jmushi1
Platinum Member
- Nov 2, 2007
- 26,329
- 25,263
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alionya tabia ya viongozi kujenga uhasama baina yao kwamba hatua hiyo inawafanya kutumia muda mwingi katika kugombana badala ya kuwatumikia Watanzania masikini.
Alisema serikali haitavumilia kuona viongozi wanatumia muda mwingi katika ugomvi wakati Watanzania wanakabiliwa na matatizo mbalimbali ukiwewo umasikini.
" Kama kweli tunataka kuwahudumia wananchi masikini hawa ni lazima tuwe na ushirikiano sisi viongozi kwanza. Idadi yetu sisi Watanzania ni kama milioni 40 hivi au na zaidi kidogo. Hata hivyo asilimia 80 ni wakulima na asilimia 20 ndio sisi viongozi.
"Iwapo sisi asilimia 20 tutajali zaidi maslahi yetu na kuwasahau hawa masikini ipo siku hawa watu watatupiga marungu," alisema Waziri Mkuu.
Alisema viongozi wa serikali wanawajibika kutumia fedha wanazozipata katika kuwasaidia masikini wanaowaongoza badala ya kujilimbikizia fedha huku wakizungukwa na watu masikini jambo ambalo ni hatari.
Kama Mtanzania ni wajibu wangu kuwaheshimu viongozi "halali" walioko madarakani. Lakini mara wanapozungumza huwa najikuta nikijiuliza ni kivipi wapo hapo walipo,yani madarakani.
Nimeshangazwa sana na hatua ya mh waziri mkuu kuthubutu kusema eti vita dhidi ya ufisadi ni ugomvi binafsi baina ya viongozi!Nimechoshwa!
Amedai kuwa viongozi hao wanatumia muda mwingi kugombana badala ya kuwatumikia wananchi masikini,madai hayo yamenifanya nijiulize uwezo wa mh waziri mkuu wa kufikiri,kwasababu ni wazi kabisa kwamba "ugomvi" huo baina ya viongozi ni kwasababu ya issue zinazochangia umasikini,yani issue za ufisadi,na kwahivyo hiyo kupingana na mafisadi na kuupinga ufisadi ni sawa kabisa na kuwatumikia wananchi masikini ambao walitakiwa wanufaike na rasilimali za taifa na sio baadhi ya "viongozi" na watu flani flani.....Kwenda huko Morogoro na kuzungumza kama vile yuko nje ya nchi ni jambo lakusikitisha,kwasababu ni wananchi wa nchi nyingine tu ndio wanaotakiwa wasisikilize yanayosemwa bungeni.
Habari hii kama ni ya kweli basi ni masikitiko makubwa sana!
Inashangaza kuona kwamba waziri mkuu anataka eti viongozi na wananchi wasiopenda ufisadi waendelee kuwapenda mafisadi na kushirikiana nao,bado nasema kuwa nawaheshimu viongozi wetu "halali" walioko madarakani,lakini kama hakuna hatua madhubuti zitakazochukuliwa ili ukweli wote uwekwe bayana na uwajibikaji ufuatie,bado kauli kwamba viongozi hawa ama wale hawafai kwasababu ni "Mafisadi" bado zitakuwepo,haziwezi kwisha tu eti kwasababu waziri mkuu kasema.....Nashangazwa zaidi kuona kwamba haya yanafanywa na wanafunzi wa mwalimu Nyerere,kama ni karata mzee wa watu kweli alilamba magalasha ya kutosha.
Na hayo yote ya asilimia 20 blah blah ni uongo mtupu....Hiyo dhana ya kwamba eti vita dhidi ya ufisadi ni maslahi binfasi sijui kaitoa wapi?EPA,Richmond,Kagoda etc ni maslahi binafsi?
Kazi Ipo watanzania wenzangu.