Pinda, Muungano, na Hatima ya Zanzibar

Kama hamuutaki muungano si muondoke tu! mnanang'ania nini? kama ni serikali mnayo maneno mengi machafu kwa Pinda aliyewaambia ukweli ya nini?

Thubutu, wana ubavu ? Mnasahau kuwa ilibidi Mjaluo kutoka Uganda, Field Marshall John Okello, aje awanasue kutoka mikononi mwa Sultani. Safari hii, mmmh sijui - labda mjukuu wake Okello atokee !!
 
Kwani hapo 1964 April Baba yako wa taifa Nyerere alipokuja kumuomba Sheikh Abeid A. Karume alikua kalewa hakujua kua znz ni kama ka-mkoa kadogo tu cha Tanganyika? Wewe labda ni katoto kadogo tu huelewi nini kilimfanya Nyerere kungangania kuungana na znz. Braza mpini wa muungano munoa nyinyi huko bara, iwapo hamziwezi terms & conditions za muungano munaweza mukawacha kamba lakini mambo ya kukaa kinda la mkulima kuwatolea maneno ya kilevi waungwana halitokubalika.
 
Mimi nilidhani wale wasiokubaliana na matamshi hayo ndio wanatakiwa kujitoa!!!!
 
Thubutu, wana ubavu ? Mnasahau kuwa ilibidi Mjaluo kutoka Uganda, Field Marshall John Okello, aje awanasue kutoka mikononi mwa Sultani. Safari hii, mmmh sijui - labda mjukuu wake Okello atokee !!
Mkuu,
Ujuwe unachokiongea ni uwongo wa wa ki-ccm waliokutia kasumba kuwa Wazanzibari walikuwa wamenasa mikononi mwa Sultan, Sultan aliepinduliwa alikuwa ni kiongozi wa kikatiba(ceromonial head of zanzibar state) mfumo sawa na ule wa Uingereza ambao waziri Mkuu ndo kiongozi wa serikali. Hili lilikubaliwa na vyama vyote vya ukombozi(ZNP&ASP) kule Lancaster house, hivyo sultani alikubaliwa na wazanzibar wenyewe na kama wangeona haja ya kutoendelea wangelitumia katiba hiyo hiyo kumuondoa. Alichofanya kibaraka Okello na askari wenzake wavamizi kutoka bara na Kenya ni kuipindua serikali halali ya wazanzibar iliyochaguliwa kwa shria halali za wakati huo. Uvamizi wa serikali ya Wazanzibar unaitwa Mapinduzi hauhusu chochote kinachoitwa ukombozi, zanzibar tayari ilishapata ukombozi wake kabla ya 1964 wakati bendera ya wakoloni wa Uingereza iliposhushwa na kupandishwa ya zanzibar huru.
Kilichofuatia ni uvamizi ambao hauwezi kufuta ukweli kuwa zanzibar ilishapata uhuru tokea December 10/1963.
 
Ebo waache makelele, si wapeleke hoja yao ya kutaka kujitoa kwenye muungano kwa vyombo husika, watu wengine bwana makelele mengi lakini vitendo ZIRO.
 
Kitu kimoja wanachonifurahisha wazanzibari ni umoja wao wanapotetea hoja wanazoamini zinalinda maslahi ya nchi yao, siku zote huondoa tofauti za itikadi za vyama vyao na kutetea hoja kwa nguvu zote wakati sisi bara hapo ungeona karibu wabunge wote wa CCM wanapinga kisa tu hoja imetolewa na mtu wa upinzani.
 
Wanzanzibar hawautaki muungano kisa wamenyimwa nafasi ya kujiunga FIFA.
Maneno meengi, hivi tukiamua hasa muungano basi na Wazanzibar wote warudi kwao, hata kama ana nyumba bara hawakuja nazo hizi, ni nani ataumia?. Kwanza watu wenyewe makeke meeengi hata Milioni hawafiki. Kama wanataka Unguja na Pemba zijitenge basi wavunje muungano.

Hawa watu sisi wa bara tunalipa kodi wao wapata ubwete tu, umeme ulikuwa bure, maji bure, Bara wengine wanamajumba na maduka kibao ya nafaka tukisema warudi kwao watakubali hawa.

PINDA OYEEEE! Futa SMZ kumaliza kidomodomo cha wala urojo kwa chapati za maji.
 
Sasa Braza unajua kua hawa watu ni wachapa kazi, wamekuja mikono mitupu na sasa wana majumba na manduka kibao, waliwakuta kwenye vibanda na mabaa tu, hajawahipo kukamatwa jambazi m-zenji bara. Wa-zenji ni kweli wanakula urojo kwa gole ukiwa hujui jina lake si chapati za maji, kwa sababu zenj Ugali na maharage ni chakula cha wafungwa na mental hospital. Kwa hivyo Pinda akija kutafuta matibabu zenj hatapata tabu kwa mlo.
 

Wewe labda ulisimuliwa, mimi nilifuatilia. Hata utawala wa Afrika Kusini ulikuwa halali kikatiba. Shukhuruni bara kwa kuwakwamua kutoka utawala wa Field Marshall Okello, mwenyekiti wa kwanza wa Baraza la Mapinduzi.



 
Wewe labda ulisimuliwa, mimi nilifuatilia. Hata utawala wa Afrika Kusini ulikuwa halali kikatiba. Shukhuruni bara kwa kuwakwamua kutoka utawala wa Field Marshall Okello, mwenyekiti wa kwanza wa Baraza la Mapinduzi.



Pole,
Hii ndo historia uliyofundishwa ww na haoukaambiwa ndo wanamapinduzi(wauwaji mungu awalani huko waliko).
Okello hakuwahi kutawala Zanzibar badala ya uhuni aliufanya tunamshukuru Prof. Abdulrahman Babu with his UMMA Party intervention.
 

Tumewalea angalau mmefikisha vimiaka 45, badala ya kushukuru mnalalamika! Mshukuruni sana John Okello, maana Waarabu hawapendi sana watu weusi, mngeipata fresh!
 
Mg3,
Ha, ha, ha, ha, maneno mazito haya. Kwangu mimi huyu Kheri ni muhuni tu, kama yeye anajiamini saana na yuko kwenye kamati kuu ya CCM, kwa nini asisubiri kwenye kamati kuu amvulie uvivu Pinda? Kama kweli wazanzibar wameamua wanaogopa nini kusema hatutaki muungano? Mnakumbuka hotuba ya JK kwa wabunge wakati alipokuwa anaelezea kuhusu kama zanzibar ni dola au lahh, aliwapasha tena na kuwaambia zanzibar si dola kwa nchi za nje, na akawaambia tatizo nini kama kuna kitu si waseme tu. Wazanzibar kuweni open hamna anayewazuia, na mnatakiwa mjue wabara sasa wamechoka na kelele za kike za jikoni.
 
Bado mnatapa tapa.
SMT is barking dog which can never bite.
kama wanashindwa na mafisadi na wahindi sita tu watawaweza wazanzibari.
Msilete hoja zilizokuwa hazipo, mambo ya kuvunja muungano hizo ni hadithi za Pinda na umbumbumbu wake wa kukwepa hoja kuwa "zanzibar ina haki ya kusimamia mambo yake yasiyokuwa ya muungano na ndivyo mkataba wa muungano na katiba zinavyosema" yeye anakwepa hayo analeta hadithi za kimwituni mwituni, huyu Pinda alikuwa usalama gani wa taifa mwenye akili tope tope anashindwa hoja nyepesi kama hizi, arudi katika mkataba wa muungano, asilete vitisho vya kipuuzi, zanzibar haijawahi kulalamika njaa kabla ya muungano na wala haitalalamika njaa badala ya muungano. kama kanuna wazanzibar kuwa na serikali yao na yeye yake haiyoni ya tanganyika, hilo si tatizo la wazanzibar, amlaumu Nyerere. Pinda aache chuki zake kwa wazanzibar kama anaumwa na imani yake hatuwezi kumsaidia, huo ugojwa wake mwenyewe.
 
Tumewalea angalau mmefikisha vimiaka 45, badala ya kushukuru mnalalamika! Mshukuruni sana John Okello, maana Waarabu hawapendi sana watu weusi, mngeipata fresh!
Nasisitiza tena shule muhimu.
 
Junius,
Fikiri na tafakari kabla ya kuandika, kama viongozi wa bara wanaimezea saana zenj, nitajie au tutajie kiongozi wa bara aliyekimbilia kujenga na kukaa zenji?
Wanzibar mu wachovu wa kufikiri mno, na msitake mtake mtaendelea kutawaliwa tu, kama bara ikiondoka then waarabu wanarudi ku watawala, mu wavivu wa akili na hata kufanya kazi.
 
Inawezekena unachokisema kinalingana na "uchovu wa akili" yangu, lakini wasiwasi wangu ni "udumavu wa fikira" zako kuwa vingozi wako wa bara hawataki kuimeza zanzibar kwa kuwa hajajenga nyumba za kukaa huko na wala hawakai huko,Mungu atakufunua utajuwa. Ndugu yangu viongozi mafisadi wa SMT hawana haja ya kujenga Zanzibar kama wasivyokuwa na haja ya kuiba fedha za walipa kodi na kuziweka BOT na badala yake zinawekwa visiwa vya Jersey na benki nyengine za ulaya huko, hawana lazima ya kuhamia na kujenga wanakohifadhi fedha za wizi na ndo hivyohivyo hawana lazima ya kujenga na kuhamia walipoweka mirija yao ya unyonyaji zanzibar, katika vyanzo vyake vya mapato. Sina haja ya kukutajia kiongozi yeyote mwenye chochote kule zanzibar lakini ujuwe tu sehemu ya fedha zako unazolipa kodi zinazofisidiwa na hao unaowaita viongozi wako(kina Pinda na wenzake) zinawekezwa katika miradi mikubwa ya hoteli za kitalii na kampuni za uwakala kule zenj, nyengine wakimiliki viongozi wako ambao nikikutajia hutaamini kwa uchamungu wao na uadilifu wao, ambao mpaka bungeni wanasafishwa kuwa wasafi na wengine wanajisafisha wenyewe, mengine inamilikiwa kwa ubia na wafanyabiashara wa nje. Ukisikia viongozi wako wanataka Muungano udumu ujuwe si kwa maslahi ya kudisha udugu na mshikamano wa mimi na wewe bali kudumisha na kusalimisha mirija yao hiyo waliyoiweka huko na faida yake wakiihafadhi ukooo ughaibuni, ww mpiga kelele na muimba nyimbo za kuwasifu hupati chochote, unabakia kidumu!!!!kidumuu!!!Kidumuu!!
Nakweli kinadumu.
 

Hivi ni wewe, Marcus JUNIUS Brutus, uliyemsaliti Julius Caesar aliyekupenda kama mwanae hasa ukizingatia uhusiano wake na mama yako Servilia Caepionis? Au ni wewe Francis Bacon, Attorney General aliyemtosa rafiki yake kipenzi Robert Devereux, Earl wa Essex katika kutaka kujikomba kwa Malkia Elizabeth?

Leo hii unaubeza Muungano ambao serikali ya Zanzibar na Pemba iliingia kwa hiari yake? Unamlaumu Nyerere ambae ndiye pekee aliyempokea na kumpa hifadhi Sayyid Sir Jamshid Bin Abdullah Al Said na waziri mkuu wake Muhammad Shamte Hamadi alipokimbia kwenye meli yake iliyoitwa Seyyid Khalifa? Huyo huyo Nyerere aliyewaondolea John Okello ( raia wa Uganda ambae alitokea Pemba wakati wa Mapinduzi na alikuwa mwanachama wa ASP) ambae alitaka kuendeleza mtindo wa chinja chinja? Leo kweli mnambeza?

Unasahau kuwa hiyo nchi iliyoingia kwenye muungano na Tanganyika ni Jamhuri ya Zanziba na Pemba (sio Zanziba kama unavyotaka kutuambia) na kuunda serikali ya Tanganyika na Zanziba ambayo miezi sita baadae ikajiita Jamhuri ya Muungano ya Tanzania! Unasahau kuwa wakati mnapigiwa ving'ora, mnalazimishwa kuolewa na weusi wa huko kwenu mlipokewa na kupewa hifadhi huko mnakokulaani hivi sasa? Hata pale mlipomuua Rais wenu wa kwanza ni Nyerere huyo huyo aliyekataa kuwakabidhi wakina Abdurahman Babu akijua mlichotaka kuwafanyia. Ni Nyerere huyo huyo aliyewapatia mwokozi wenu Jumbe ambae hakuwa na ufuasi mkubwa katika Baraza la mapinduzi.

Mnasema hamkuridhia Muungano na ati Nyerere aliwarubuni! Unasahau ni Rais wenu ( ambae hakuenda shule) ndiye aliyempa likizo ya wiki moja Attorney General wake Wolfgang Dourado na kufuata ushauri wa mganda Dan Nabudere badala yake? Mwenzake alimtumia AG wake Roland Brown kuhakikisha maslahi ya upande wake. Hapa nani alaumiwe? Na ni Nyerere huyo aliyekataa Muungano wa jumla akisisitiza kuwa identity ya Zanzibar ni lazima ilindwe! Leo amekuwa muovu? Mnasahau pia kuwa kikatiba za nchi zao wakati huo, hao marais wawili walikuwa na haki kuingiza nchi zao katika mkataba wowote. Mnadai Baraza la Mapinduzi halikuridhia Muungano? Mbona Babu na Khamis Abdallah Ameir wamekiri kuwa ulijadiliwa katika Baraza na kukubalika baada ya Abdallah Kassim Hanga kuutetea kwa nguvu zake zote? Hanga huyo huyo mliokuja mnyonga baadae! Mnasahau kuwa mlikuwa na chama chenu cha ASP na ni kwa ridhaa yenu wenyewe mkakitosa na kukubali kuungana na TANU kuunda CCM mwaka wa 1977. Leo mnadai kubururwa na CCM, hamkuona hilo mlipoimba ngonjera kufurahia kifo cha ASP? Mnasahau kuwa hata katika kamati ya Nyalali, kwenye suala la Muungano ni wazanzibari watatu tu katika 11 waliotaka muundo wa serikali tatu na saba walitaka muundo uliopo uendelee. Wakati huo, watanganyika 9 kati ya 11 walitaka serikali 3 na ni wawili tu walitaka muundo wa sasa uendelee. Hao wenzenu si walijua maslahi wanayopata kutokana na muundo wa sasa na kama alivyosema Pinda, hasara mtakayopata ukivunjika ( na kila mmoja anajua kuwa muundo serikali tatu ni kituo tu katika safari ya kuvunja Muungano)!

Uvumilivu una mwisho na Pinda amewaambia msichotaka kusikia. Kama hamna haja na Muungano si heri mseme wazi badala ya kuendeleza malumbano yasiyo na tija. Si mna uwakilishi katika Bunge? Kwa nini maneno haya msiyasemee huko badala ya kubakia ambako hao mnaowabeza hawako?

Shule kweli muhimu. Msome hapa Profesa Othman aliyosema kuhusu huu Muungano
http://www.kongoi.com/forty-years-of-the-union-is-it-withering-away-by-prof.-haroub-othman-2.html . Na yeye hakuwatakia mema?

Nilikuwapo.

Amandla................
 
Last edited:
pinda katoa mawazo yake ni vyema kama kunahoja ya kupinga mawazo
yake isemwe kistaarabu badala ya matusi na kejeli.

hakika laana ya mafuta inatunyemelea.
 
Mimi ni admin wa mzalendo.net ambayo ni community website ya wazanzibari, tumepiga kura ya maoni juu ya muungano huu, na haya ndio maoni ya wapiga kura 80 (Clean votes hakuna mtu aliepiga zaidi ya mara moja):


  1. 46% hawataki muungano kabisa, wameshachoka kuburuzwa na kupotezewa utaifa wa visiwa vyao.
  2. 42% wanataka Serekali 3, Tanganyika, Zanzibar na Serekali ya Muungano.
  3. 7% hawataki mabadiliko wameredhika kabisa 🙄
  4. 5% wanataka serekali 4, Tanganyika, Unguja, Pemba na Muungano..
Suala la moja bila genocide ya kuwauwa wazanzibari wote, naona kama haiwezekani....suali muhimu kuna ulazima wa Tanganyika kumwaga damu kuhakikisha kuwa muungano unadumu?...😕

Aaaagh I forgot this was Pinda && Tanganyika's day dreams!

Cheers
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…