Pinda amshukia Zitto

hapa PM amecheza ovyo kabisa, ananikumbusha enzi za mzee Malecela. Siasa mbovu kama hizi hazipaswi kuonekana kwa PM mambo mengine awe anawaachia akina Chiligati na Hiza.
 
Inatia uchungu sana kwa kuona mtu makini kama yeye naye anaingia na kauli kama wakini Makamba na Wakina Tabwe Hizza na wangine wengi mwenye mawazo mgando juu ya Democrasia ya Kweli
 
Alelluya!

Ni Hakika kuwa PM kafanya Kosa fulani katika kuadress hili jambo na uchama umemuelemea kidogo, lakini watu wa Mungu lazima Muelewe huyu ni mwanadamu ambaye kapewa hiyo nafasi na mtu tuliye mpa mamlaka yote ya nchi hii, anahitaji msaada wa maombi kutoka kwako ili yale anayoyasema na kushauri yawe ni kwa maslahi ya Taifa la Tanzania, unajua linapokuja swala la utaifa Si Pinda wala Zitto binafsi anaye pata hasara au faida ila ni ya kwa ujumla wa Taifa letu. Hivyo tuombe sana yote yanazungumzwa na viongiozi wetu yawe ni kwa manufaa ya Taifa na siyo kwa manufaa ya Chama.
Ninategemea kuwa uwanja huu utatumika kwa maslahi ya taifa na siyo Chama, tunapokosoa tuwe makini kidogo ili utulivu iliopo udumu na kila mtu afanikiwe kwa hilo.
Zaidi nawapongeza wana JF KATIKA kutonyamazia maovu ndani ya taifa letu. Mungu wangu na azidi kuwatia Nguvu ya ziada na damu ya Yesu ilifunike taifa letu.
Mbarikiwe na Bwana!
 
Ni Kweli kabisa ila lazima naye kama Binadamu akosolewa maana kama siyo Miungu watu hivyo ni Haki yetu sisi Kusema na Kuwasemea, Lazima angepaswa kuadress vizuri au kujibu vizuri, na tena Kwasababu hii inaongoza sana kufanya na kufanya hata Wakuu wa Wilaya na Makada huko Wilayani kuwa Miungu watu, Ina Impact kuwa sana katika hili
 

Labda alijisahau kuwa ana address Bunge na siyo kamati ya CCM.
 
Ni Kweli na ndio maana kuna wabunge wengi sana wa CCM, Pale Upinzani ni kama 46 hivi Wote ni CCM, Tunaweza kusema kuwa ni Kamati ya CCM ya Siasa na ndio maana tunaona vitu vya ajabu toka Bungeni na Kauli Tata kama hizi, Haya Mambo ni ndani ya Chama, Kwani Mikopo watailipa wao tu CCM, Watu wote ni Watanzania na hata Katiba inasema hivyo. Sasa Haya Yanatoka wapi?? Huku ni Kuwatisha watu na wapinzani wa Kigoma, Kumbe ni Heri kuchagua Upinzania kuliko CCM.
 
Aleluya!
Hakika Josh hapo tunaenda sambamba, Hii nchi ni yetu na siyo ya CCM, na mambo haya ya utata ndio yanasababisha wapinzani kuwachachafya CCM na kuweka maneno makali. Hivyo ujue Ukweli unauma pia!
Mungu wetu aendelee kuwapa hekima na busara ya kulitetea nma kulinusuru taifa letu.
Mbarikiwe na Bwana!
 
Cha msingi hapa ni Kwamba CCM waache Kujigamba na kufanya wao ndio mwisho na Mwanzo, Kama Maendeleo kote inabidi yapelekwe na sio majimboni ya CCM, Bila ya Upinzani wa Kweli tunazaa Serikali Legelege na pia ni Hasara kwa Taifa letu na Vizazi vyetu wote.
 
Mizengo Pinda said:
"Mheshmiwa Spika labda niseme hivi serikali ni ya chama chetu, fedha ni za serikali ya CCM na barabara zinajengwa na CCM, labda mheshmiwa Zitto pamoja na Chadema yake wangeniambia tu, Waziri serikali yako imejitahidi sana".

Sasa mameno kama haya anayasema Waziri Mkuu hivi kweli tutafika huko tuendako??? Nini maana ya Upinzani ndani ya Tanzania. Sisi watanzania nadhani tutakuwa tumelogwa hii sio bure...
 
Haya ndiyo matatizo ya kuwa na wasanii kwenye serikali badala ya viongozi. Yaani Pinda naye anaongea kama wale madiwani wao waliokimbia umande na kuishia darasa la pili (Wanaoandika barua kwa kuchanganya herufi kubwa na ndogo) na baadae kujiingiza kwenye siasa kwa kuwa na uwezo wa vijembe majukwaani tu.

Unaposema hela za CCM, kwa kuwa serikali ni ya CCM, unakuwa umebagua wale wasio na chama au walio vyama ambavyo si CCM, ambao kila siku wanalipa VAT, PAYE na kodi kibao. Je hawa wakienda kushitaki kuwa hawataki kulipa michango ya CCM kwa njia ya kodi kwa sababu wao si waumini wa chama hicho Pinda atapata la kujibu?.

PINDA EEE!, Pesa ni za watanzania ambazo serikali ni custodian tu, Pinda au ndiyo kutetea nafasi kwenye uteuzi ujao? Maana haya sasa yamekuwa low kuliko ya "NDEGE YA UCHUMI"
 
Last edited:
Umesema ukweli kabisa maana kama mtu hana chama atakwenda wapi?? ndio maana tunasema kuwa Katiba ya Tanzania inalazimisha watu wajiunge kwenye vyama hata kama hawataki kabisa, PM asingesema maneno kama ya watu wengine tuliwazoea kwenye Siasa miaka nenda rudi, Je Kura zote walipigiwa na Wana CCM tu??? Mbona anasema kama vile Hajui nini cha kufanya na mgawanyiko wa Madaraka ya Katika Tanzania
 
Duh! Pinda kachemsha big time!..
Inaonyesha hafahamu jinsi Utawala wa vyama vingi unavyofanya kazi ktk ujenzi wa nchi..Yaani nemesoma na nimeshindwa kabisa kumwelewa, kaazi kweli kweli!
 
Duh! Pinda kachemsha big time!..
Inaonyesha hafahamu jinsi Utawala wa vyama vingi unavyofanya kazi ktk ujenzi wa nchi..Yaani nemesoma na nimeshindwa kabisa kumwelewa, kaazi kweli kweli!
Au ni makosa ya Uandishi wetu na yupo kwa ajili ya Kiasiasa zaidi, maana hata sisi hatuamini kama kweli yeye NDIYE MKULIMA wetu na anajua kweli utawala wa Kisheria na Vyama vingi.. au ndio mtindo wa Kampeni tu
 
fedha ni za serikali ya CCM

Hivi hawa watu concept ya stewardship wanaielewa? Wanaelewa kwamba wao ni custodians tu? No wonder wanafuja mali kwa sababu wanaamini ni zao!

Pinda inabidi arudi kusoma ile hotuba excellent ya Nyerere alivyokataa tabia ya kuita "dereva wangu" au "kampuni yangu" kwa vitu vya umma, this shows Pinda to be what I have always said despite the leeway he is afforded, a security apparatus nincompoop way out of his league trying to sound statesmanlike, coming out all wrong.
 
Last edited:
Pengine ndio Kupanda na Kushuka kwa Presha za Uchaguzi mzee wangu, maana yeye mwenyewe alisema kuwa presha inapanda na kushuka wao wanajua kuwa washindani wao ni CHADEMA
 
[QUOTE=



"Mheshmiwa Spika labda niseme hivi serikali ni ya chama chetu, fedha ni za serikali ya CCM na barabara zinajengwa na CCM, labda mheshmiwa Zitto pamoja na Chadema yake wangeniambia tu, Waziri serikali yako imejitahidi sana"aliongeza Waziri Mkuu.



sasa jamani kumbe fedha ni za serikali ya ccm na wala sio za walipa kodi sasa mbona kila siku tunalia na ccm wakati wao ndio wanaifadhili nchi yetu? au mie nimeelewa vibaya? au waziri mkuu alitakiwa badilisha kauli hapa? nisaidieni jamani kama haya maneno ya waziri mkuu yako sawa kwamba " fedha ni za serikali ya ccm na barabara zinajengwa na ccm"
 
Au ni makosa ya Uandishi wetu na yupo kwa ajili ya Kiasiasa zaidi, maana hata sisi hatuamini kama kweli yeye NDIYE MKULIMA wetu na anajua kweli utawala wa Kisheria na Vyama vingi.. au ndio mtindo wa Kampeni tu

Ah mkuu wangu wewe hiyo mtoto wa mkulima it was just a gimmick. Si unajua kabla yake waziri mkuu ailieondolewa ilikuwa kwa ajili ya nini? Pinda walitaka tu kumuonyesha kama mtu wa hali ya kawaida ambae hana utajiri wa EL. Unafikiri baada ya kuwa waziri mkuu yeye "mtoto wa mkulima" tena? Ile ilikua janja tu ya wakati ule watu wafurahie uteuzi wake ili JK asiwe under fire kwa kuchagua wenzie ambao ni matajiri. Just a political move & political propaganda.
 

Si unajua tena Pinda alipata "zali la mentali" kuwa waziri mkuu ndiyo maana sasa madaraka yanamchanganya. "Mtoto wa mkulima" kashatoka shambani sasa.
 
Pinda kakosea kwasababu walisema ccm ina watu 5mil.Kwanza wengi wao ni disadvantegious wa vijijni.Kwa hiyo hata kodi ya mapando, ya wafanyakazi hawana.Pesa za ccm zitolewazo na mafisadi akini RA zinafadhali shughuli za ccm za kurubuni wanawake kwa kanga wakati wa kampeni.Kamwe hazitumiki kwa shughuli za maendeleo ya taifa.Kwa hiyo barara imejengwa na pesa zetu wafanyaki na walipa kodi wote.haina uhusiano na ccm
 
this is embrassing kwa PM kuingia kwenye siasa za punch and Judy

kwani kuna ubaya gani angeyamaza?

this is so low, yeye angesema wanatekeleza ilani ya chama ya 2005 kungekuwa na ubaya gani?


Hivi Zitto akiamua kujibizana naye atamweza?
Huwezi kujua bwana, labda na yeye homa ya uchaguzi imeshaanza kupanda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…