri, ikabidi nichukue boda,, mwanzoni kaanzisha singeli nikamwambia nina matatizo ya masikio naomba uzime,, kweli akanielewa,,
kimbembe kikaja kwenye chocho nilizo pitishwa et anaita shortcut weeee nilikoma plus huo mwendo🤣🤣🤣 ikabidi nimwambie kama anataka kufa anishushe ili aendeleee na safari zake,, ndo akapunguza spid

nilipofika mwisho wa safari ilibidi nisali kwanza🤣🤣🤣🤣
 
🤣🤣 Hawa jamaa ni hamnazo, yaani ukifikishwa salama unashukuru Mungu, halafu sio usafiri wa kuzoea utazikwa mapema sana maana yeye kulichomekea Semitrela haoni shida
 
ni kweli ila hamna namna,, wengine tunapokaa bajaji hazifiki ni lazima upande boda ili akusogeze barabarani otherwise utembee kwa miguu mpka barabara kubwa,,, na mimi asubuhi siwezi kutembea maana nitafika kibaruani nimechafuka au nimepata jasho au nimechoka
 
Kamati ya Usalama ya Wilaya ya Arusha imeanzisha operesheni maalum ya kukamata pikipiki zinazokiuka sheria za usalama barabarani, hususan zile zinazotoa kelele za milipuko na zilizofungwa taa zenye mwanga mkali. Hatua hiyo inalenga kuboresha usalama wa usafiri na kupunguza kero kwa watumiaji wengine wa barabara pamoja na wananchi kwa ujumla.

Akizungumza katika Kituo Kikuu cha Polisi Arusha, Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, Dkt. Jacob Julius Rombo, aliwataka waendesha bodaboda wanaoharibu mifumo ya pikipiki zao kuacha mara moja, akisisitiza kuwa kazi ya bodaboda ni muhimu lakini inapaswa kufanywa kwa kuzingatia sheria, kanuni na maadili ya kazi bila kusababisha usumbufu kwa jamii.

Kwa upande wake, Mkuu wa Polisi Wilaya ya Arusha SSP Georgina Matagi amesema kuwa katika operesheni iliyofanyika kwa miezi mitatu, jumla ya pikipiki 248 zenye taa kali na pikipiki 13 zinazotoa kelele kali zilikamatwa. Pia wamebaini baadhi ya pikipiki zinaficha namba za usajili kwa kuandika majina ya watu, jambo linalohusishwa na vitendo vya uhalifu.​
Safi
 
Wafanye ukamataji huu nch nzima.

Kuna watanzania wenye asili ya asia kwenye baadhi ya miji, huwa ni ni namna ya kujifurahisha pale wanapoendesha pikipiki lenye kelele na mwendo mkali katikati ya mji.

Kuna wamatumbi wengine huwa wanafanya hivyo baada ya kupuliza cha Arusha na wengine ni baada kupiga smart gin

Hawa wote wadhibitiwe.
 
Unakuta boda ana Kiduku, ana kitshirt amevaa kandambili akitimua mbio ile kandambili moja ni kama inataka kuchomoka, amefungulia singeli sauti kubwaaa..🙄🙄
Serikali iwaangalie kwa jicho kali hawa madogo.
 
Back
Top Bottom