Nakubaliana na hoja ya mafuta kama utavyoona chini kabisa ya maoni yangu. Lakini hapa katikati, nyinyi mnaojiita Wazalendo ambao mnaoniengua mimi katika listi yenu kutokana na baadhi ya vipengele vya maoni yenu, naombi mzingatie yafuatayo:
Sio kweli kwmaba Dola yetu ya Zanzibar ilivamiwa hapo usiku wa Januari 11, 1964. Bali ni Wazanzibari na Wazanzibara waafrika/weusi waliondosha "kwa bahati mbaya violently" utabaka. Utabaka uliojengwa chini ya utawala wa kisultani, waarabu, ambao kama kawaida wafanyavyo mpaka hii leo (angalia wanavyowauza kwa bei rahisi ndugu zao wa Palestine). Kiburi chao kinyume na uislamu waliwafanya makafiri (British) ndio protector wa utabaka wao. Hili la utabaka na kuwafanya makafiri protector ndio exactly Allah (SW) alilotukataza katika Qur-ani na Sunna za Mtumewe, Haramu safi.
Yaliyotokea siku ile ni haramu sio kwasababu kuwa utawala wa kitabaka wa waarabu uling'olewa, la hasha !!!. Bali ni kwasababu waislamu wa waislamu walimwaga damu, simple as that, ndio haramu. Kwanini ilifikia vile??? mtawala wa wakati ule ndio mas-uula kama nilivyooeleza hapo juu. Na kama nyinyi mnasema kuwa Wazanzibari na Wazanzibara kwasababu ni weusi/waafrika basi sio waislamu au makafiri , basi jiangalieni vizuri maana kauli au fikra za namna hii ni Allah mwenyewe ndie mjibuji na kuwaweka wahusika wanapostahili. Na kama mnasema sio wazalendo, basi mnarudi kule kulee, "kukaanga mbuyu kuwaachia wenye meno watafune". Mnatayarisha kidogo kidogo ili damu ije kumwagika tena huko mbeleni, iwe miaka mia au mia mbili ijayo lakini Mwenyezi Mungu atawafanya mas-uula kesho akhera.
Damu ilimwagika 1964 na likubalike hilo, na iwe mwisho kwa damu ya waislamu kumwagika tena katika visiwa vile. Hii itakuja kwa misingi ya usawa na haki sio kwa utabaka na kukumbatia makafiri (Masultani/Waarabu) au ufisadi, kiburi na kupalilia chuki baina ya watu(viongozi wa sasa wa CCM)
Watanganyika tegeni masikio!!! Mafuta na gesi na mali ya Zanzibar na kwa waZanzibari, si vinginevyo, kama ilivyo almasi ya Mwadui ni ya Tanganyika kwa Watanganyika. Kilichobakia ni kwamba Wabara kwa kutumia Muungano(angalia chini) wanataka kuendelea kuidhulumu Zanzibar. Pinda kwa kauli zake za vitisho na Watanganyika wengine, kwanini hamjali kuwa hakuna haja ya waZanzibari kudai haki hii violently? Ni haki yao.
Nani asiyejua humu jamvini kwamba Muungano una mashaka, anyooshe mkono. !!! Lakini Wabara wanajihisi kama vile wamekamata mpini na Wazanzibari wamekamata makali. Kila siku kubwabwaja tuuuu. Kwani hamjawahi kusikia nyie mke akimtia shoka mume anaemtesa, hivi huwa makosa ya nanai hivi???. Why is this Watanganyika? Kama mimi kesho niamke ndio raisi wenu, basi siku ya pili tu, Tanzania, kwa tamko, tamko rasmi ni nchi ya serikali tatu. Na kilichobakia hapo ni utekelezaji tu ambapo natoa miezi sita kwa kila waziri anaehusika na mambo ya Muungano kukamilisha, nataka kamili, sio nusu ofisini kwangu mfumo wa serikali tatu. Kila upande una haki yake safiii na Muungano una haki yake saafi ndani ya miezi tisa tu. Maana sisi tunajua maana na faida za Muungano, lakini huu haujakaa sawa huu. Mambo mengine yanahitaji Tamko rasmi tu na utekelezaji kufuata hatua kwa hatua kwa furaha na amani.
"Hakika milki ya utajiri bora ni kinaya" sio material wealth obtained from oppression.