Pilipili ya mwendo kasi

Pilipili ya mwendo kasi

Kasie

Platinum Member
Joined
Dec 29, 2013
Posts
22,379
Reaction score
41,294
Sifa zake:

Inanukia vizuri
Kumvutia mlaji kuwa na hamu ya kula chakula hata kama hakuna ladha.
Inaongeza namna ya kifikiri...
Ni tamu, kuwasha kwake ndo utamu wenyewe.
Inapatikana kwa wingi na bei yake si mbaya.

Angalizo:

Ni kali mithili ya pilipili mbuzi
Kama una hasira za haraka unaweza kupandisha ukichaa
Ukila na chakula cha moto sanaa tegemea au jiandae kukinga au kufuta kamasi mchuruziko.
Nyingine siri ya kambi, uhondo wake ichukue itafune pamoja na chakula chako halafu utupe mrejesho, yamekukuta?

Saasaa baanaa, Kilichomkuta bi Zinduna na pilipili ya mwendo kasi hana hamu.

Bi Zinduna ametoka kwenye mishughuliko yake anasikia njaa maana hakupata muda wa kula siku nzima. Baada ya kupambana na foleni ya siku nzima akafika nyumbani na kukuta dada ameshatayarisha chakula. Akafika moja kwa moja mezani na kupakakua chakula kisha akachukua pilipili ule ya mwendo kasi, akaikata vipande vinne kwa mkono na ukiweka kwenye sahani tayari kuilumanga.

Ghafla akasikia kwenda haja ndogo, kisha akajiambia amalize kula kwanza ndiyo aende ili afurahie mlo wake na asikatishwe na haja. Shika mwendokasi tonge nyama, tonge pilipili Ila taarifa ya haja ndogo kubana ikawa palepale. Akaamua kunyanyuka mezani na kuelekea msalani. Huko akanawa mikojo na maji kisha akamaliza haja yake akajiswafisha na maji maeneo pendwa ili arudi kula kwa uhuru zaidi na kufurahia chakula.

Weeh, ile amekaa mezani akasikia mmhh mbona kama kuna sisimizi wanamng'ata huko eneo pendwa, yooh muwasho ukaanza akashindwa kuhimili na kuanza kujikuna juu ya nguo. Kumbe anavozidi kujikuna muwasho nao unazidi kuchachamaa.

Chakula hakikulika tena maana pilipili ya mwendo kasi ilishafanya yake ikabaki vidoleni alivyoenda msalani kujiswafi akapaka muwasho hukooo. Ikabidi anyanyuke mezani, kachukua barafu na kuzibandika ili muwasho upungue ila ilikuwa kila baada ya dakika kadhaa anapiga yowee... ya motooo! ya motooo!

Angalizo jingine:

Ukila pilipili ya mwendo kasi na ukaipasua na kuishika na mikono yako, chondechonde usijiguse kwenye ngozi yako.

Pilipili ya Shamba, yakuwashia nini?

Cheers to hot pepper!!.

Matata the K.
 
Kasie,
inaleta utamu hahahahahahahahah hapo mzee angekuwa karibu basi angempa mambo jumlisha na muwasho wa mwendokasi haaaaah basi mambo yente yente mdundo bila buti
 
Pilipili mwendo kasi ni habari nyingine kabisa. Nilikua siijui maana muonekano wake ni kama pilipili mbuzi. Baada ya kuagiza msosi kama kawaida yangu pilipili lazima iwepo.

Siku hiyo nilipoitafuna hiyo pilipili ambayo niliona kama zile za siku zote,mara nikahisi kama kaa la moto kinywani, mishipa ya shingo ilisimama, nikahisi kichwa kinataka kupasuka, kijasho kikanitoka japo ilikua eneo la wazi na upepo wa kutosha! Kiufupi chakula nilikiacha, hamu yote na njaa vikakata palepale. Hapana chezea pilipili mwendo kasi aisee
 
Sesten Zakazaka,


Ahahahahahhaaa looh,

Pole kwa yaliyokusibu ila hii mwendo kasi si bure iko namna imefanywa, hata pilipili kichaa haioni ndani looh!!
 
Pilipili ukiishika mkononi hata ukinawa huwa haiishi kirahishi yaani.

Na kama una ngozi teke, inawasha hata kwenye viganja na vidole, sembuse ukijipaka bahati mbaya kunakoo...

Wale waliowahi kupata ajali ya pilipili kuingia jichoni wanaelewa walau aina ya muwasho ulioko maeneo pendwa....
 
Na kama una ngozi teke, inawasha hata kwenye viganja na vidole, sembuse ukijipaka bahati mbaya kunakoo...

Wale waliowahi kupata ajali ya pilipili kuingia jichoni wanaelewa walau aina ya muwasho ulioko maeneo pendwa....
Hata mimi huo wa maeneo pendwa unanitokea sana, bora hata iingie jichoni.
Kule unapata aibu ukiwa unajiona kabisa.
 
Back
Top Bottom