Pinda ambeba Rostam Igunga

Huyu naye njaa tu! ati mtoto wa mkulima....@#@#@#...aliingia masikini atatoka tajiri la kutupwa...wait and see...Mkapa style.....Mr. Clean, na tume ya Warioba chapchap...mmmh...alitoka kaoza! Fisadi la kutupwa!....Ndio maana mimi nasema, watz sasa kila mmoja ni fisadi mtarajiwa....ni nafasi tu mtu anaharibu mda mfupi. Aibu kwako Wazuri mkuu kutumia ziara ya kiserikali kumfasafisha mwanasiasa aliyeoza!
 


Waamuzi ni wananchi wa igunga si vinginevyo pia waziri mkuu hajakosea kwani wasimpime mtu kwa maneno na shutuma za bunge bali amewafanyia nini kwa kipindi chote alipokuwa anawawakilisha na pia si kwa RA tu bali majimbo yote wananchi wawapime wabunge wao kwa yaliwaliofanya kutoka na ahadi walizotoa wakati wanaomba ridhaa ya kuwawakilisha.

Bravo pinda bravo ccm
 
Nimekumbuka kauli ya Mwalimu,..viongozi wetu na hatima ya taifa letu..kusema kweli itakuwa ngumu sana kuendelea kama viongozi tuliokuwa tunawaamini kama Pinda kuingia kwenye mtego wa mafisadi wa chama chake,wengi tulisadiki kwamba Pinda si miongoni mwa wanamtandao ambao wameifikisha nchi yetu hapa ilipofikia,lakini sasa polepole naona ameamua kjiunga na kundi hilo hata miaka mitatu haijapita,..kwa kauli hii ya kutaka wananchi wa Igunga waendelee kumchagua Fisadi ni kuwadhalilisha kwamba hawajui chochote kuhusu uovu unaofanywa na mbunge wao dhidi ya fedha za walipa kodi wakiwemo wanaigunga wenyewe.
 
But he is right kwamba wananchi wake wapime kwa yale aliyofanya Igunga kama katimiza yale aliyoaidi what wrong to chose him again,me sioni kosa la PM
 
mgololafinyonge,
Capacity charge za Richmond alizokuwa anachukua RA ulikuwa wizi kwa kuwa hapana shaka tena, na Pinda anajua kuwa richmond ilikuwa kampuni hewa ya kitapeli. Kama waziri mkuu, tena mwanasheria kwa taaluma, sehemu pekee ambako angemsaidia RA kufika ni gerezani. Short of that he has failed the Tanzanians.

https://www.jamiiforums.com/members/mgololafinyonge.html
 
Serikali alioiweka madarakani RA ndio iliomteua Pinda kuwa WM. Na huenda Pinda alikuwa mwanamtandao wa kimyakimya kama tulivyokuwa wengi! Na sasa Pinda ndio ameanza kuwa mwanasiasa wa Tz. Unafiki kidogo, uongo kidogo, kuuma na kupuliza,........
 
Serikali alioiweka madarakani RA ndio iliomteua Pinda kuwa WM. Na huenda Pinda alikuwa mwanamtandao wa kimyakimya kama tulivyokuwa wengi! Na sasa Pinda ndio ameanza kuwa mwanasiasa wa Tz. Unafiki kidogo, uongo kidogo, kuuma na kupuliza,........
Kwa nchi inayotawaliwa na UWT usishangae huyu alikuwa mwanamtandao mzuri tu
 
Pinda dole lake alivyoliweka kikwetu ni tusi zito sana!!
Kazi kweli kweli. Umenichekesha sana. Nadhani hapa alikuwa anatoa ujumbe kwa wanaombeza boss wake pale Igunga na watanzania wanaompinga RA
 
Hivi huo si ndio ufisadi wenyewe? Naona kama tayari ccm wameanza kampeni kupitia mlango wa nyuma. Rostam mjanja yule, anajua Pinda hataki rushwa kamkatia msaada fulani, naye Pinda anarudisha fadhila, hawezi kurogwa kiasi hicho. Anajua implication yake maana ni mwanasheria huyo.

Haya, yetu macho.
 
Pinda, sijawahi kuwa shabiki wake, kutoka moyoni , na bado namuona kuwa yeye, na wanaCCM woote, ni sehemu ya tatizo ktk nnchi hii,
KALELEWA PALE IKULU, amekulia pale Ikulu, amechangia kuifikisha nnchi hapa ilipo, hana tofauti na mafisadi wengine woote ambao ni matunda ya kusameheana, na kuyaacha mambo yapita ilihali ugali wao wa kila siku unapatikana,
 
Sasa hapa kuna nini jipya maana mimi naona kuwa ni kusafishana kwenda mbele na hivyo ndio maana nasema kuwa mambo haya ni ya ajabu sana katika historia ya Taifa letu Tanzania. Tutawahukumu siku moja. Mungu saidia Taifa la Tanzania katika ulimbukeni wa mambo ya ajabu na serikali yetu ya kifisadi na mfumo ule ule. Kuna ajenda yuma ya hapa. RA ndiye anafadhili sana Chama chao
 
I told u guys, Nchi hii inaendeshwa na Rostam, hakuna cha Raisi wala Waziri Mkulu Period!. Thats why he is above the law! Shame on them!
 
Duh huyo Rostam ni moto wa kuotea mbali. Hivyo keshamwingiza Pinda kwenye pay roll yake. Hivi viongozi wetu wamerogwa au ni nini hata kujiabisha namna hii??????

Walahi kwa mtu mwenye akili timamu na cheo cha uwaziri mkuu hawezi kupeleka p***b* zake kwenda kumpigia kampeni mtu anaetuhumiwa kwa ufisadi nchi nzima, aaaaaangriiiiiiiiiiiiiii shame on u Pinda.
 
Sishangai kwani huyu nilisha mdharau toke wakati ule alipolia bungeni, Amna kitu hapa, RA ni fisadi anayejulikana ata mtoto mdogo anajua sasa wewe una mtetea tukuelewe vipi? Na wewe si FISADI.
 

Ni kweli waamuzi ni wananchi wa Igunga sasa Halmashauri wanausika na nini?



Hata hivyo hakujibu ombi la wananchi hao la kumwomba mbunge huyo kubaki jimboni humo. Pinda juzi mara baada ya kuwasili mjini hapa alizungumza na watendaji wa halmashauri ya wilaya ya Igunga na kuwaomba kutomkataa mbunge huyo.


Wafanyakazi wa halmashauri kwani wao no mawakala wa ccm?
 
Naona ipo kazi kubwa kuliko tulivyofikiri kuirudishai hii nchi utawala wa sheria!
Je waraka wa wapiganaji utafanya kazi? Je, ni kweli kuwa hao wapiganaji wapo?
Hapa suluhisho ni kuhakikisha kuwa utawala huu haurejei madarakani! Lakini, ni kwa vipi?
 

Teh teh teh...Kaiyanza Mizengwe Mpinda Haki.....Money is trully a root to all evil.
 
Nashindwa kuelewa kama kiongozi mkuu wa shughuli za bunge anaweza kuwaambia wapiga kura wasisikilize yaliyozungumzwa bungeni. Je bunge ni kjiwe cha kuwapumbaza wapiga kura? Inawezekana ndo maaana swala la Richmond likafunikwa kwa msingi wa funika kombe mwendawazimu apite. Kidemokrasia hili halikubaliki kabisa la kuwashauri watu kuchagua yai bovu ingali wao wenywe wanaliona kuwa ni viza. Naomba viongozi wa aina hii waache kuwakwanza wanachi kwa njia hizi. Vile vile ningependa kuwasihi wapiga kura wamchague wanayemjua kuwa atawanyia nini na siyo kumchaua mtu anayetaka nyinyi muwe ngazi yake ya kujipatia mali kifisadi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…