Pilipili ya mwendo kasi

Pilipili ya mwendo kasi

Sifa zake:

Inanukia vizuri
Kumvutia mlaji kuwa na hamu ya kula chakula hata kama hakuna ladha.
Inaongeza namna ya kifikiri...
Ni tamu, kuwasha kwake ndo utamu wenyewe.
Inapatikana kwa wingi na bei yake si mbaya.

Angalizo:

Ni kali mithili ya pilipili mbuzi
Kama una hasira za haraka unaweza kupandisha ukichaa
Ukila na chakula cha moto sanaa tegemea au jiandae kukinga au kufuta kamasi mchuruziko.
Nyingine siri ya kambi, uhondo wake ichukue itafune pamoja na chakula chako halafu utupe mrejesho, yamekukuta?

Saasaa baanaa, Kilichomkuta bi Zinduna na pilipili ya mwendo kasi hana hamu.

Bi Zinduna ametoka kwenye mishughuliko yake anasikia njaa maana hakupata muda wa kula siku nzima. Baada ya kupambana na foleni ya siku nzima akafika nyumbani na kukuta dada ameshatayarisha chakula. Akafika moja kwa moja mezani na kupakakua chakula kisha akachukua pilipili ule ya mwendo kasi, akaikata vipande vinne kwa mkono na ukiweka kwenye sahani tayari kuilumanga.

Ghafla akasikia kwenda haja ndogo, kisha akajiambia amalize kula kwanza ndiyo aende ili afurahie mlo wake na asikatishwe na haja. Shika mwendokasi tonge nyama, tonge pilipili Ila taarifa ya haja ndogo kubana ikawa palepale. Akaamua kunyanyuka mezani na kuelekea msalani. Huko akanawa mikojo na maji kisha akamaliza haja yake akajiswafisha na maji maeneo pendwa ili arudi kula kwa uhuru zaidi na kufurahia chakula.

Weeh, ile amekaa mezani akasikia mmhh mbona kama kuna sisimizi wanamng'ata huko eneo pendwa, yooh muwasho ukaanza akashindwa kuhimili na kuanza kujikuna juu ya nguo. Kumbe anavozidi kujikuna muwasho nao unazidi kuchachamaa.

Chakula hakikulika tena maana pilipili ya mwendo kasi ilishafanya yake ikabaki vidoleni alivyoenda msalani kujiswafi akapaka muwasho hukooo. Ikabidi anyanyuke mezani, kachukua barafu na kuzibandika ili muwasho upungue ila ilikuwa kila baada ya dakika kadhaa anapiga yowee... ya motooo! ya motooo!

Angalizo jingine:

Ukila pilipili ya mwendo kasi na ukaipasua na kuishika na mikono yako, chondechonde usijiguse kwenye ngozi yako.

Pilipili ya Shamba, yakuwashia nini?

Cheers to hot pepper!!.

Matata the K.
Wakongwe hatuwezi kuingizwa chaka kirahisi... ngoja kwanza nisome katikati ya mistari ili nijue hii pilipili inayozungimziwa hapa ni ile ya shambani au ya chumbani

Will be right back...
 
Mareale makaveli aahahahahahaa yaani weeweee.....

Muwasho wa mwendo kasi ndo mpango mzima, mbuzi mie alikuwa hanikolei utamu aahahahahahaaa kwaheriiiii....

Ila asante kwa elimu ya kukata muwasho.

Gracias.

Mbuzi gani hakukolei! Mbuzi kagoma au mbuzi wa kibao cha mbuzi!!!?
 
Wakongwe hatuwezi kuingizwa chaka kirahisi... ngoja kwanza nisome katikati ya mistari ili nijue hii pilipili inayozungimziwa hapa ni ile ya shambani au ya chumbani

Will be right back...

Ahahahaaaaa babuuu usifanye ajizi, nimekumisiii.....

Halafu leo nna hamu ya kula chipthi yai.... mida ya saa kumi hivi jioni...
 
Ahahahahahaaaaaaa looh sina hamu, kamasi zinanitoka tu hapa kwa kuwashwa.... Ila taamuuu...

Uzur wa huku hamu unapandishwa halafu zinatolewa baada ya kuangusha kamasi!! Ieleweke ni kamasi na sio kumasi kule kwetu ghana.

Utamu unakuwepo kati ya kupandishwa hamu na kutolewa zoote!!
 
Uzur wa huku hamu unapandishwa halafu zinatolewa baada ya kuangusha kamasi!! Ieleweke ni kamasi na sio kumasi kule kwetu ghana.

Utamu unakuwepo kati ya kupandishwa hamu na kutolewa zoote!!

Mareale twende tukale pre lunch.....

Ahahahahaaaaaaa.
 
Tangulia bibie..
naja kwa nyuma!!

Niko kwa nyuma nakusindikiza kwa macho! Nipate wasaa wa kumeza mate ya uchu wa msosi tarajiwa! Sintakuwa na haja ya kungoja ugeuke tena.

Seeengeeehhh weeeh aahhahahahaahahahahhahaaaaaaaaaaaa

Niko sirias ujue...
 
Ama kwa hakika wish nikuone uso kwa uso

Sent using Jamii Forums mobile app

Sema SUUU..... Halafu angalia avatar yangu mara 6 kisha ita Kasinde mara tatu na ubusu hewani mara moja ntatokea hapo hapo ulipo...

Ukiniona utachotakiwa kufanya ni kutabasamu tuu, usizungumze, usinisemeshe, usitingishike wala usiniguse hata nikikusemesha au kukuita au kukutekenya aahahahahahahaaaa
Cheers.
 
[emoji23]🤣🤣
 
Na kama una ngozi teke, inawasha hata kwenye viganja na vidole, sembuse ukijipaka bahati mbaya kunakoo...

Wale waliowahi kupata ajali ya pilipili kuingia jichoni wanaelewa walau aina ya muwasho ulioko maeneo pendwa....
Kipindi nime vunja ungo nilikuwa natamani kuwa na matiti makubwa, nikasikia wanafunzi wakisema ukiyapaka pilipili yanakua haraka haraka, nyumbani kulikuwa na mpilipili nikachuma nikakata vipande vidogo dogo nikavua nguo nikapaka
Matiti yangu ili yawe makubwa ......nilipomaliza nikasemaje embu nipake na huku chini nione kutakuwaje nilikuwa nujua pili pili inawasha mdomoni tu we we we we we nilivyopakaaa ni siri yangu ya kilicho nikutaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sema SUUU..... Halafu angalia avatar yangu mara 6 kisha ita Kasinde mara tatu na ubusu hewani mara moja ntatokea hapo hapo ulipo...

Ukiniona utachotakiwa kufanya ni kutabasamu tuu, usizungumze, usinisemeshe, usitingishike wala usiniguse hata nikikusemesha au kukuita au kukutekenya aahahahahahahaaaa
Cheers.
Duuuuuh hayo mashart mbona ya moto sana bibie kasie mwenye yake Matata ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kipindi nime vunja ungo nilikuwa natamani kuwa na matiti makubwa, nikasikia wanafunzi wakisema ukiyapaka pilipili yanakua haraka haraka, nyumbani kulikuwa na mpilipili nikachuma nikakata vipande vidogo dogo nikavua nguo nikapaka
Matiti yangu ili yawe makubwa ......nilipomaliza nikasemaje embu nipake na huku chini nione kutakuwaje nilikuwa nujua pili pili inawasha mdomoni tu we we we we we nilivyopakaaa ni siri yangu ya kilicho nikutaa

Sent using Jamii Forums mobile app

Aahahahahahhaaaa utoto raha sana...
 
Back
Top Bottom