Huko juu kote umedanganywa isipokuwa mchangiaji mmoja tu.Pilaf rice ni wali aina nyingine na ni tofauti na pilau.Pilaf ni wali una kitunguu cha kawaida,safron ,cayene pepper na stock.Kwa ufupi ni wali unaopikwa na seasoned stock.Stock ni mchemsho wa mifupa ya kuku,au mifupa ya nyama ya ng'ombe,Mifupa ya kondoo,(wanyama wote isipokuwa nguruwe)Samaki,vitunguu,vitunguu swaumu,carrot,leeks na cellery,inachemshwa taratibuu kwa mda mrefu alafu unachuja yale maji unatumia kupikia huo wali wako.Pilau kwa kiingereza unaweza kuiita spiced rice lakini kwa nini uhangaike,jina la kitu linatakiwa libaki hivyohivyo tu mkuu.Mwambie utampikia our special Tanzanian Xmass/festive rice called pilau.Lakini hata hivyo wazungu wengi wanaijua pilau.