Pinda amshukia Zitto

Pinda amshukia Zitto

Pinda homa ya uchaguzi inapanda na kushuka inapanda na kushuka, Sisi hizi amegeuka na kuwa mtoto wa Tajiri au vibosi wa CCM maana huwezi kusema kuwa ni mtoto wa Mkulima na walisema hivyo kwa ajili ya kujitofautisha na EL
 
"barabara hiyo"alisema Pinda na kuongeza:
"Mheshmiwa Spika labda niseme hivi serikali ni ya chama chetu, fedha ni za serikali ya CCM na barabara zinajengwa na CCM, labda mheshmiwa Zitto pamoja na Chadema yake wangeniambia tu, Waziri serikali yako imejitahidi sana"aliongeza Waziri Mkuu.

Pinda alisema, alitegemea Zitto angekiri kuwa serikali ya CCM imempa barabara bila ya kuonesha ubaguzi wa kiitikadi za kisiasa pamoja na kwamba Zitto ni wa chama kingine siasa.
Source: Mwananchi Read News
Hivi Pinda anamaanisha nini hasa? kwa kusema fedha ni za serikali? na eti serikali ni ya CCM. Hivi yamekuwa hayo jamani, yaani fedha si za mtanzania mlipa kodi wa nchi hii. Na je, serikali pia si ya wananchi? eti ya CCM? CCM wamepewa dhamani tu ya kuisimamia. Kwa maoni yangu Pinda anamatatizo hasa ya ku-reflect anachokisema.
 
Hivi Pinda anamaanisha nini hasa? kwa kusema fedha ni za serikali? na eti serikali ni ya CCM. Hivi yamekuwa hayo jamani, yaani fedha si za mtanzania mlipa kodi wa nchi hii. Na je, serikali pia si ya wananchi? eti ya CCM? CCM wamepewa dhamani tu ya kuisimamia. Kwa maoni yangu Pinda anamatatizo hasa ya ku-reflect anachokisema.
Pinda naye kazungumza OVYO OVYO Bungeni kama yule naibu waziri wa Fedha.
 
Pengine akili ya Pinda imemtuma kufikiria kuwa, maadam nchi yetu inategemea misaada basi hata wananchi wa Kigoma walichopewa ni msaada toka chama tawala CCM.. sijui wao wamewzikusanya toka wapi! Ndio maana maswala ya Ufisadi hayawezi kupatiwa dawa kwani CCM wanafikiria kwamba zile fedha zinazoibiwa ni zao wenyewe hivyo kama ni uchungu inatakiwa CCM ndio iwe na uchungu zaidi..
Ama kweli viongozi tunayo yaani sikutegemea kabisa!
 
Pinda anazidi kupinda.....ametumia lugha ya kuudhi...Spika alitakiwa kumchukulia hatua. Kwa upeo wake mdogo hawezi kutofautisha chama na serikali. Angekuwa ni katibu kata ambaye hakuona darasa ningemwelewa lakini si Pinda anayejinadi kuwa ni "mtoto wa mkulima".
 
"Mheshmiwa Spika labda niseme hivi serikali ni ya chama chetu, fedha ni za serikali ya CCM na barabara zinajengwa na CCM, labda mheshmiwa Zitto pamoja na Chadema yake wangeniambia tu, Waziri serikali yako imejitahidi sana"aliongeza Waziri Mkuu.

Source: Mwananchi Read News

Hapa nafikiri (kwa mawazo yangu) Waziri Mkuu kachemka na anapaswa kuwaomba radhi watanzania. serikali ni ya watanzania wote ila inaongozwa na CCM. Serikali hii inategemea kodi ya mtanzania kuendesha shighuli zake. Si wana CCM tu ndiyo wanalipa kodi ila hata wa vyama vingine. Na historia pamoja na ushahidi umeonyesha wengi wa wakwepa kodi ni wanachama wa CCM. sasa leo PM huwezi kutamka kuwa fedha ni za serikali ya CCM, watanzania wote wana haki ya kupata maendeleo kutokana na kodi wanazolipa.
PM, waombe radhi watanzania kwa tamko hilo.
 
this is embrassing kwa PM kuingia kwenye siasa za punch and Judy

kwani kuna ubaya gani angeyamaza?

this is so low, yeye angesema wanatekeleza ilani ya chama ya 2005 kungekuwa na ubaya gani?


Hivi Zitto akiamua kujibizana naye atamweza?

ehhhehe...Zitto sasa naona anaanza kutafuta kwa kuibukia baada ya Dowans na zile trip za Canada

Bora akubali tuuu kung'atuka kama ni kweli ilivyowekwa humu JF siku zilozopita
 
Ndio maana maswala ya Ufisadi hayawezi kupatiwa dawa kwani CCM wanafikiria kwamba zile fedha zinzoibiwa ni zao wenyewe hivyo ka a ni uchungu inatakiwa CCM ndio iwe na uchungu zaidi..
Ama kweli viongozi tunayo yaani sikutegemea kabisa!

Ndio maana mimi siku zote huwapigia kelele CCM - wote ni wezi, wadokozi na wanyang'anyi watupu. Walianza kwa kuipora katiba ya Jamhuri kuwa yao na hivyo kuwa na karata muhimu ya kuhalalisha vitendo vyao vya unyang'anyi na ufisadi. Kilichofuatia walipora mali zote zilizochumwa kwa nguvu za wananchi na kuzigeuza za genge hili la CCM kuanzia ofisi za serikali, viwanja vya michezo, mashirika ya Umma hadi jumuiya za wazalendo kama vijana, wazazi na mengineyo.

Kwa kiu chao na ulafi usio mpaka, wamefikia hatua ya kudai kuwa hata kodi zetu wananchi tunazolipa ili serikali ituletee maendeleo wanaanza kuzikomba na kuziita zao. Wamekomba benki kuu kupitia kampuni feki za Kagoda, Deep Green, Tangold na mengine mengi, na leo Waziri Mkuu kwa jeuri na mikogo anakiri bungeni kuwa wana haki ya kufanya hivyo kwa kuwa ni hela za serikali ya CCM - Waziri Mkuu Mizengo Pinda, kwa mbwembwe anatamka haya:-

Mizengo Pinda said:
Mheshmiwa Spika labda niseme hivi serikali ni ya chama chetu, fedha ni za serikali ya CCM na barabara zinajengwa na CCM, labda mheshmiwa Zitto pamoja na Chadema yake wangeniambia tu, Waziri serikali yako imejitahidi sana.

Ni kwa nini Pinda alikosa ujasiri wa kusema CCM ndio walikomba pesa Benki Kuu ? Huu undumilakuwili ni wa nini kwani pesa si zao ? Kwani angekubali hilo angefanywa nini na serikali ni yao, Raisi ni wao, bunge ni lao na mahakama ni yao - aliogopa nini ? Polisi ni wao, TAKUKURU ni yao, Tume ya Uchaguzi ni yao, Jeshi ni lao, Usalama wa taifa ni wao. Tunashangaa nini Wazee kama John Samwel Malecala wanapoibuka na kudai CCM itakaa madarakani hata kwa miaka mia !! Wezi na mafisadi wote ni wao 😡
Kinachosikitisha na kutia kinyaa
Na ukweli mchungu uliyojaa balaa
Ni kwamba katika uchaguzi ujao
Pamoja na uharamia na uovu wao
CCM chama kichojaa mafisadi
Kinaweza kuibuka na ushindi
Mungu tuepushe na hii laana
Tulifanye angalau lile la maana
Kulitokomeza hili genge la wezi
Watoto wetu waweze kutuenzi.

 
Back
Top Bottom