Wizara ya Ardhi
Govt Institution
- May 14, 2024
- 306
- 165
Algiers, Algeria – Julai 17, 2025
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Geophrey Mizengo Pinda (Mb), ameiwakilisha Tanzania katika Mkutano Mkuu wa 44 wa mwaka wa Taasisi ya Shelter Afrique, uliofanyika jijini Algiers, Algeria kuanzia Julai 15 hadi 17, 2025.
Mkutano huo wa siku tatu ulilenga kujadili fursa za upatikanaji wa mikopo nafuu kwa ajili ya ujenzi wa nyumba bora na za gharama nafuu kwa nchi 44 wanachama wa taasisi hiyo ya fedha ya maendeleo ya makazi barani Afrika.
Mhe. Pinda ameambatana na Dkt. Upendo Matotola, Mkurugenzi wa Kitengo cha Milki Wizara ya Ardhi,
Bw. Awadhi Salim, Mkurugenzi Msaidizi wa Nyumba na Uendelezaji Milki, Bw. Richard Ndeona na Meneja wa Hazina kutoka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).
Shelter Afrique ni taasisi ya Kimataifa iliyoanzishwa na nchi 44 wanachama kwa lengo la kuchochea maendeleo ya sekta ya makazi na miji Afrika.
Tangu mwaka 2023, taasisi hiyo yenye Makao Makuu yake jijini Nairobi, Kenya imeanza kufanya kazi kwa mfumo wa benki na sasa inajulikana kama Shelter Afrique Development Bank (ShafDB), ambapo Tanzania ni miongoni mwa wanahisa wake.