CUF ndani ya Tanganyika je?
Tatizo la ,matatizo ya Tanzania sio CUF ,kama wewe unaona CUF ni Chama cha WaPemba au Waunguja,sina ubavu wa kukulazimisha usione hivyo ni wewe na akili yako kutokana na ufahamu ulionao. Kuna watu wanamaliza darasa la saba hawajui kuandika wala kusoma sasa inawezekana wengine wakamaliza kusoma wakawa wanajua kuandika na kusoma lakini hawafahamu ,si ajabu wewe ukawa mmoja wao.
CUF ni Chama Cha Siasa ,kama vilivyo vyama vingine na kwa idadi ya wanachama CUF ina wanachama wengi zaidi upande wa Tanganyika kuliko Zanzibar yote na vile vile ukifuatilia chaguzi kuu za Tanzania zote kama sikosei kura za CUF zilikuwa ni za pili.Hivyo usikae na kuzuka tu ukiandika bila ya kuona kule unakotoka ni wapi na kuna nini.
Wala usitegemee kuwa Muungano ukivunjika basi WaZanzibari watarudishwa kwao hilo haliwezi kufanyika kwa dunia ya leo na hata likitokea ,watakaofanya hivyo ni vibaka tu ,na sio serikali itakayokuwepo ,na pia litafanyika ikiwa bado serikali ya CCM haijataka kuachia madaraka ya Nchi.
Pinda amepindisha kwa sababu kuna mambo na hoja kibao ambazo zinamkabili yeye na serikali yake hadi leo hajazipatia ufumbuzi ,anahangaika nazo akienda huku akirudi ,hana jawabu zaidi ya kuwaambia wananchi kuwa mambo ni makubwa na yatahatarisha amani ya Nchi na zaidi hawana ubavu nayo ,kumbuka mambo ya mafisadi mambo ya madawa ya kulevya ,kauli walizozitoa ni za kukatisha tamaa kwa serikali ambayo wananchi waliweka tamaa ya maisha bora ,leo ni miaka mitani ni wapi kwenye dalili ya kumaliza na kuwafikisha wale wote ambao kila kukicha Raisi Kikwete na wenziwe walisikika wakisema majina tunayo ,sasa ikiwa majina wanayo na wanawajua inakuwaje hadi leo Jemedari Mkuu anashindwa kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria wahusika na badala yake analala na majina ya wadau wa unga na mafisadi ,pale bandarini Raisi alisema listi anayo ,sasa hata pale panamshinda kuchukua hatua kali ?
Hizi ni karata wanazocheza nazo wafuasi wa Sultani CCM ,:-
Mafisadi ,Maalbino ,matajiri wa kuagiza na kusambaza unga ,dini na muungano.
Mambo hayo huwa wanayachezea kwa nyakati tofauti na kuwahamisha wapinzani kutoka walipo ,tatizo vyama vya upinzani vinapoteza msimamo na kujiingiza kichwa kichwa bila ya kuelewa kuwa Sultani CCM anacheza na akili zao na kuwapoteza lengo ,hata ule mori wa wananchi kuwasikiliza wapinzani huwa unapotea.Na utawasikia wananchi wakiguna huku wakisema vyama vyenyewe vya upinzani havisikilizani wala havina msimamo.
Kama ni kuikamata CCM pabaya basi ni kuibana kote huko katika kila penye karata vyama vya upinzani ni lazima viwe na msimamo wa kupingana na CCM na si kuipa mwanya.
Hawa Serikali ya CCM inaongoza nchi kienyeji ,kila mmoja wao ni mbabe kumshinda mwenzake kuanzia huku Tanganyika hadi kule Zanzibar kila mmoja anasema anavyotaka akijua fika hakuna wa kumkataza wala kumuonya na akiteleza atalia na kutoa machozi ya mamba.
Hivi kauli ya vyama vya upinzani inahitajika sana katika mambo hayo hizo karata za CCM hapo juu ,ni muhimu sana kwa wakuu wa vyama vya upinzani mbali ya tofauti zao ni lazima wawe na mambo wanayokubaliana na si vinginevyo ,mambo ambayo yanaitatiza CCM hayo ndio mambo ya kuyatolea msimamo unaoipinga CCM ili uwepo upinzani imara.
Sasa tunataka kusikia msimamo wa Vyama vya upinzani kuhusiana na mambo makuu matatu ,kuhusiana na ufisadi ,kuhusiana na majina kukaliwa na Raisi na hili la kubanwa kwa Zanzibar kutokana na ukandamizaji wa Serikali ya CCM ya Muungano ,ni lazima upatikane msimamo ili kuiweka kona CCM na si vinginevyo.