Mpita Njia
JF-Expert Member
- Mar 3, 2008
- 6,997
- 1,172
Elimu ni muhimu si kwa hao tuJamani shule kweli muhimu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Elimu ni muhimu si kwa hao tuJamani shule kweli muhimu.
Kama hamuutaki muungano si muondoke tu! mnanang'ania nini? kama ni serikali mnayo maneno mengi machafu kwa Pinda aliyewaambia ukweli ya nini?
Kwani hapo 1964 April Baba yako wa taifa Nyerere alipokuja kumuomba Sheikh Abeid A. Karume alikua kalewa hakujua kua znz ni kama ka-mkoa kadogo tu cha Tanganyika? Wewe labda ni katoto kadogo tu huelewi nini kilimfanya Nyerere kungangania kuungana na znz. Braza mpini wa muungano munoa nyinyi huko bara, iwapo hamziwezi terms & conditions za muungano munaweza mukawacha kamba lakini mambo ya kukaa kinda la mkulima kuwatolea maneno ya kilevi waungwana halitokubalika.Kwi kwi kwi, mie sioni tofauti kati ya Zanzibar nzima na mkoa mmoja tena mdogo wa Tanganyika.
Pinda kasema kweli na wengi ukweli hawautaki, ndio umoja na serikali moja, na zanzibar waendelee na serikali ya mitaa (madiwani n.k). Ajabu kweli, mbunge wa watu 3000-5000. Kweli mnainyonya Tanganyika, wabunge zaidi ya 50 badala ya 2 wawili tu stahili kwa pemba na unguja!
Kama hamuutaki muungano si muondoke tu! mnanang'ania nini? kama ni serikali mnayo maneno mengi machafu kwa Pinda aliyewaambia ukweli ya nini?
Mimi nilidhani wale wasiokubaliana na matamshi hayo ndio wanatakiwa kujitoa!!!!Kwani hapo 1964 April Baba yako wa taifa Nyerere alipokuja kumuomba Sheikh Abeid A. Karume alikua kalewa hakujua kua znz ni kama ka-mkoa kadogo tu cha Tanganyika? Wewe labda ni katoto kadogo tu huelewi nini kilimfanya Nyerere kungangania kuungana na znz. Braza mpini wa muungano munoa nyinyi huko bara, iwapo hamziwezi terms & conditions za muungano munaweza mukawacha kamba lakini mambo ya kukaa kinda la mkulima kuwatolea maneno ya kilevi waungwana halitokubalika.
Thubutu, wana ubavu ? Mnasahau kuwa ilibidi Mjaluo kutoka Uganda, Field Marshall John Okello, aje awanasue kutoka mikononi mwa Sultani. Safari hii, mmmh sijui - labda mjukuu wake Okello atokee !!
Sasa Braza unajua kua hawa watu ni wachapa kazi, wamekuja mikono mitupu na sasa wana majumba na manduka kibao, waliwakuta kwenye vibanda na mabaa tu, hajawahipo kukamatwa jambazi m-zenji bara. Wa-zenji ni kweli wanakula urojo kwa gole ukiwa hujui jina lake si chapati za maji, kwa sababu zenj Ugali na maharage ni chakula cha wafungwa na mental hospital. Kwa hivyo Pinda akija kutafuta matibabu zenj hatapata tabu kwa mlo.Wanzanzibar hawautaki muungano kisa wamenyimwa nafasi ya kujiunga FIFA.
Maneno meengi, hivi tukiamua hasa muungano basi na Wazanzibar wote warudi kwao, hata kama ana nyumba bara hawakuja nazo hizi, ni nani ataumia?. Kwanza watu wenyewe makeke meeengi hata Milioni hawafiki. Kama wanataka Unguja na Pemba zijitenge basi wavunje muungano.
Hawa watu sisi wa bara tunalipa kodi wao wapata ubwete tu, umeme ulikuwa bure, maji bure, Bara wengine wanamajumba na maduka kibao ya nafaka tukisema warudi kwao watakubali hawa.
PINDA OYEEEE! Futa SMZ kumaliza kidomodomo cha wala urojo kwa chapati za maji.
Mkuu,![]()
Ujuwe unachokiongea ni uwongo wa wa ki-ccm waliokutia kasumba kuwa Wazanzibari walikuwa wamenasa mikononi mwa Sultan, Sultan aliepinduliwa alikuwa ni kiongozi wa kikatiba(ceromonial head of zanzibar state) mfumo sawa na ule wa Uingereza ambao waziri Mkuu ndo kiongozi wa serikali. Hili lilikubaliwa na vyama vyote vya ukombozi(ZNP&ASP) kule Lancaster house, hivyo sultani alikubaliwa na wazanzibar wenyewe na kama wangeona haja ya kutoendelea wangelitumia katiba hiyo hiyo kumuondoa. Alichofanya kibaraka Okello na askari wenzake wavamizi kutoka bara na Kenya ni kuipindua serikali halali ya wazanzibar iliyochaguliwa kwa shria halali za wakati huo. Uvamizi wa serikali ya Wazanzibar unaitwa Mapinduzi hauhusu chochote kinachoitwa ukombozi, zanzibar tayari ilishapata ukombozi wake kabla ya 1964 wakati bendera ya wakoloni wa Uingereza iliposhushwa na kupandishwa ya zanzibar huru.
Kilichofuatia ni uvamizi ambao hauwezi kufuta ukweli kuwa zanzibar ilishapata uhuru tokea December 10/1963.
Pole,Wewe labda ulisimuliwa, mimi nilifuatilia. Hata utawala wa Afrika Kusini ulikuwa halali kikatiba. Shukhuruni bara kwa kuwakwamua kutoka utawala wa Field Marshall Okello, mwenyekiti wa kwanza wa Baraza la Mapinduzi.
![]()
![]()
Kwani kabla ya huo muungano ndivyo walivyokua wakijiita ? BRAZA WEWE NAONA KUA UNA UMRI AU UWEZO MDOGO SANA WA KUJADILIANA KWA SUALA LA ZANZIBAR. Kumbuka hizi ni nchi mbili zilizokubalian ( atleast naweza kusema Znz iliingia kwenye makubaliano ya muungano kwa nia nzuri) kuungana na znz ikaweka mashrti yake kua haitapoteze utaifa au serikali yake, hiyo ilikua 45 years ago na ikakubalika pande zote mbili, leo hii anakuja mtu aliopinda akili yake na kujisemea as if yuko mkahawani maneno hata huyo mwendazimu alioko mental hospital in znz angeliyasikia basi nina hakika siku hiyo angelikataa dawa na akasema sasa nimepona hii nafasi ndani ya hii mental hospital bora aletwe pinda na BUCHANA. Mimi kwa mtizamo wangu naona hii ni njama ya kuimaliza znz kwa wivu wa wadanganyika, Lakini znz ina Raisi wa kuchaguliwa kama wana wa CCM wanavyosema, sasa ikiwa amechaguliwa na wazanzibari kweli, basi wacha tumsikie msimamo wake. Na huyo bwana mikasi mwache akae kimya tu angoje muda wake kwisha.
Nasisitiza tena shule muhimu.Tumewalea angalau mmefikisha vimiaka 45, badala ya kushukuru mnalalamika! Mshukuruni sana John Okello, maana Waarabu hawapendi sana watu weusi, mngeipata fresh!
Inawezekena unachokisema kinalingana na "uchovu wa akili" yangu, lakini wasiwasi wangu ni "udumavu wa fikira" zako kuwa vingozi wako wa bara hawataki kuimeza zanzibar kwa kuwa hajajenga nyumba za kukaa huko na wala hawakai huko,Mungu atakufunua utajuwa. Ndugu yangu viongozi mafisadi wa SMT hawana haja ya kujenga Zanzibar kama wasivyokuwa na haja ya kuiba fedha za walipa kodi na kuziweka BOT na badala yake zinawekwa visiwa vya Jersey na benki nyengine za ulaya huko, hawana lazima ya kuhamia na kujenga wanakohifadhi fedha za wizi na ndo hivyohivyo hawana lazima ya kujenga na kuhamia walipoweka mirija yao ya unyonyaji zanzibar, katika vyanzo vyake vya mapato. Sina haja ya kukutajia kiongozi yeyote mwenye chochote kule zanzibar lakini ujuwe tu sehemu ya fedha zako unazolipa kodi zinazofisidiwa na hao unaowaita viongozi wako(kina Pinda na wenzake) zinawekezwa katika miradi mikubwa ya hoteli za kitalii na kampuni za uwakala kule zenj, nyengine wakimiliki viongozi wako ambao nikikutajia hutaamini kwa uchamungu wao na uadilifu wao, ambao mpaka bungeni wanasafishwa kuwa wasafi na wengine wanajisafisha wenyewe, mengine inamilikiwa kwa ubia na wafanyabiashara wa nje. Ukisikia viongozi wako wanataka Muungano udumu ujuwe si kwa maslahi ya kudisha udugu na mshikamano wa mimi na wewe bali kudumisha na kusalimisha mirija yao hiyo waliyoiweka huko na faida yake wakiihafadhi ukooo ughaibuni, ww mpiga kelele na muimba nyimbo za kuwasifu hupati chochote, unabakia kidumu!!!!kidumuu!!!Kidumuu!!Junius,
Fikiri na tafakari kabla ya kuandika, kama viongozi wa bara wanaimezea saana zenj, nitajie au tutajie kiongozi wa bara aliyekimbilia kujenga na kukaa zenji?
Wanzibar mu wachovu wa kufikiri mno, na msitake mtake mtaendelea kutawaliwa tu, kama bara ikiondoka then waarabu wanarudi ku watawala, mu wavivu wa akili na hata kufanya kazi.
Bado mnatapa tapa.
SMT is barking dog which can never bite.
kama wanashindwa na mafisadi na wahindi sita tu watawaweza wazanzibari.
Msilete hoja zilizokuwa hazipo, mambo ya kuvunja muungano hizo ni hadithi za Pinda na umbumbumbu wake wa kukwepa hoja kuwa "zanzibar ina haki ya kusimamia mambo yake yasiyokuwa ya muungano na ndivyo mkataba wa muungano na katiba zinavyosema" yeye anakwepa hayo analeta hadithi za kimwituni mwituni, huyu Pinda alikuwa usalama gani wa taifa mwenye akili tope tope anashindwa hoja nyepesi kama hizi, arudi katika mkataba wa muungano, asilete vitisho vya kipuuzi, zanzibar haijawahi kulalamika njaa kabla ya muungano na wala haitalalamika njaa badala ya muungano. kama kanuna wazanzibar kuwa na serikali yao na yeye yake haiyoni ya tanganyika, hilo si tatizo la wazanzibar, amlaumu Nyerere. Pinda aache chuki zake kwa wazanzibar kama anaumwa na imani yake hatuwezi kumsaidia, huo ugojwa wake mwenyewe.