ZeMarcopolo
Platinum Member
- May 11, 2008
- 14,040
- 7,303
Pinda: Wawekezaji kwenye kilimo watapewa ardhi
Na Joseph Mwendapole
3rd June 2009
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, amesema serikali itawapa ardhi wawekezaji wa kigeni wanaotaka kuwekeza kwenye kilimo nchini bila kujali kelele za wananchi.
Vile vile, amesema ingawa yeye ni Waziri Mkuu, lakini baba yake ambaye ni mkulima, bado ni fukara hali inayomfanya ajisikie kuwa ana deni la kuinua sekta ya kilimo nchini.
Aliyasema hayo juzi jioni wakati akizungumza kwenye chakula cha jioni kilichoandaliwa na Taasisi ya Sekta Binafasi (TPSF), kwa ajili ya kubadilishana mawazo na wafanyabiashara wa ndani.
Wafanyabiashara hao ni wale wanaohudhuria mkutano wa siku mbili ulioanza jana jijini Dar es Salaam unaoongozwa na Rais Jakaya Kikwete.
Pinda alisema Tanzania ina ardhi nzuri na yenye rutuba kwa ajili ya kilimo ambayo haitumiki kwa uzalishaji lakini wanapopewa wawekezaji kuitumia wananchi huanza kulalamika.
Alisema Tanzania inakadiriwa kuwa na hekari zaidi ya milioni 40 ambazo zinafaa kwa kilimo lakini mpaka sasa watu wamebaki kuitizama bila kuifanyia chochote.
Aliongeza kuwa hakuna nchi yoyote duniani iliyofanya miujiza katika mapinduzi ya kilimo na mifugo na kwamba kilichofanyika ni kuwa makini na kufanya tafiti za kina katika kuendeleza sekta hizo.
Aliongeza kuwa serikali sasa lazima ifanye jambo la kusogeza mbele sekta ya kilimo na kwamba isipoweza kufanya hivyo sasa ni dhahiri haitakuja kuweza tena.
Mkurugenzi wa TPSF, Dk. Evans Rweikiza na Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Ester Mkwizu, walisema sekta hiyo imekuwa ikikua siku hadi siku na waliomba ushirikiano wa serikali katika kukamilisha mipango yake.
Source:NIPASHE