Pinda atimua watumishi Bagamoyo

Pinda atimua watumishi Bagamoyo

Mayolela

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2009
Posts
384
Reaction score
7
Habari tulizozipata muda mfupi ni kwamba maofisa sita wa Halmashauri ya wilaya Bagamoyo wametimuliwa kazi na WAZIRI MKUU Mh. Pinda leo hii kwa kosa la ubadhirifu wa mali ya umma, na kutojali kero za wananchi.

Wadau mnasemaje katika hili? Maana huko ndio kwa Mh. RAIS JMK.

Wapo wengi sana wa mfano huu, katika maharmashauri hapa nchni.

Pinda asafisha nyumbani kwa JK

Thursday, 21 January 2010 07:21

*Amtimua mkurugenzi, mweka hazina Bagamoyo
*Ni kwa tuhuma za ubadhirifu, kutowajibika

Na Edgar Nazar, Bagamoyo

WAZIRI Mkuu, Bw. Mizengo Pinda amegeuka mbogo na kuwavua madaraka Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Mweka Hazina na maofisa wengine wa halmashauri hiyo kutokana na tuhuma za ubadhirifu wa fedha za maendeleo ya umma na kushindwa kuwajibika ipasavyo.

Mbali ya hatua hiyo, Bw. Pinda alitoa onyo kuwa atakuwa mkali na asingependa kuona yaliyojitokeza katika halmshauri hiyo, ambayo ndio nyumbani kwa Rais Jakaya Kikwete, yakitokea kwingineko na kuwataka wakuu wa wilaya na mikoa kuzitizama halmashauri zao kwa jicho la karibu na kuwabana watendaji ambao wanaonekana kuwa walaji wa fedha za serikali.

Kama hiyo haitoshi, Bw. Pinda pia aliwaonya madiwani kuacha kupenda kuchukua posho kutoka kwa wakurugenzi wa halmashauri zao, hali ambayo inawafanya kuwa sehemu ya wakurugenzi na kushindwa kuwabana wanapoona kuwa wanakwenda kinyume, hivyo aliwataka kuwa wakali kama wabunge wanavyokua katika ukumbi wa bunge.

Hatua hizo za Bw. Pinda zilizoonekana jana alipokutana na viongozi na watendaji wa wilaya hiyo, zimetokana na mapendekezo ya ripoti ya uchunguzi uliofanywa Septemba na Oktoba mwaka jana na Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Serikali (CAG) uliobaini ukiukwaji mkubwa wa kanuni za fedha, uzembe na kushindwa kuwajibika na matokeo yake kuzorota kwa miradi mbalimbali ya maendeleo katika wilaya hiyo.

Watendaji walioshukiwa na Bw. Pinda ni pamoja na Bi. Rhoda Nsemwa (Mkurugenzi Mtendaji), Mweka hazina Bw, Carlo Wage, Mkaguzi wa Mahesabu wa Ndani, Bw, Abdul Mwinyi, Afisa Kilimo, Mifugo na Ushirika, Bw. Anaftal Remtulah pamoja na Ofisa Mipango, Bw. Aloyce Gabriel.

Akizungumza kwa ukali, Bw. Pinda alisema kuwa amechukizwa sana baada ya kupitia ripoti ya CAG na kugundua kuwa kuna matatizo katika kila kona, hali ambayo inaonesha wazi kuwa watendaji wakuu wa halmashauri wanahusika kwa kiasi kikubwa.

"Hawa watendaji ambao nimewavua madaraka kuanzia leo na saa hii, watachunguzwa na kama itathibitika kuwa na makosa ya jinai wanaweza kufukuzwa kazi au hata kupelekwa mahakamani na kushtakiwa au hata kushushwa vyeo walivyokuwa navyo kwa uzembe wa kutofuatilia shughuli za maendeo au kula fedha za serikali," alisema Bw. Pinda.

Watendaji wengine waliopitiwa na panga la Bw. Pinda ni pamoja na Mhandisi wa Ujenzi, Bw. Felix Ngomano, Mhandisi wa Maji, Bw. Galson Rafael ambaye ameondolewa katika nafasi hiyo na kubaki mtendaji wa kawaida baada ya kubainika kuwa hana sifa kushika nafasi hiyo.

Alisema kuwa baada ya kutokea kutokuelewana kati ya Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Bw. Mugesa Mulongo na aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya, Bi. Rhoda Nsemwa juu ya kuwepo miradi hewa, serikali iliamua kuwaleta wakaguzi ili kujua ukweli ambao sasa umebainika wazi.

Alisema kuwa katika ripoti hiyo kumebainika mapungufu makubwa yanayotokana na uzembe wa ufuatiliaji wa masuala ya maendeleo ya watu wa Bagamoyo, Baraza la Madiwani kutokuwa na nguvu ya kuhoji masuala yanayohusu maendeleo ya wananchi wao, hali ambayo imesababisha kuwepo kwa ubadhirifu katika miradi mingi ya maendeleo.

Kwa upande wa Ofisa Elimu wa Wilaya ya Bagamoyo, Bi. Cheka Omar, yeye amewekwa chini ya usimamizi mkali na kama atabainika ameshindwa kazi kutokana na sekta ya elimu katika Wilaya ya Bagamoyo kuwa na matatizo makubwa naye atavuliwa madaraka aliyonayo.

Bw. Pinda alisema kuwa amewavua madaraka viongozi hao kuanzia jana kwa mujibu wa kanuni ya 37 ya Kanuni za Utumishi wa Umma za Mwaka 2003 na watakuwa watendaji wa kawaida, huku wakiwa katika ukaguzi mkuu wa kuangalia kila sekta kama wataonekana kuwa wamefanya ubadhirifu wa makosa ya jinai sheria itafuata mkondo wake.

Bw. Pinda aliwataja watakaouchukua nafasi za watendaji walioondolewa kuwa ni Bw. Samuel Saiyanga kuwa Mkurugenzi Mtendaji mpya akitokea Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Vijijini, Bw. Fidelis Nenetwa atakuwa Mweka Hazina, akitokea Shinyanga.

Wengine walioteuliwa ni Fidelica Gabriel Myovelo, kutoka Wilaya ya Iringa ambaye atakuwa Ofisa Kilimo, Mifugo na Ushirika, Felista Chuki Masamba kuwa Mkaguzi wa Ndani kutoka Wilaya ya Lindi na Prudence Mtiganzi kuwa Mhandisi wa Maji kutoka Wilaya ya Kilombero, Ofisa Mipango mpya atakuwa Bw. Lucas Mweri kutoka Moshi.

Amesema kuwa watendaji hao wanatakiwa kufika mjini Bagamoyo haraka iwezekanavyo na kufanya shughuli za maendeleo kwa ufanisi kwani ana imani na watendaji hao hivyo, watafanya kazi zao kwa uadilifu mkubwa ili kuiendeleza Bagamoyo.

Gazeti hili lilipomfuata aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Bi. Nsemwa alisema kuwa ameridhika na uamuzi huo na kushukuru, huku akisema kuwa angeweza hata kutolewa roho yake kwa kuwa alikuwa anasakamwa sana.

Kauli hiyo ilienda sambamba na ile ya aliyekuwa Mweka Hazina, Bw. Wage ambaye alidai ameridhishwa na maamuzi hayo, ambayo yanamfanya kuwa na amani sasa, bila kufafanua alikuwa akimaanisha nini.
 
...kawatimua tu halafu yamekwisha ama ameagiza wafikishwe mahakamani kujibu tuhuma zao?
 
nimeipata sasa hivi kwenye wapo redio ila kama wamefuja pesa wangebanwa kwanza warudishe chenji bana au wakawataifishwe bana au ndo kampeni ya safisha njia ccm ishinde kama jb ni no pls waiziri mkubwa timua na wa epa
 
Nilijua tu vitakuwa vidagaa fulani tu, hivi rahisi sana kuvitimua huku PM akitafuta ujiko.

Ikija kwa mipapa Pinda anakiri kwamba haiwezi, so what's the use?

Wewe umepewa missile unaenda kuua panya, pick a target your size, hao wa wilaya waachie wakuu wa mikoa.

BS tupu, hamna lolote.
 
..amtimue na Prof.Ndulu kwa kufuja 2.5 bilions za BOT.
 
Nilijua tu vitakuwa vidagaa fulani tu, hivi rahisi sana kuvitimua huku PM akitafuta ujiko.

Ikija kwa mipapa Pinda anakiri kwamba haiwezi, so what's the use?

Wewe umepewa missile unaenda kuua panya, pick a target your size, hao wa wilaya waachie wakuu wa mikoa.

BS tupu, hamna lolote.

Well said mkubwa.......!

Yaani huko bagamoyo macho yake manne ndo yameona ubnadhilifu serikalini? yaani pale mgogoni penyewe hajauona uozo huo? .....shame on him aiseee.....!

Sitetei wouvu wowote, bali mto huo inatakiwa aureplicate na kwa grand corruptions kama zile za Richmonduli, EPAs etc!...sio kukimbilia hao wasiokuwa na ''kinga'' tu........!
 
Nasikia file lipo dpp pccb wameshamaliza kazi yao....Pinda ametumwa kutokana na feedback ya dpp....kifuatacho ni kamata kamata....wait and see....
 
Well said mkubwa.......!

Yaani huko bagamoyo macho yake manne ndo yameona ubnadhilifu serikalini? yaani pale mgogoni penyewe hajauona uozo huo? .....shame on him aiseee.....!

Sitetei wouvu wowote, bali mto huo inatakiwa aureplicate na kwa grand corruptions kama zile za Richmonduli, EPAs etc!...sio kukimbilia hao wasiokuwa na ''kinga'' tu........!

Na nyie mmezidi bwana, hakuna zuri kwenu? Mlitaka awaache hata kama wamekosea? Ni vizuri pia mjue kwamba Pinda siyo Rais, ni Rais pekee mwenye mamlaka ya kumtimua yeyote katika nafasi yoyote. Lakini si waziri mkuu anayeweza kumfukuza Ndulu. Ya kupongeza tupongeze, na ya kuponda tuponde. sasa nyie yote mnaponda tu, kwani nyie wapinzani?
 
Habari tulizozipata muda mfupi ni kwamba maofisa sita wa Halmashauri ya wilaya bagamoyo wametimuliwa kazi na WAZIRI MKUU mh. Pinda leo hii.kwa kosa la ubadhirifu wa mali ya umma,na kutojali kero za wananchi.
wadau mnasemaje katika hili? maana huko ndio kwa mh. RAIS- JMK.
toeni maoni. maana wapo wengi sana wa mfano huu,katika maharmashauri hapa nchni.

Ayafanyie kazi basi na mapendekezo ya kamati ya Mwakyembe maana amekuwa akiyakimbia kwa muda mrefu sasa.
 
Well said mkubwa.......!

Yaani huko bagamoyo macho yake manne ndo yameona ubnadhilifu serikalini? yaani pale mgogoni penyewe hajauona uozo huo? .....shame on him aiseee.....!

Sitetei wouvu wowote, bali mto huo inatakiwa aureplicate na kwa grand corruptions kama zile za Richmonduli, EPAs etc!...sio kukimbilia hao wasiokuwa na ''kinga'' tu........!

Mkuu si walishatuambia hao wa EPA ni matajiri wakubwa nchini wakikamatwa au kuchukuliwa hatua basi nchi itawaka moto na wao hawataki kuiwasha nchi moto kwa hiyo ni bora hao wa EPA waachiwe wapete tu lakini watalala mbele na hivi vidagaa, lakini mapapa hawataguswa.
 
Habari tulizozipata muda mfupi ni kwamba maofisa sita wa Halmashauri ya wilaya bagamoyo wametimuliwa kazi na WAZIRI MKUU mh. Pinda leo hii.kwa kosa la ubadhirifu wa mali ya umma,na kutojali kero za wananchi.
wadau mnasemaje katika hili? maana huko ndio kwa mh. RAIS- JMK.
toeni maoni. maana wapo wengi sana wa mfano huu,katika maharmashauri hapa nchni.

Mbona hao mafisadi papa hawagusi bana? Kama ana nia ya uongozi afanye kweli kabla ya uchaguzi kuondoa takataka zote za wahujumu uchumi akina Vijisenti, EPA, Dowans, et al. Sio hawa dagaa kutoka Ziwa Tanganyika.
 
Hawajatimuliwa...ila wamesimamishwa uchunguzi ufanyike,kama watakutwa na hatia wataadhibiwa kama vinginevyo wanarudi kazini na fidia juu..tatizo sio ubadhirifu DC na DED walikuwa hawasalimiani kwa hiyo wakikubali kusalimiana yanaisha
 
Jamani ukifukuzwa kazi serikalini wewe umeshindikana. Maana serikalini watu wanaonywa sana.

Private sector kosa moja nje,hakuna masihara hata kama kosa ni dogo sana. Tatizo serikalini kulundana kwingi sana.
 
Na nyie mmezidi bwana, hakuna zuri kwenu? Mlitaka awaache hata kama wamekosea? Ni vizuri pia mjue kwamba Pinda siyo Rais, ni Rais pekee mwenye mamlaka ya kumtimua yeyote katika nafasi yoyote. Lakini si waziri mkuu anayeweza kumfukuza Ndulu. Ya kupongeza tupongeze, na ya kuponda tuponde. sasa nyie yote mnaponda tu, kwani nyie wapinzani?

Kama mtazamo wako ni huo basi inabidi upewe ushauri nasaha!! Kwa hiyo wewe unataka watu wote wawe na mawazo sawa. Kwani sote tuko kwenye ile 70% ya wafuata upepo kama wewe? Naona uko JF kimakosa au umetumwa. Vinginevyo usingeweza kuandika kitu kama hicho kwenye hili jamvi!
 
Habari tulizozipata muda mfupi ni kwamba maofisa sita wa Halmashauri ya wilaya bagamoyo wametimuliwa kazi na WAZIRI MKUU mh. Pinda leo hii.kwa kosa la ubadhirifu wa mali ya umma,na kutojali kero za wananchi.
wadau mnasemaje katika hili? maana huko ndio kwa mh. RAIS- JMK.
toeni maoni. maana wapo wengi sana wa mfano huu,katika maharmashauri hapa nchni.

Pinda amesema kuwa wametumia report ya CAG ya 2008 ambayo ilionesha kuwa wameshindwa kuthibiti matumizi ya pesa i.e wanatumia vibaya pesa za halmashauri. Kwani CAG aliitaja Bagamoyo peke yake? Nadhani kuna mambo zaidi ya hilo. Haiwezekana ufisadi ufanywe na kila idara ya serikali lakini wawajibishwe Bagamoyo tu!
 
Back
Top Bottom