Pinda, Muungano, na Hatima ya Zanzibar


Suwala linakuja hapa kuwa Uzanzibari si kuzaliwa Zanzibar bali ni ukaazi wa sehemu hiyo. Wazanzibari hawagombanii kuiondowa Zanzibar na kuiweka mbali na Bara hilo haliwezekani. SUALA hapa ni masilahi ya Zanzibar na wakazi wake . Hivyo tunategemea mkaazi wa Zanzibar akose huduma muhimu eti kwa sababu waliobara wanaamuwa maisha yao? Si mwenye damu ya Kiarabu, Kisukuma , Kizaramo au mkiristo au muislamu awepo pahala popote atakaeacha kutetea sehemu aliyopo iwe Mwanza, Kigoma, Pemba atakaeacha kuiteteyea sehemu anayoishi. Kwani hatuoni Wabunge wakigombana na mawaziri kutetea hadhi ya sehermu zao?
Ukiangalia kwa mtazamo huu ndio utaona wenye asili zote kule Zanzibar wanapigania Zanzibar na kwa bahati mbaya Serikali ya Muungano ni double Crosser. Inahubiri Utanzania kwa faida ya upande mmoja na kujivua madaraka ya upande wa pili katika masuala ya kuiendeleza Zanzibar. Wazanzibari wanahisi basi watumie kilicho chao (mfano mafuta) kujiendeleza. JEE WAUNGWANA HILO NI BAYA?
 
Mkira,
Jambo la kwanza wambie wajomba zako CCM waachilie uchaguzi wa haki na huru ili uone matokeo, hapo ndio utajua kua wa-zenj wanautaka muungano au la. Karume msimuonee jamani yeye hakuchaguliwa na wa-zenj amewekwa na kamati ya ccm Dodoma hili kila mtu anajua hata yeye mwenyewe, kwa hivyo usitegemee kua ana uwezo wa kuikataa amri ya ccm na waliomueka. Kwani Braza kweli haya ni mageni au hamyajui ? ZNZ haihitaji eti kwenda kwa Waarabu kwani waarabu wamo tayari ndani ya Znz infact ndani ya Ikulu, kwani huko bara hakuna waarabu kila mkoa. Mbona wewe wakuuma sana hawa waarabu? na pengine tukichunguza utaona lazima kapita / kaowa au kaolewa mwaraabu katika jadi zako. Wacha chuki na waarabu Marekani na nchi za ulaya ndio waliokua mbele kwenye ubaguzi wa rangi lakini haya huyaoni kwenye nchi za kiarabu. Tuulize sisi tunaokwenda Dubai kila wiki hal tunabaguliwa?
 
Kwa nini Visiwani wanakubali kuchaguliwa Raisi na CCM Dodoma?
Kwani huko Bara muna uhakika gani kama wananchi ndio waliomchagua kikwete? Au kwa sababu Kanisa ndio limesema kikwete ni chaguo la Mungu. at least visiwani wana uhakika na wanachokifanya isipokua uwezo wa kukataa kuchaguliwa rais ni mdogo. Hukumsikia Rais kikwete alipotembelea visiwani alivyosema ? Ati watu wa visiwani (ccm na cuf ) kazi yenu kwenye uchafuzi ni kutafuta wabunge na wakilishi , Raisi ni kazi yetu Dodoma. Braza yanayoendelea dodoma si mageni kwa wa-zenj.
 

Nini ushauri wako juu ya madini yanayotoka Bara na kuambiwa si ya Muungano?
 

Hii unayozungumza wewe ni double standard. Mbona Wabunge wanazungumza mambo ya Serikali ndani ya Bunge. Wawakilishi wanamakosa gani kuyazungumza mambo ya Zanzibar kwenye BUNGE lao?
Serikali inaposhindwa kutekeleza matarajio ya wananchi wawakilishi wa wananchi wana haki ya kudadisi na kuonya. SMT na miungano kwa ujumla unawaangusha Wazanzibari na hivyo wawakilishi wao wana wajibu wa kuyazungumza. Na hili Public limetoka wapi kwa mambo ya Taifa?
 

Haku8nana vikao halali vya kuzungumzia masuala ya Muungano zaidi ya Bunge na Baraza la Wawakilishi. Ustaarabu gani unaoutaka kutoka kwa viongozi wa Zanzibar huku unafurahia Wabunge wa Bara wakiiripua Serikali? Kwani kwa hili hakuna vikao rasmi? Sijui unaweza ukanieleza ni chombo gani chenye haki ya kuzungumzia Muungano zaidi ya Wananchi wenyewe na wawakilishi wao?
 
Achana na udaku wa kutawaliwa kiroho kama wakati wa ukoloni. Hivyo hiyo elimu haitaki kugharamiwa? Gharama itatoka wapi iwapo kuna wengine wanahodhi kile ambacho kingesaidia kuleta mtaji wa kutowa elimu. Mawanzo hayo ya kusema kuwa watu wasidai haki zao na badala yake eti watafute elimu yatawasaidia nini wanaonyimwa haki hata hiyo ya kupata ekimu?
 

Pengine ungeacha kejeli zako na kwenda huko ili ukaoshe macho pengine ungeweza kujuwa ukweli. Fahamu tu kuwa machinga mliowafukuza Bara wote wamehamia huko.
 

Aisee mbona unajidanganya. Kwanza Zanzibar haijataka kuvunjika Muungano, wanachotaka mafuta yao watumie wenyewe. Kwani sasa Muungano si upo na mafuta hayapo tatizo ni nini tena?

Ama hili la Zanzibar kupata chakula Bara hilo si tatizo. Una umri gani Bwana Mdogio? Wakati wa Karume Mkubwa hakukuwa na biashara hii ya chakula baina ya pande mbili hizi na Zanzibar ilinawiri na kuendelea. Aidha kipindi kifupi kilichopita miaka ya mwanzo wa 1980 Bara kulikuwa na njaa na umasikini wa paka kula mkia wake na Zanzibar ikinawiri. Wakati huo Zanzibar ilikuwa ulaya kwa Bara. Mambo yalikuja kubadilika pale ASP ilipovunjwa kwa hila na kuanzia hapo kuididimiza Zanzibar kulianza.
Nakuhakikishia kuwa leo kama Bara wataamuwa kuuvunja Muungano Zanzibar itaanza kunyanyuka tena kwa haraka kwani SIRI KUBWA YA MAENDELEO YA NCHI NI KUWA NA UWEZO WA KUJIAMULIA MAMBO YAKE YENYEWE na hichi ndio inayoitwa SMT inajaribu kuinyima Zanzibar.
 

Hivyo kabla ya kuja huu Muungano Wazanzibari waliishi vip? Hao wachache mnaowaonea choyo huko Bara hawawezi kuwafanya waliowengi wasidai haki yao. Hivyo mnawatumia hao kama kinga? Elewa kuwa hicho walichonacho kinawafaidia wao wakiwa huko kama nyinyi mlivyoenea nchi za watu kutafuta riziki.Wao wataamuwa kuishi huko au kurudi kwao kwani si watu kama Machupa wako tayari kuukana utaifa wao kwa kuangalia masilahi. Tunapozungumzia mambo ya Zanzibar tunakusudia masilahi ya wakaazi wa Visiwa vya Pemba na Unguja wakiwamo Wazaramo, Wanyamwezi, Wachaga na wengine wote waliotoka Bara ambao wanaishi Zanzibar
Hili la chakula kutoka Bara ni la kupangwa tu kwani chakula hicho hakiji bure bali kinanunuliwa hivyo kinaweza kununuliwa pengine popote ulimwenguni. Wazanzibari hawakuwa watumiaji wa vyakula vitokavyo bara wamejizoesha baada ya kukaa pamoja na ndugu zao wa Bara. Si kitu kigumu kuachana na magharage.
 

Wacha utoto wako. Hivyo mnashindiwa nini kuendeleza mikowa yenu na kukimbilia Zenj? Unataka kunambia kuwa mnakimbilia kufanywa manamba kule? Wazanzibari ni wavivu , maduka mnaendesha nyinyi sasa la kujiuliza pesa za matumizi mnatowa nyinyi na hayo maduka mnayoyaendesha mnayaendesha kwa mpango wa Cherity? Wallahi hujui unavyojitukana, eti unaacha kukaa kijijini kwenu wewe usie mvivu ukagombana na jembe badala yake unakimbilia Zanzibar kufanya umanamba. Unajitukana nafsi yako na wote wanaomtazamo kama wako na wala huwatukani hao wavivu wa Zanzibar.
 
bana eeeh!! mambo mengine kuosha vinywa tuu!! waache wajiungee yakhee! kwani shida iko wapi? wakifika FIFA wataambiwa nyie si mkoa wa Tanzania? sasa mnataka nini? labda kwa wakina OIC watawakubalia kwa sababu wavivu kufikiri!

Werevu husema thamani ya mtu inaonekana kwa mtazamo wake kwa ndugu yake.
 

Kutawaliwa bado kuko. Hata mtu akisahau rubega na kuifanya Suti ndio bwana ipo kazi.
 

Kwani huu mnauita Muungano si wa nchi mbili? Akili ya mtu asiepotoshwa na choyo ni kuwa atamsikiliza mwenzake na pasipo muwafaka mtatafuta wenye busara na hata hilo likishindikana basi lengo la umoja halipo tena na ni bora mtafute njia nyengine ya ushirikiano. Unapoona mmoja anatunisha misuli kumtisha mwengine basi pana mushkeli hapo. Nafikirikuna upande una hoja ya ubabe na kuna upande kuna hojua ya kuonewa kwani ubabe mwenzake ni kuonea alie dhaifu.
 
Poleni Ngekewa na Mwiba kwa uchungu wa kutawaliwa; lakini bado sijaona jawabu la kujinasua, ndiyo maana tunasema hiyo ni porojo tupu.
 
Vipo visiwa na nchi ndogo kuliko Zanzibar zilizostawi na hazijaungana na nchi yoyote.
 
Tatizo kubwa ambalo huwa naliona kwa watu wa kipande ile, ni kwamba katika kila argument wanayoleta wanasema wanapigania haki yao. HIVI HAKI YENU NININI? haki yenu ninini hata mnasema hivyo? hivi tz tunafaidika nini na hawa watu wasiofika hata milion moja? mbona mimi huwa nawaona ni kero tupu? kama muungano hawautaki, piga chini tuendelee na maisha kila mtu ya kwake. KITU CHA AJABU wazanzibar huwa wanafikiri watanzania wanaoishi bara wanawategemea kuwa bila wao hawawezi, kwa kifupu NI VIONGOZI WETU TU WANATUBURUTA, hata sisi hatuwataki kama nyinyi hamtaki kuwa pamoja na sisi. duniani kama mtu hataki kuambatana na wewe ni kuachana naye, na kama kuna kiongozi mwingine akiingia hapo nakwambia anaweza akawapiga chini ili muwe watu wa huko shelisheli labda. kama ni mafuta, hivi SIKU MKICHIMBA MAFUTA YAKAWA HAMNA, SISI HUKU BARA TUKACHIME HALAFU TUKAWAAMBIA TUNAVUNJA MUUNGANO mtajisikiaje? mbona akili zenu hazijakombolewa jamani?
 

AMA KWELI! Kwani lengo lenu kwa Muungano lilikuwa lipi? Umoja au kuhodhi cha wenzenu? Wazanzibari wanataka kutumia kilicho chao ndani ya Muungano. Huu uungwana wa kutishia kuvunja Muungano hautajenga bali kubomoa tru. Zanzibar ilikuwepo kabla ya Muungano na haikuwahiu ku7tegemea Bara kwa lolote sasa hali ikirudia kama awali haitokuwa tabu kwao. Kwani hamuoni mifano ya nchi zilizokuwa katika Muungano wa Urussi mbali ya kubanwa bado wanaendelea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…