Mimi huwashangaa sana watu wanaopenda kuniga tai kwenye nchi yenye joto kama hii yetu. Kwanza ni ushamba wa hali ya juu. Wazungu walibuni vazi hilo kutokana na hali ya hewa ya nchi zao ambako karibu mwaka mzima hali ya hewa ni baridi kali mno isiyoweza kueleweka kwa mtu anayeishi kwenye joto kama hapa kwetu. Sie Waafrika kwa kupenda kuiga mambo ya Ulaya na kudhani kwamba ndio maendeleo tunajikuta tunajitesa na suti. Si hilo tu, mtu akiniga hiyo suti ili kukimbia joto atahakikisha anakuwa na gari airconditioned na ofisi airconditioned etc. Matokeo yake anatumia fedha nyingi mno kugharimia manunuzi ya suti, gari airconditioned ambalo hutumia mafuta mengi kuliko kawaida, na huko ofisini atataka airconditioner inayotumia umeme mwingi. Mwisho wa yote ili kuweza kuzimudu gharama zote hizo itabidi mtu/afisa huyo ajiingize kwenye hujuma za rushwa na ufisadi ili aweze kulipia gharama hizo.
Kwa bahati nzuri nimewahi kuishi na Wazungu wanatucheka na kutudharau sana kwa tabia yetu ya kuiga mambo yao ambayo wala hayana mantiki kwetu sisi katika hali yetu ya umaskini.
Asante Pinda! Usife moyo, endelea, kazana kuwaelimisha wananchi na tunakuomba utumie rungu lako la Uwaziri Mkuu kusitisha mianya yote ya ubadhilifu ndani ya Serikali. Mungu atakuwa pamoja nawe!