Pinda yuko sahihi kuvaa suti ni gharama mno kwa uchumi wa nchi na ni kumaliza pesa za kigeni.Kwa nini na sisi tusivae nguo za batiki na vitenge zinazotengenezwa na viwanda vyetu na pamba yetu humu humu nchini.
Kuvaa nguo zetu wenyewe kungesaidia kupanua viwanda vya ndani,vya ushonaji n.k na mafundi cherehani wetu waliozagaa mitaani wangekuwa na soko la uhakika la kazi zao ambalo linachukuliwa na ready made suits za ulaya.Viwanda vyetu vikipanuka na wakulima watalima zaidi na hivyo kupata faida zaidi.Yako manufaa mengi tu ndio maana kiongozi wa Indonesia anapenda kuvaa bidhaa zake zizalishwazo nchini mwake hata kama si nzuri kama suti za ulaya.
Watu wa afrika magharibi na kati huvaa sana nguo za viwanda vyao si kuanzia akina baba,akina mama ndio usiseme hupenda zaidi hizo kuliko za ulaya hivi watanzania kuna nini kwenye vichwa? Afrika magharibi na kati watu wameamshwa sana kuvaa vyao Tanzania wasomi wazima hawaelewi wanamkalia kidedea prime minister wengine hadi kuthubutu kusema apimwe akili.Tanzania ruhusuni uraia wa nchi zaidi ya moja haraka kuna hawara yangu anataka kukimbia nchi kachoka ujinga wa Tanzania.
Kama kweli raisi a mawaziri ni wazalendo na wakareketwa wa nchi na bidhaa zake waanze kuvaa nguo za urafiki,karibu textile na kadhalika na viatu aina ya yeboyebo zinazozalishwa na viwanda vya Tanzania. Nasubiri kwa hamu siku nitakayoona Kikwete katinga mashati na suruali za kitenge cha urafiki halafu chini akamalizia miguuni kwa kuvaa yeboyebo za sh.elfu moja akienda kukutana na Obama halafu tuone kama Obama atamtambua kuwa ni Raisi wa Tanzania au la kwa kuangalia kitenge na yeboyebo.
.