Pinda:Mpaka wa Tanzania na Malawi una utata

Pinda:Mpaka wa Tanzania na Malawi una utata

Sheria za kimataifa mpaka kwa kwenye maji kawaida unapita 12 kilometers from the land (kama inawezekana) au katikati ya hayo maji. Inasemekana Nyerere aliwahi waambia hao akina Kamuzu kuwa kama mpaka upo kandokando ya ziwa Nyasa basi wayazuie maji yao kugusa nchi yake! Sarcastic statement showing the absurdity of the Malawian claim.

Watu wote wa Mbamba Bay, Liuli, Matema Beach, Manda, etc wakiingia tuu kwenye maji wamevuka mpaka! Absurd, if you ask me.

Hizi kauli za Mwalimu ni nzuri kuliko uzuri wenyewe na ndio maana wakati wake hatukuwa tukisikia habari hizo za mpaka. angalia sasa hata wahindi wanatutengenezea ramani zinazoonyesha kuwa Ziwa Nyasa lote lipo Malawi na bado tunawaacha tu. Huu ni uzandiki na mahala pao ni AIDHA Ikwao India au Ukonga
 
hawa nao wana matatizo!! utata umeanza tangu enzi za Banda! na huko huko Bungeni wamejadili miaka nenda rudi.

Tatizo lilianza na waingereza. Nasikia kwa sababu za kiutawala wakaamua ziwa lote pale linapopakana na Tanganyika liwe chini ya administration ya Federation of Rhodesia and Nyasaland. Mpaka wa Tanganyka na Nyasaland uwe beach ambayo inamaanisha kuwa wanyasa wakitaka kwenda kuvua samaki au kuoga ziwani wanaingia katika nchi nyingine! Hii haikuwa na matatizo wakati wa muingereza maana sote alikuwa anatutawala. Tatizo lilijitokeza mara baada ya Tanganyika kupata uhuru na baadae Nyasaland nayo kupata uhuru na kufanya ziwa liwe katika milki ya nchi mbili tofauti. Ni uzembe tu kukaa zaidi ya miaka 40 bila kujaribu kutatua tatizo hili once and for all. Kwa sababu watanganyika halafu watanzania wamekuwa wakilitumia kwa zaidi ya miaka 4o bila kuzuiwa na mwenye ziwa basi kama law of tort inafanya kazi katika masuala kama haya, hilo ziwa ni letu sote, Malawi na Tanzania.

Amandla........
 
Point utata wa mpaka hauna manufaa kwa mwanachi leta issues tatizo la usafiri ktk ziwa nyasa. Sio meli ni maboti toka enzi za mkoloni na yamechoka kwelikweli. Unapotaka kusafirisha mizigo unatozwa mara mbili hizo ni baadhi ya kero za hilo ziwa kwa mwananchi.
 
We are in the second month of the second decade of the 21st Century alafu serikali ya Tanzania na hawa wanyasa wanashidnwa kukubaliana kuhusu hili ziwa wanfanye GPS mapping wagawane hilo ziwa rather than kusema katikati ndio mpaka wakati maji yana evaporate..lol

Kinyambiss for President 2020. We will fix all this
 
Back
Top Bottom