Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Geophrey Pinda amesema ataunda timu ya wataalamu kufanya utafiti kuwabaini wamiliki wa mashamba ikiwa ni jitihada za kutatua migogoro ya ardhi wilayani Kiteto pamoja na mgogoro wa mpaka kati ya wilaya hiyo na Wilaya ya Chemba.
Naibu Waziri Pinda ameyasema hayo Februari 15, 2024 wakati akizungumza na umati wa wananchi wa wilaya hizo mbili katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Ndareta na kuhudhuriwa na Kamati ya Usalama ya Wilaya ya Kiteto ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya, Remidius Mwema.