mi nilikuwepo UDOM siku hostel za kwanza kabisa zinahamiwa za college of humanities ... ni typical na mabibo hostel. ilikuwa siku ya jumamosi ndio wanafunzi wanaingia, ijumaa tulikaa na uongozi wa chuo kuwaeleza kuwa majengo hayajafanyiwa testing yeyote hata ya umeme kwani umeme ulikuwa umeunganishwa siku hiyo hiyo ya ijumaa (kumbuka hitilafu yaweza tokea). na maji yaliunganishwa siku wanafunzi wanaingia, ilikuwa aibu. mabomba ya maaji yanavuja, vyoo vinavuja, kulinuka kote kama chooni. kisa nini haraka. we fundi yuko chooni anamalizia bomba anaona mtu wa gorofani kaflush na vitu vyaja.
siasa inapeleka mambo ovyo kuliko hali halisi, hiyo shida ya maji ilionekane kama miaka 3 iliyopita tatizo wanasubiri kila mwaka wanafunzi wakiongezeka nao waongeze bomba 1. mi nadhani huduma za maji na umeme from day 1 ilitakiwa ziwe na uwezo wa kukidhi idadi ya mwisho na ziada.
ni project ya maana sana na nzuri ila utekelezaji wake unasiasa sana hata kwenye maamuzi ya kitaalam