Hivi ni lini mtakaa chini na kukubali kuwa serikali hii yote imeoza pamoja na CCM yao?
Nakubaliana na wewe mkuu asilimia mia, sioni mtendaji aliye bora na mwadilifu katika serikali hii - kwa ufupi tu CCM na serikali yake imeoza.
Tatizo la watanzania wagumu wa kuelewa na wepesi wa kusahau.
- mkaambiwa maisha bora kwa kila mdanganyika
- juzi mkaambiwa kilimo kwanza
- KAGODA mzimu usiojulina kabisa, ( kiumbe kisichoishi)
- juzi bungeni wakakaa kama makada wa CCM wakalimaliza la richard monduli - nani aliyekuwa
analipwa sh 152m kwa siku hadi leo hajulikani.
- Rada hadi serikali nyingine inachunguza kwa niaba yetu na kugundua kulikuwa na rushwa ila sisi
raha mustarehe - eti tunasubiri riport itoke "ungireza bungeni kwao" kwanza ili tuanze uchunguzi.
- sasa wameanza kusafishana majimboni kuelekea uchaguzi mkuu - mweee!! nitatapika nimikunywa chai
asa ivi.
yote haya na mengine mengi tu ndugu zangu hamuungani ya waberoya kwamba CCM na Serikali yao wote chungu kimoja? - wameoza? - fikeni pahala mseme " YATOSHA"