Pinda ambeba Rostam Igunga


Kama Mtanzania ni wajibu wangu kuwaheshimu viongozi "halali" walioko madarakani. Lakini mara wanapozungumza huwa najikuta nikijiuliza ni kivipi wapo hapo walipo,yani madarakani.

Nimeshangazwa sana na hatua ya mh waziri mkuu kuthubutu kusema eti vita dhidi ya ufisadi ni ugomvi binafsi baina ya viongozi!Nimechoshwa!

Amedai kuwa viongozi hao wanatumia muda mwingi kugombana badala ya kuwatumikia wananchi masikini,madai hayo yamenifanya nijiulize uwezo wa mh waziri mkuu wa kufikiri,kwasababu ni wazi kabisa kwamba "ugomvi" huo baina ya viongozi ni kwasababu ya issue zinazochangia umasikini,yani issue za ufisadi,na kwahivyo hiyo kupingana na mafisadi na kuupinga ufisadi ni sawa kabisa na kuwatumikia wananchi masikini ambao walitakiwa wanufaike na rasilimali za taifa na sio baadhi ya "viongozi" na watu flani flani.....Kwenda huko Morogoro na kuzungumza kama vile yuko nje ya nchi ni jambo lakusikitisha,kwasababu ni wananchi wa nchi nyingine tu ndio wanaotakiwa wasisikilize yanayosemwa bungeni.
Habari hii kama ni ya kweli basi ni masikitiko makubwa sana!

Inashangaza kuona kwamba waziri mkuu anataka eti viongozi na wananchi wasiopenda ufisadi waendelee kuwapenda mafisadi na kushirikiana nao,bado nasema kuwa nawaheshimu viongozi wetu "halali" walioko madarakani,lakini kama hakuna hatua madhubuti zitakazochukuliwa ili ukweli wote uwekwe bayana na uwajibikaji ufuatie,bado kauli kwamba viongozi hawa ama wale hawafai kwasababu ni "Mafisadi" bado zitakuwepo,haziwezi kwisha tu eti kwasababu waziri mkuu kasema.....Nashangazwa zaidi kuona kwamba haya yanafanywa na wanafunzi wa mwalimu Nyerere,kama ni karata mzee wa watu kweli alilamba magalasha ya kutosha.

Na hayo yote ya asilimia 20 blah blah ni uongo mtupu....Hiyo dhana ya kwamba eti vita dhidi ya ufisadi ni maslahi binfasi sijui kaitoa wapi?EPA,Richmond,Kagoda etc ni maslahi binafsi?

Kazi Ipo watanzania wenzangu.
 
Tuliambiwa na JK na Pinda mwenyewe kwenye mikutano ya Bunge kuwa mswaada kuhusu kutengansha siasa na biashara upo njiani;na walituambia utapelekwa bungeni kwenye kikao kijacho cha Bunge ambapo wafanyabishara HAWATARUHUSIWA KUGOMBEA nafasi za kisiasa za kuchaguliwa!

Sasa kama Rostam Azizi anajulikana kuwa ni mfanyabiashara mkubwa,iweje PM Pinda audharua waraka aliotueleza wenyewe watz?Ndiyo kusema ule mswaada wa kukataza wafanyabishara kugombea hauletwi tena Bungeni kupitishwa na hatimaye Rais autie saini kuwa sheria?

Mwenye dondoo kuhusu mswaada huu please atueleze!
 
Msisikilize kile kinachosemwa bungeni juu yake. Bunge lina mambo yake, mimi kama Waziri Mkuu nafahamu mambo ya pale bungeni,” alisema Waziri Mkuu.

Hii inamaanisha kwamba kinachosemwa juu jake pale bungeni na wabunge waliotumwa na wananchi ni porojo, uongo, na kwamba wabunge hawana hoja yeyote ya msingi na kwa maana hiyo basi kwa kuwa yeye anayafahamu mambo ya pale bungeni kwamba ni porojo porojo tu za kiasa, na hivyo hakuna la manufaa linanalojadliwa pale bungeni.
Kwa mtazamo huu hatufiki! Kama waziri kubwa sana anachukulia masuala nyenti kama hili kwa urahisi rahisi hivi! Kwanza hayo ni madharau! Kwamba bwekeni lakini hakuna mnachosema ni pumba tu! No wonder serikali ilikuwa reluctant kuchukua hatua kwa mafisadi wa Richmond, Maana mtazamo ni huu huu! Mzee Makwaiya wa Kuhenga tutafika kweli?
 
mheshiwa mwenye nchi si alisema mambo kupigiana ndogo ndogo hayajaanza ,huyu pinda iweje aanze chokochoko hizi mapema ?

Jana kule Nzega kawapiga na changa la macho alisema hivi "Inshallah JK amenichagua mimi kutoka western province na kama atanichagua baada ya uchaguzi huu unaokuja basi barabara ya Nzega mpaka Tabora, Manyoni-Itigi, na kigoma mpaka kwangu Rukwa zitaungana" baada ya hapo akachukua asali yake na vitenge alivyopewa zawadi mtoto wa mkulima akajikata kiaina kuelekea kwa 6
 
Kwa mawazo yangu, Serikali pamoja na chama tawala CCM haioni maovu ya huyo Rostam, na kama inaona, basi inayaesabu hayo maovu kama ni sehemu ya Serikali.
Rostam ndiye anaye kifadhili chama kilichowaweka hao viongozi wakuu wa Nchi madarakani. Wasipomsafishia njia RA, ni kujimaliza wenyewe, kwani akianguka, basi na wao wataanguka tu.
 
Wako KISIASA ZAIDI uchaguzi ni October jamani, hebu tuongee mambo ya maana
 
Pinda hana kosa kumbeba RA kwa wananchi..ni kada wao tena anayejitoa zaidi kufanikisha malengo yao.
 

Ukimsoma waziri mkuu kwa makini utangudua kuwa mwelekeo wa serikali ni kwamba wabunge ni lazima wawe matajiri,kwasababu anatoa msisitizo kwa wabunge hao kutumia utajiri wanaoupata "Kuwagawia" wananchi kiaina na wakati huo huo wananchi hao wasiwe na haja ya kufuatilia yanayoendelea bungeni,wala hawatakiwi kusikiliza kinachoendelea huko bungeni kwasababu ni uzushi......Na kwahivyo basi mbunge ama mgombea ambaye hawezi "Kutumia fedha" hawezi kamwe kuchaguliwa ama hata kupitishwa na ccm kwasababu huyo atakuwa anajali mambo ya bungeni zaidi ya "kutumia fedha" Dili ni uwe na fedha za kuwapa masikini,basi.
Ni hatari.
Alisema viongozi wa serikali wanawajibika kutumia fedha wanazozipata katika kuwasaidia masikini wanaowaongoza badala ya kujilimbikizia fedha huku wakizungukwa na watu masikini jambo ambalo ni hatari.
 
huyu ndiye mtoto wa mkulima? kazi ya uwaziri mkuu imemshida sasa kadakia ya kusafisha mafisadi - duh shughuli tunayo watanzania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…