..nadhani Pinda alimaanisha kwamba,kwa kiongozi anaetumia muda wake mwingi kuwaza na kupanga namna ya kuwaondoa watz kwenye umaskini walio nao, hana muda wa kuwaza habari za suti! utakuaje wewe kiongozi uko smart ilhali wale unaowaongoza wana midabwada??wakati wao kodi yao ndo inakupa huo ufahari??
Ni suala la kutumia common sense tu, namna ya kuco-ope na watu wa chini, ambao hawana uhakika na mustakabali wao kwa ujumla.
Kama nakumbuka vizuri wakati wa Budget ya 2009, State house wamepewa fungu la mavazi & viburudisho, mapesa mengi tuu
ni kweli mkuu huyu jamaa anaboa sasa,maana juzi katoa ya vx leo suti ,kesho,keshokutwa itakuaje mpaka atasema tule vyura na nyoka na minyoo badala ya kununua nyama,na hiyo nadhani ni safari yake ya pili kutoka.akisafiri tena kama mara kumi nadhani atarudi na story kama hizi mpaka tutakoma,na sasa nimeelewa kwanini vasco da gama anaenda yeye tu viwanja maana naona kaona huyu mtoto wa mkulima atamuaibisha maana ukulima wake mwisho,kawababaikia wachina mpaka kawagawia ardhi kwa mkopo sasa anakuja na story zisizoeleweka,hawa ndio viongozi wetu hawaInasikitisha sana kuona mtu akienda nje ya nchi tu basi anafikiri kila akionacho huko ni lazima alete bongo hata bila kutumia akili akakaa na kutulia. Ndio matatizo ya watu tuliosoma hapa bongo. Tukitoka nje kidogo basi tunaona kama vile kila kitu tunachokiona ni lazima tukilete home. Hivi huyu jamaa anafikiri hizo nchi za Asia ndio kioo kikubwa kwetu kuliko nchi zingine zote duniani? Hivi kila aendae nje akileta anayoyaona kuimpliment hapa bongo tutakuaje jamani? Kila alikoenda lazima alete maneno ya ajabu tu...kenya,india,indonesia ...arghhhhh!!!!
hapana mkuu hapa nakataa sidhani kama watu huko bongo huvaa suti kila siku?mara nyingi nimeona watu kuvaa suti maranyingi kunapokua na matukio muhimu yanayohitaji unadhifu,au mtu anaelekea ofisini na ana semina au mkutano na hata siku mojamoja unavaa tu kazini au hata kutoka sio mbaya,watu watavaa mabatiki kila siku?Mimi huwashangaa sana watu wanaopenda kuniga tai kwenye nchi yenye joto kama hii yetu. Kwanza ni ushamba wa hali ya juu. Wazungu walibuni vazi hilo kutokana na hali ya hewa ya nchi zao ambako karibu mwaka mzima hali ya hewa ni baridi kali mno isiyoweza kueleweka kwa mtu anayeishi kwenye joto kama hapa kwetu. Sie Waafrika kwa kupenda kuiga mambo ya Ulaya na kudhani kwamba ndio maendeleo tunajikuta tunajitesa na suti. Si hilo tu, mtu akiniga hiyo suti ili kukimbia joto atahakikisha anakuwa na gari airconditioned na ofisi airconditioned etc. Matokeo yake anatumia fedha nyingi mno kugharimia manunuzi ya suti, gari airconditioned ambalo hutumia mafuta mengi kuliko kawaida, na huko ofisini atataka airconditioner inayotumia umeme mwingi. Mwisho wa yote ili kuweza kuzimudu gharama zote hizo itabidi mtu/afisa huyo ajiingize kwenye hujuma za rushwa na ufisadi ili aweze kulipia gharama hizo.
Kwa bahati nzuri nimewahi kuishi na Wazungu wanatucheka na kutudharau sana kwa tabia yetu ya kuiga mambo yao ambayo wala hayana mantiki kwetu sisi katika hali yetu ya umaskini.
Asante Pinda! Usife moyo, endelea, kazana kuwaelimisha wananchi na tunakuomba utumie rungu lako la Uwaziri Mkuu kusitisha mianya yote ya ubadhilifu ndani ya Serikali. Mungu atakuwa pamoja nawe!
vazi la chu Eng_lai linauenzi vipi utamaduni wa mwafrika wakati limebuniwa china?mi naona ni yaleyale ya kupindaLusinde alisema "katika kipindi cha utawala wa Nyerere hata wakati nakwenda kujitambulisha katika nchi nilizowahi kuwa balozi, nilikuwa katika vazi la 'Chu Eng-Lai' ambalo kwa wakati huo lilikuwa kama vazi rasmi lililotoholewa kutoka China na hata picha zangu zote ukiziona utakuta niko katika vazi hilo kwa kulinda na kuenzi utamaduni wa Mtanzania" Imeandikwa na Salim Said, Leon Bahati, Arusha na Habel Chidawali, Dodoma
vazi la chu Eng_lai linauenzi vipi utamaduni wa mwafrika wakati limebuniwa china?mi naona ni yaleyale ya kupinda
Mbunge wa viti maalumu, Anna Abdallah licha ya kuunga mkono kauli ya Pinda, alishauri uwepo utaratibu maalumu wa mavazi ili kuepusha mkanganyiko kwa wananchi na hata watendaji serikalini.
Kwa upande wake, Balozi mstaafu ,Job Lusinde naye aliunga mkono kauli ya Pinda na kusema kuwa kiongozi huyo yuko sahihi.
...jamani hawa ndio viongozi wetu wanaotuingiza karne ya 21,mbona kazi tunayo!
Mkuu tell me youre not serious,kwanini wasinunue hayo mawvazi kwa mishahara yao?Hii ni kali ya mwaka,yani kuna fungu la mavazi na viburudisho specially kwa viongozi?Kweli nchi inaliwa mbele na nyuma,no wonder Rev.Kishoka kasema huu ni "Ukahaba"
JMushi1,
>Kweli nchi inaliwa mbele na nyuma<
Please, zionee huruma mbavu zetu!!!
Nd. Lamaprt,
Wewe ndio wakuzionea huruma mbavu zetu!
Maanake katika yote haya yanayozungumzwa kuhusu mzee wetu Punda wewe umeona huko kuliwa nchi yetu mbele na nyuma ndio kichekesho kikubwa sana!
Ama Watanzania tumekwisha jamani!!!!